mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Wanafunzi hao wanadaiwa kuiba madawati hayo kwa nyakati tofauti na kuwauzia watu watano ambao tayari wamekamatwa na polisi.
Akizungumza leo Jumatano Desemba 16, 2020 wakati akiwaadhibu watoto hao mbele ya wazazi wao na wanafunzi, mkuu huyo wa Mkoa amesema madawati hayo yana thamani ya Sh10 milioni na kwamba watakaohusika kuhakikisha yanapatikana mengine ni walioyanunua pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.
Mkuu wa shule hiyo, Nteles Lorna amesema walinzi wa shule walibaini wizi huyo baada ya kuona madawati yamepungua.
Chanzo: Mwananchi