Arsenal wala hawakosi usingizi wa kwamba Fabregas ataondoka kwani wataweza kuingiza benki kiasi kisichopungua 40mil.
Haipingwi kwamba ni mchezaji mwenye intelligence na vision awapo uwanjani lakini kama atalazimisha kwenda Barcelona ambako ndio alikuwa anakuzwa kwenye kitalu chao Arsenal hawataweza kukaa mlangoni na kumzuia.
Arsenal wana wachezaji wengi wa kiungo kama Jack Randall, Jack Wilshere,Aaron Ramsey,Fran Merida, Denilson, Abou Diaby, na Barazite.
Hawa ni wachezaji ambao umri wao ni wastani wa miaka 19 na 21 ambao ni umri wa Fabregas.
Na kwa sasa Arsenal hawatakuwa na matatizo na wachezaji wa Afrika ambao mara nyingi huondoka kwenda Afrika kucheza Africa Nations Cup, kwa hio ikifika mwezi January ni Alex Song wa Cameroon na Emanuel Ebue tu ndio waafrika waliobaki Arsenal wataoweza kwenda huko ikiwa watachaguliwa na nchi zao.