Arusha: DC Kenani awachapa mboko wanafunzi 3 kwa tuhuma za kuiba madawati 108 na kuyauza kama vyuma chakavu

Arusha: DC Kenani awachapa mboko wanafunzi 3 kwa tuhuma za kuiba madawati 108 na kuyauza kama vyuma chakavu

Vipi kama wamekiri kuyauza na wenzao wakatoa ushahidi. Na vipi kama waliokamatwa wamekiri kununua madawati kutoka kwa watoto hao. Kwanza wewe huna mtoto, unajua malezi ya watoto?
Sina watoto? Kwani kuna daftari la usajili la wanachama wenye watoto humu? Mbona una harisha kupitia mdomo wako wakati makalio unayo? Vipi wewe?! We ukitandikwa nusu ya kufa hutakiri hata kama ni uwongo?

Hao walinzi na walimu wamechapwa bakora ngapi kwa kuruhusu watoto waibe madawati 108?! Walileta Fuso au walibeba kichwani? Imbicile , umenikera sana, eti unajua malezi ya watoto, bastard, wewe ndio unajua sio?!
 
Wanafunzi wa kidato cha kwanza? Hao mnawasingizia tu, walinzi wa shule na walimu ndio wameyaiba, msitufanye wajinga
Ww hujui Arusha watoto wa darasa la saba wanavuta bangi na hao form1 kuiba wala sitilii mashaka kwasababu ya mienendo ya kihuni ya watoto wa Arusha, na kuhusu walinzi naweza nikawatetea kwasababu kwanza shule nyingi za government hapo Arusha wanalinda wazee 60+
 
Ww hujui Arusha watoto wa darasa la saba wanavuta bangi na hao form1 kuiba wala sitilii mashaka kwasababu ya mienendo ya kihuni ya watoto wa Arusha, na kuhusu walinzi naweza nikawatetea kwasababu kwanza shule nyingi za government hapo Arusha wanalinda wazee 60+
Wamechapwa bakora ngapi kwa kuruhusu huo wizi? Waliruhusu vipi watoto wa form 1 wakaingia na fuso shuleni kuiba madawati 108? Au waliiba kwa kutumia mitutu ya bunduki?
 
Chuga kama chuga....
Macho kwenye fedha....
Hapo wameshaandikwa kwenye blackbook.
 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi amewacharaza bakora wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Sinoni kwa tuhuma za kuiba madawati 108 ya shule hiyo na kuyauza kama vyuma chakavu.

Wanafunzi hao wanadaiwa kuiba madawati hayo kwa nyakati tofauti na kuwauzia watu watano ambao tayari wamekamatwa na polisi.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 16, 2020 wakati akiwaadhibu watoto hao mbele ya wazazi wao na wanafunzi, mkuu huyo wa Mkoa amesema madawati hayo yana thamani ya Sh10 milioni na kwamba watakaohusika kuhakikisha yanapatikana mengine ni walioyanunua pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Mkuu wa shule hiyo, Nteles Lorna amesema walinzi wa shule walibaini wizi huyo baada ya kuona madawati yamepungua.

Chanzo: Mwananchi
Hizi shule za elimu bure zinatia simanzi sana, mpaka DC ana mamlaka ya kumchapa mwanafunzi
 
Nikiwa nasoma olevel kuna form one walivamia shamba ya karoti si kwamba waliiba yaani walivuna kabisa kabisa hakuacha kitu mpaka shule nzima tukaa kikao na mwenyekiti wa kijiji.. nikiwa form 3 kuna form 2 mmoja alikula ramani na mjomba wake wakavunja stoo wakaiba cement zaidi ya mifuko 50, pia ishu za kuja kuchukuliwa mwanafunzi na defenda ya polisi wakati tupo class nimeziona sana ...hiyo ndio arusha wala sishangai
 
Wamechapwa bakora ngapi kwa kuruhusu huo wizi? Waliruhusu vipi watoto wa form 1 wakaingia na fuso shuleni kuiba madawati 108? Au waliiba kwa kutumia mitutu ya bunduki?
Wewe nae ..!
Umeambiwa asilimia kubwa ya walinzi ni wazee.
Na tunajua wazee wengi wamechoka na kukosa umakini

Utawachapa wazee umri sawa na baba yako?
 
Hii issue ni ya kusikitisha sana. Yaani hao watoto hawajafikisha hata miaka 18, na tayari wamevishwa tuhuma nzito kama hizo za wizi wa madawati. Maisha yao yameishaingia dosari.

Najiuliza, huo wizi ulikuwa unafanyika muda gani? Jioni baada ya shule, au usiku mkubwa? Waliwezaje kuyahamisha madawati mengi kiasi hicho kutoka shuleni mpaka kwa mnunuzi ?

Kama wengi walivyoulizwa, je shule haina walinzi? Halafu, japo hawa wanafunzi ni wadogo kiumri, lakini wizi ni kosa la jinai. Hii kesi ilistahili ichunguzwe na Polisi ili ukweli ujulikane. Pia ningependa kujua msimamo wa idara ya Ustawi wa Jamii kuhusu hili suala. Pole sana wazazi wa hao vijana.

Kinachonikera mimi, ni kuona mkuu wa Wilaya ameamua kuwa mwendesha mashtaka na jaji/hakimu hapo hapo. Huyu wasipomuangalia, atakuja kuleta yale mambo ya Makonda kule Bandari salama.
 
Huyu DC anatamani sana kutrend, anataka kufanya kazi na makamera na mapichapicha, yetu macho! Nilifikiri bwana mkubwa kakataza utaratibu huu!

Everyday is Saturday................................😎
 
Wewe nae ..!
Umeambiwa asilimia kubwa ya walinzi ni wazee.
Na tunajua wazee wengi wamechoka na kukosa umakini

Utawachapa wazee umri sawa na baba yako?
Wachapwe ndio,si ndio utaratibu huo au? na hilo fuso liliingiaje hapo, au hao wazee ni viziwi, au walisukuma hilo Fusi?
 
Hili la wanafunzi wakora kuwepo mashuleni huwa lipo na halikwepeki,ishu ni udhibiti tu.Shule hukusanya wanafunzi wengi wenye tabia tata licha ya walimu kuwaweka katika mfumo mmoja wa malezi.Kuna mmoja alinyofoa swichi madarasa yote na kuzipeleka alipopajua,baada ya kubainika aliishia kufukuzwa shule ila aliendelea na masomo shule nyingine.Aliendelea na tabia ya ukora mpaka ukubwani,madhara yake amejeruhika vibaya katika tukio la ukora na kuishia kupoteza mkono.Ki ujumla shule huwa zina wanafunzi wa ajabuajabu na wenye tabia mbaya mpaka ukubwani hawabadiliki
 
Najaribu kuwaza nakosa majibu,hebu disii chunguza vizuri hapo shuleni
 
Back
Top Bottom