Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Arusha: Afisa Upelelezi (Omary Mahita) akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Duh police shida ninj..ukute mtuhumiwa alikuwa akihojiwa kwa vipigo nasikia wanafanya hivyo wakati nijuavyo mtuhumiwa hawi keshakosa mpaka ithibitike mahakamani..naona hio sheria ingefutwa watuhumiwa wasiteswe kwa lolote kabla ya mahakamani..wenyewe wakamate kisha wapeleke mahakamani kwisha, labda kwa makosa yanayohitaji uchunguzi watumie njia zingine sio short cut ya vipigo mtu anaweza kubali kumbe sio ikija ushahidi mahakamani jibu hapana
 
Hii ya tuna fanya uchunguzi!!! tunafanya uchunguzi.!!
Ni ishara ya watu wenye utamaduni wa kutojiamini kwenye kufanya maamuzi.
Au ni namna ya kuhalalisha uovu uonekane halali, kwa kutuoa majibu ya uchunguzi miaka 3 ijayo.
wakati huo muathirika amekata tamaa ya kufuatilia madai yake.


Iko siku kutakua na ulazima wa kuunda tume ya kufuatilia uchunguzi unao chunguzwa.
Police to police
 
Afisa Upelelezi Wilaya ya Arusha Mjini, Omary Mahita anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumvunja mguu mtuhumiwa wakati wa mahojiano akiwa kituo cha polisi.

Askari huyo anatuhumiwa kumvunja mguu wa kushoto Peter Charles (21), mkazi wa Daraja II, jijini Arusha Juni 6, 2024.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Agosti 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia ofisa huyo wa polsi na kwamba uchunguzi umeshaanza na endapo atabainika kuwa na kosa, atachukuliwa hatua za kisheria.

"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.

Mwananchi
Hakuna kesi hapo. Mambo yataisha kimya kimya, kwa sababu ya kulindana! Na pia kwa sababu baba yake alikuwa ni kigogo ndani ya hilo jeshi.
 
Uwe raia mwema au mtu wa madili, epukana na kujipendekeza na polisi wa ktz. Kutana au changamana nao pale tu inapobidi na kulazimu tu basi . NB: tuepukane na kuvunja sheria za nchi kwa kutenda makosa ya jinai au madai ili kuepukana na kujichanganya kwenye 18 za polisi. Utaepuka mengi..
 
"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,” amesema Masejo alipozungumza na Mwananchi.
Tangu June 6 2024!
Hili jeshi ni uozo
 
Hii nchi inachekesha sana sio siri

Inspector wa Polisi anakiri hilo tukio limetokea na Wanamshikilia Askari huyo THEN anasema tena Uchunguzi unaendelea

Unaendelea ili wagundue nini tena?
Delay tactics
Jion anatolewa selo anaenda kulala kwake
Asubh anarud
 
"Ni kweli hilo tukio liko ofisini kwangu na tumeanza uchunguzi tangu Agosti 8, 2024 nilipopata taarifa kwa simu kutoka kwa ndugu wa huyo kijana akimtuhumu askari wangu kumpiga hadi kumvunja mguu,”
"Tumeanza uchunguzi"
"Nilipopata taarifa kwa simu"
"Kutoka kwa ndugu wa huyo kijana"
"Wakimtuhumu"
"Kumpiga hadi kumvunja mguu"
POLISI........POLISI.........POLISI.........
TUNA D 2 ........
 
Back
Top Bottom