ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

ARUSHA: Askari Polisi 7 waliombambikia pembe za ndovu Prof. Justin Maeda na kuchukua milioni 100 wafukuzwa kazi, Profesa afunguka

Kuna miaka ya nyuma majambazi walimvamia kwake wakamkuta na elfu hamsini tu baada ya kusearch sana. Walimmaindi kwa kumuwasha vibao kadhaa na kumpa onyo kali siku nyingine awe anakaa na hela nyingi nyumbani.
Jamani😀😀🙌
 
Ni mhuni tu huyo na tapeli mkubwa sana nchini sijui wale wajinga ni lini wataachana naye. Yeye huyo huyo Gwajiboy hakuona tatizo jamaa atoe rushwa kwa dhalimu ili aaiende lupango. Dhalimu kafa sasa anang’aka kuhusu ushauri alioutoa!!!
Kama Gwajima na uaskofu wake kakalia kiti cha ubunge alichokipata kwa dhuluma kwa kupitia kura fake ujasiri wa kumshauri mwenzake asitoe rushwa ataupata wapi?.
 
Kuna siku polisi walinikamata, wakawa wanataka kunibabatiza na kesi zao za kipuuzi.

Wakawa wanataka kunipeleka kituoni.

Nikasema sawa, si tatizo. Ngoja nimpigie simu mshua nimtaarifu mmenikamata watu nyumbani wapate habari nimekamatwa na polisi. Halafu mtawaeleza kosa langu ni lipi.

Wakaniuliza kwani mshua wako nani?

Nikawaambia mshua tu.Msijali.

Nikaona wanaanza kuogopa.

Wakang'ang'ania kumjua.

Nikawatajia.

Haraka sana wakaanza kujibaraguza basi nenda tu.

Nikasema hapa kama mtu hajulikani angelala polisi.

Siku nyingine tumekaa maskani Upanga.

Tunaona polisi kama 20 wametanda mtaani wanakuja.

Mimi nikawaambia madogo fulani tumekaa nao, nikasema hapa kama mtu hawezi kuongea nao hawa ajikate kabisa, hapa tunabaki wabishi tu.

Basi wakafika mpaka pale tulipokuwa.

Mmoja akaanza kusema "hapa mnafanya nini nyie?".

Dah, kosa. Jamaa mmoja akamjibu "Hivyo ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu?"

Ikawa kama mzozo. Watu wakasema hapa tupo nyumbani.Polisi wakaanza kuuliza mmoja mmoja, wewe unakaa wapi? Watu wanaonesha nyumbani hapo, nyumbani hapo.

Wakamfikia jamaa mmoja tuko naye maskani.

Wewe unakaa wapi?

Jamaa akajibu "Kwa Ben".

Polisi wakawa wanashangaa, wakauliza, kwa Ben? Ben gani?

Jamaa akajibu, Ben Mkapa huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani wewe unamjua Ben gani?

Hapo rais ni Ben Mkapa.

Askari wakastuka. Ikawa kama hawaamini.

Mmoja wao akawa kama anawanong'oneza, nikamsikia anasema "huyu namjua, nilikuwa namuona nyumbani kwa Mkapa pale Sea View kwenye lindo". Presumably wakati Mkapa akiwa Waziri.

Basi hapo hapo tukaona askari polisi walioanza kutuingia kwa inda wanabadilika mara moja.

Wakaanza kusema "mnajua wazee ni katika kufahamiana tu, hatukuwa na lengo baya, ni kufahamiana tu".

Nikasema hawa huko mitaa ya watu wasio na majina wanawakamata watu na kuwatoa upepo vizuri sana, bila kosa.

Bahati yao mbaya leo wamekutana na kisiki.

Ile maskani waliipigia alama kituoni kwao, waliambizana maskani hii msiguse, kuna mtoto wa rais anakaa hapo.

Haki ya kikatiba ya kila mtu ya kutosumbuliwa na kuchukuliwa hana hatia mpaka atakapopatikana na hatia inavurugwa na inakuwa privilege ya watu wenye majina.

mbona ni kama mlitumia nguvu na muda mwingi kujieleza!!!

ni kwamba mlikutana na polisi vilaza tu,vinginevyo mngekuwa wahanga.
kimsingi ukiwa mitaa ya kwenu hutakiwi kuwa na stori nyingi na hakuna wa kukuletea longo longo.
simply tu unaulizwa wewe nani??? unajibu mimi kiranga nakaa nyumba hiyo hapo kwa mzee kabudi,imeisha hiyo.
hakukuwa na kisiki kati yenu bali,wao ndio walikua vilaza.
 
Askari wa bongo njaa kali sana. Kuna siku wamenikuta maskani moja hivi usiku wakanidaka na kunipa kesi ya bangi.

Walianza kuniswaga kuelekea kituoni nikasema sawa twendeni, kituo hakikuwa mbali sana tukaanza kuelekea. Meter kama 200 kutoka kituoni ndio wakaanza kuniuliza nina shilingi ngapi waniachie nikawaambia sina hata mia, wananiambia weka simu bondi hapo dukani sisi tuchukue elfu hamsini nikakataa.

Wakasema wewe utalala sero leo na kesho asubuhi unaenda central nikawaambia poa. Tumekaribia kituoni wanaona sijalainika nikasikia "mfungue pingu mseng.e huyo aondoke zake".
huu ndio uanaume.

usilete ujuaji sana mbele ya askari na usitie unyonge,bali kuwa mtulivu wakati wote.
 
Polisi anaenda kumuingia mzee, halafu hajui mzee kasoma na RPC.

Polisi wanambambikia mzee kesi famba, mzee anavuta waya kwa RPC anamblast inakuwaje vijana wako wanafanya mambo ya aibu?

Watajuta.
si bora wasome wote!!!kwa miaka 77 hiyo unakuta kamfundisha siro,diwani ama DCI na anamjua.

hakuna kitu kibaya duniani ukiacha tamaa/umasikini wako uamue jambo.
utu na utashi vitajitenga nawewe kabisaa.
unambambikia mtu kesi ambayo unajua kabisa anaweza kushindwa na akaishia jela!!!!
sijui nyinyi atheist labda ndio mna akili hizi maana hamuamini katika superior powers.
 
Kwa wasiomjua huyu prof. Lile ghorofa pale Leganga ambako TRA wamepanga,NSSF etc ndio la huyo dingi.

Na lile jengo ambako Meru Community bank walikua wamepanga ni la mdogo wake huyo Prof.(ambako ndipo alipoenda kuomba hio mil 30 iliyopelea kwny ile rushwa ya mil 100).
Hao police kwanza inatakiwa watema pesa yote,rpc kajibu kirahisi sana hajaongelea kuhusu pesa kurudishwa sembuse nae kala mgao....police wote tabia zao ni moja
 
Mdude alipenyeshewa mtoto wa Ki-Iraq ana nywele hadi kwenye kitako. Kumbe amebeba vitu vyake Mdude akajipigia mzigo asbh wanazengo wanakuja na search warrant na kumnasa na drugs.... kabaki anashangaa kuja kuhamaki mtoto wa Ki-iraq kumbe ndo ameleta kimeo!!
huyo naye ni fala wa karne,unashinda kutukana watu halafu unaishi kama mbuzi!!!.

hakuwa hata anajua gharama ya anachokifanya.
 
Like Profesa Like Mdude Nyagali
[emoji23][emoji23][emoji1732][emoji125][emoji125]
 
mbona ni kama mlitumia nguvu na muda mwingi kujieleza!!!

ni kwamba mlikutana na polisi vilaza tu,vinginevyo mngekuwa wahanga.
kimsingi ukiwa mitaa ya kwenu hutakiwi kuwa na stori nyingi na hakuna wa kukuletea longo longo.
simply tu unaulizwa wewe nani??? unajibu mimi kiranga nakaa nyumba hiyo hapo kwa mzee kabudi,imeisha hiyo.
hakukuwa na kisiki kati yenu bali,wao ndio walikua vilaza.
Hatukufanya zaidi ya kujieleza hivyo, na kuwafundisha wao kwamba wakikutana na raia wajifunze kuanza maongezi kwa kuwasalimu kwa heshima.

Huko kwingine walijibabatiza wenyewe wakakutana na walichokitafuta.
 
Back
Top Bottom