ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Pale karibu na uwanja wa mpira NAIC ni nyumbani kwao( wazazi wao) kwa sasa anaishi mdogo wake. Aina maeda ni mwanafamilia, huyu mzee anaishi Nshupu ni njia ya dik dik, huko ndio amejenga kasri zake na wanae wanaoishi marekani.
Hii familia ni matajiri sana kaka yao mkubwa ndio alikua mayor wa kwanza wa arusha miaka ya 60
 
Kwa sasa hivi polisi wakijua una hela wanakutungia kesi, TRA wakijua una hela wanakubambikia kodi.

Labda huyo rais mpya awafunge speed gavana na raia wamsaidie.
Tuko tayari kuwafichua wahalifu wa nanna hiyo,Mama awapige spana kwani hao ndio wanawafukuza wawekezaji,na kuwafilisi waliojaribu kupiga hatua.
 
Askari wanakula rusha sana na wanabambikia watu kesi sana ila wanalidwa na mfumo wa serikali ambao hautoi nafasi kwa wananchi kusema ukweli na hakuna uchunguzi huru wa matukio hayo, Ni vyema sasa sheria hizi zikabadilishwa na kuhakikisha wananchi wanapata wanasheria wao na uchunguzi ufanywe na taasisi huru na si police.
 
Copenhagen umenichekesha sana Mkuu, hivi Timothy ni mtoto wa Profesa au mdogo wake wa Hardware??
 
Ikawaje sasa ulitoa mpunga au ulikomaa

Ova
 
Y
Pale karibu na uwanja wa mpira NAIC ni nyumbani kwao( wazazi wao) kwa sasa anaishi mdogo wake. Aina maeda ni mwanafamilia, huyu mzee anaishi Nshupu ni njia ya dik dik, huko ndio amejenga kasri zake na wanae wanaoishi marekani.
Yule mama maeda mwenye petrol station opposite na the arusha hotel wana mahusiano na huyu mzee??
 
Askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamefukuzwa kazi na maofisa wawili wa jeshi hilo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh100 milioni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi Aprili 29 ,2021 na kubainisha kuwa walipokea taarifa kuhusu askari hao Aprili 19, 2021 kwamba wameomba na kupokea rushwa na uchunguzi ukaanza.

"Baada ya uchunguzi jeshi limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi maofisa wawili kwa kuwa haliwezi kuvumilia tuhuma hizi,” amesema.

Amebainisha kuwa baada ya uamuzi huo hatua nyingine za kisheria zinafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Askari hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa Profesa Justine Maeda ambaye amewahi kuwa mshauri wa uchumi wa rais wa awamu ya kwanza, Hayati Julius Nyerere.

Wanadaiwa kuomba fedha hizo na kupatiwa baada ya kumpekua nyumbani kwake na kudai kukuta vipande viwili vya meno ya tembo vikiwa kwenye mzinga wa nyuki.

Profesa Maeda ameieleza Mwananchi Digital kuwa alitoa fedha hizo ili ajinusuru asifunguliwe kesi ya uhujumu uchumi kama alivyoelezwa na polisi hao.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawa askari wa Kizazi hiki, ukiona una Mali na Majambazi yamekutinga ni bora Mara 100 kukimbilia Porini kuliko kujisalimisha kwao..,
 
Hao polisi wenyewe mmoja wao kasanda
Huyo Prof kwanza anakuambia maisha yake
Yote hajawahi ona pembe wala ngz ya chui

Ova
🤣🤣🤣🤣 hajawahi kuona pembe wala ngozi ya chui duhh
Hata kwenye tv kweli mzee kaonesha msisitizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…