Iddy Mukuluu alikuwa na Gym yake pale Kaloleni na hapo ndio kundi zima lilikuwa linapigia matizi(Mazoezi) yaani akina Banjoo, Nyari, Gody Mollel, Wilbert n.k...Na Idd alikuwa na nguvu sana...yeye pamoja na Frank Mwamba wa Meru, yaani ni ile akikupiga ngumi huamki...
Huyo Hanny ni Mwembamba mrefu ila anapiga Karate vibaya sana...hata hawa wana HipHop kina LORD EYES na BOU NAKO walikuwa wakienda kutrain nao pale japo walikuwa machalii wadogo...so sio Wazembe wale
Kitunguu alikuwa Mtu wa silaha na aliuawa kwa risasi sio miaka mingi hata, na aliuawa akiwa kwa hawara wake pale Shangarai ndanindani, huyo mwanamke ni Mtu mzima Mjane alifiwa na Mume wake.
Yaani ilifika Mahala katika Masjid za Arusha, Masheikh wakihutubia wanasema kama walikufa Firaun, Sadick Mkindi na Idd Mukuluu wewe una ubabe gani mbele ya kifo? 🤣
Wakati tunakuwa ule mtaa wa Mianzini kushuka mpk Makao Mapya kuliitwa Mtaa wa KIBLA/QIBLAH kwasababa haikuipita siku 2 au 3 hakujaokotwa maiti kadhaa mpaka za Wakenya waliopokonywa magari...na hadi sasa bado hili jina lipo
Iko hivyo Sheikh na hiyo ndio Arusha, kwasasa nipo Zanzibar ila nimekulia mitaa hiyo katikati ya mji na kusomea hapo, napafahamu vizuri sana