ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Waliosimamishwa inamaanisha nn, maana kuna kufukuzwa na kusimamishwa hapo[emoji848][emoji848]
 
hao waliofukuzwa wameonewa tuu...small fish...hawakukurupuka kwenda... walitumwa wakaweke then waliumwa wakakague na kumshika.....aibu yao......
 
Hataki attention ya wahuni.Ila many'angau wamemkwaruza.
 
Hii stori haijakaa sawa mara upelelezi bado , mara masuala ya kipolisi etc, pia haielezi wazi mtu anatoaje mihela yooote hiyo kirahisi namna hiyo Takokuru na polisisiem nao hawaelewani sijui yaani vurugu tupu. Ila kimsingi polisisieeem na wao hawajambo kwenye ishu za ubambikaji akiunganishwa na Biswalo Mganganjaa a.k.a Nusrat Hanje jela out Ubunge Jobo Nduuugway balaa.Unakuta mtu ana mbavu mbili eti anamiliki vogue only in Tanzania.
 
Sijui polisi wa bongo wanafundishwaga kumjaza kwanza mtu upepo kabla hawajamkandamiza au wanaambukizana tu hiyo tabia. Karibia polisi wote ukikutana nao kwenye tukio lazima wakupanikishe kwanza bila kujali wewe ndio mhalifu mwenyewe au upo tu eneo la tukio!
 
Tatizo kubwa ni njaa mkuu. Nadhani (sina uhakika) polisi ni moja ya makundi ya watumishi wanaolipwa mishahara midogo hapa TZ. Sasa kwakuwa wana mamlaka fulani ya kudeal na uhalifu ndio njia wanayotumia ili kupiga vi deal anagalau ku supplement mshahara kiduchu ili kujikimu.

Kwahiyo hili ni suala lenye mizizi ambayo inaanzia mbali. Ukiangali nchi zenye kujali askari wao na wana mishahara mizuri na posho nzuri huwezi kukuta askari anakula rushwa au kumbambikia mtu kesi.
 
Mzee wa watu alionewa bure,wale Ni majambazi na Ni matapeli,fukuza kazi funga jela maisha
 
Wanaochafua jeshi la Polisi ni ofisi za OCD kushuka chini ni mara chache sana kukuta uaminifu kwenye ofisi hizo nchi nzima, hata hao majambazi sugu wanaouliwaga ni watu kama huyu prof kama angegoma kuwakubalia hilo deal au angekuwa amewajulisha kwamba atawaumbua baada ya hapo lazima wangembatiza hilo jina la jambazi sugu.

Mfumo wa utoaji taarifa kutoka chini kwenda viongozi wa polisi ngazi ya juu hautoi nafasi ya kujiridhisha na taarifa zinazoletwa kwao kabla ya kuwaita waandishi wa habari kutangaza habari hizo.
Na kwa bahati nzuri tunao waandishi wasiojuaga kuhoji na kudadisi taarifa wanayopewa wao wanameza kama zilivyo na kwenda kucheua kwenye media zao hivo hivo.
Juzi Mambosasa kawaita waandishi kuongelea ukamataji wa wezi wa vipuri vya magari lakini wakati hui huo akamfokea mwandishi aliyetaka kujua upelelezi wa watuhumiwa hao umefikia wapi! Na mwandishi alishindwa kuendelea na swali nadhani kwa kuiona lockup inamnyemelea!
 
I'd , oc cid , Dto , Ocs a hao Saba wote wafilisiwe halafu wapewe kesi ya uhujumu uchumi meno ya tembo wameyatoa wapi ?
 
Wewe hujui kitu, hivi uliisha wahi kumiliki pesa? Hayo ya kubambikizwa kesi yatatokea kila siku .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…