Mhe Kisoda hapa umenena
Kuhama tim kwa kuwa wachezaji fulani wameondoka ni sawa na kuhiama familia yenu kwa kuwa dada yako ameolewa.
Arsenal itaendelea kuwa chama langu siku zote hata kama itashuka daraja achilia mbali kuondolewa kwenye top four, sio kitu mpira unadunda na hata huyo Man City nae anatafuta mafanikio ambayo Arsenal amekuwa nayo miaka nenda miaka rudi,
Kwanini tusijifunze kwa mashabiki wa Juventus na Newcastle ambao pamoja na timu zao kushuka daraja kwa vipindi tofauti lakini bado waliendelea kuishabikia timu na kwenda uwanjani kushangilia kwa nguvu zote.
Tatizo sisi tuna mapenzi ya mpira ule wa Simba na Yanga kwamba siku Simba aun Yanga wanacheza na Toto Affirca hakuna shabiki wala mwanachama wa timu hizo anayekwenda uwanjani hadi siku ya mechi ya Simba na Yanga ndio uwanja ujae
Ukipenda mpira ndugu zangu hata ukipita ukakuta ule wa mchangani unachezwa utasimama na kuutazama pasipo wewe kujua umesimama. Sasa kama mpira wewe ni mpaka siku ya Man U na Chelsea au Arsenal na Man U basi wewe sio mpenzi wa mpira ila mdokozi wa mpira
Nawasilisha