Arusha: DC Kenani awachapa mboko wanafunzi 3 kwa tuhuma za kuiba madawati 108 na kuyauza kama vyuma chakavu

Arusha: DC Kenani awachapa mboko wanafunzi 3 kwa tuhuma za kuiba madawati 108 na kuyauza kama vyuma chakavu

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
viboko-pic.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi amewacharaza bakora wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Sinoni kwa tuhuma za kuiba madawati 108 ya shule hiyo na kuyauza kama vyuma chakavu.

Wanafunzi hao wanadaiwa kuiba madawati hayo kwa nyakati tofauti na kuwauzia watu watano ambao tayari wamekamatwa na polisi.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 16, 2020 wakati akiwaadhibu watoto hao mbele ya wazazi wao na wanafunzi, mkuu huyo wa Mkoa amesema madawati hayo yana thamani ya Sh10 milioni na kwamba watakaohusika kuhakikisha yanapatikana mengine ni walioyanunua pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Mkuu wa shule hiyo, Nteles Lorna amesema walinzi wa shule walibaini wizi huyo baada ya kuona madawati yamepungua.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanafunzi anaweje kutoka na dawati eneo la shule bila mlinzi kuona? Walinzi au Mwalimu mkuu ahojiwe vizuri.
 
apo ni sekondariii ...wakifika chuo na kumaliza kisha wakaajiriwa katika serikali ama makampuni binafsi ....itakuwa full upigajii

yaani ndani ya mwaka kijana ana miliki magari/mijengo etc
 
Rekebisha andiko, mara Mkuu wa Wilaya mara Mkuu wa Mkoa.

Mimi sijafuatilia mkasa huu kwa undani lakini nauita Shutuma, sidhani kama ni kweli kuwa wameiba madawati 108. Hayo ni mengi sana na ukizingatia ndio wapo kidato cha kwanza, itakuwa wameiba lakini sio yote hayo

Pia huyo kiongozi alipaswa aanze kuwachapa Walinzi wa shule kabla ya hao Wanafunzi.
 
Binafsi kama kweli hao wanafunzi wamefanya ivyo binafsi nawaona kama mashujaa Wa kuisaka chapaa. Ninahitaji niwajue sema madogo wanaonekana wanaipenda Hela so hata shule wameenda kupoteza muda Kiukweli. Madogo wanatakiwa waijue Tanzanite. Hao ni mabilionea kesho.

Mbona hao ma Dc ,director na serikalini wanapiga Hela kwa njia yao so dogo kula kulingana na kamba yake wanamchapa.alitakiwa apewe u waziri Wa madini ili asaini miktaba huku wakiwa kwenye towers na briefcase zimejaa madolari na mapaundi pia na mayuro ya kufa MTU. Yaani dogo anasainisha mktaba Wa madini mpaka mwisho Wa dunia jamani na sio miaka mia moja
 
Vizazi vya chuga huwa ni macho kwenye mapato tu hili liko damuni,wazazi wa hao watoto wawe nao karibu huko mbeleni ni shida hao.
 
Mkuu madogo walitakiwa wapewe vyeti vya ujasiri kabisa ama vya ufisadi. Huo ni ufisadi kama ule Wa Richmond tu ama pori tengefu
Mkuu una maana unataka fananisha na ufisadi ule wa 1.5 tr wa jiwe?
 
Wanafunzi wa kidato cha kwanza? Hao mnawasingizia tu, walinzi wa shule na walimu ndio wameyaiba, msitufanye wajinga
Vipi kama wamekiri kuyauza na wenzao wakatoa ushahidi. Na vipi kama waliokamatwa wamekiri kununua madawati kutoka kwa watoto hao. Kwanza wewe huna mtoto, unajua malezi ya watoto?
 
Najiuliza waliyabebaje mpaka kuyafikisha mtaani na kuyauza [emoji15]
Ukiwa na mwanao nyumbani utajisifu mwanangu ni mtulivu. Akiaachana na wewe hasa akiwa shule, siyo yule wa nyumbani.

Binti mmoja akisoma sekondari, wazazi wake walimpa sifa kuwa ni mtulivu zaidi ya sister - mtawa. Akiwa shuleni walimu na wanafunzi wote walimpigia saluti. Mtiifu na mwaminifu mfano wa kuigwa.

Lakini mimi niliwahi kumwona mazingira tata akifumuliwa marinda. Bila shaka asipate mimba. Aliniogopa na kunihofia nitatoa siri zake. Yeye na mpenzi wake waliniheshimu kupita kiwango cha heshima.

Hadi leo nimetunza tu siri yao na sasa amehitimu kidato cha nne na mpenzi wake yuko kidato cha tatu.

Haraka haraka huwezi amini kuwa form one anaweza kuiba madawati. Kiukweli hadi wawekwe hadharani lazima uchunguzi wa kina umefanyika na kubaini UKWELI wa jambo. Tuamini walifanya hilo.
 
Back
Top Bottom