Arusha: Je, kifo cha Banjoo (Abdilah Musa) ni ''auaye kwa upanga hufa kwa upanga''?

Arusha: Je, kifo cha Banjoo (Abdilah Musa) ni ''auaye kwa upanga hufa kwa upanga''?

😂😂 watu wa Arusha tumefurahi sana

Ila Nina shoga angu nimesoma naye alikua bwana ake 😂😂 yupo kulia Kwa status alimuambia amuombee awe na pesa mingi

R.I.P banjooo
Banjoo alikuwa mbabe kwa wanawake, wakila vitu vyake lazima nae awapige miti tena kwa nguvu, nilishuhudia akiteka mtoto wa kike kwa kushirikiana na wahuni wenzie na kumwiingiza kwenye gari yake aina ya R4 na kwenda kumpiga miti. Nae ametekwa hivyo hivyo kwa mazingira hatarishi
 
Banjoo alikuwa mbabe kwa wanawake, wakila vitu vyake lazima nae awapige miti tena kwa nguvu, nilishuhudia akiteka mtoto wa kike kwa kushirikiana na wahuni wenzie na kumwiingiza kwenye gari yake aina ya R4 na kwenda kumpiga miti. Nae ametekwa hivyo hivyo kwa mazingira hatarishi
Nashangaa Leo whatsap yangu status ni sura yake wanawake wako buzy kumpost mara mshikaji mara mwingine uncle 😂
Kwakweli aende salama
 
😭 R.I.P
Baada ya kusambaa taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, Abdilah Musa maarufu kama Banjo, mkazi wa Sanawari, hatimaye mwili wake umekutwa katika eneo la Bereko wilayani Kondoa mkoani Dodoma ukiwa umeharibika.

Kwa mujibu wa mtoto wake Mussa Abdilah amesema kuwa walipigiwa simu kwamba kuna mwili umekutwa pembezoni mwa barabara maeneo ya Bereko Kondoa na wamefika na kuona mwili huo na kuthibitidha ni baba yao, akiwa ametobolewa macho na kuvunjwa mikono.

Banjo anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana February 12 jioni akitoka mazoezi katika "gym" iliyopo eneo la jengo la Ngorongoro. Walikuja watu wakamchukua na kuondoka naye. Ndugu zake walimtafuta bila mafanikio hadi leo mwili wake ulipopatikana huko Kondoa ukiwa umetobolewa macho na kuvunjwa mikono
Tangu lini banjoo akawa mfanyabiashara wa madini? Yule ni jambazi wa madini
😂😂 watu wa Arusha tumefurahi sana

Ila Nina shoga angu nimesoma naye alikua bwana ake 😂😂 yupo kulia Kwa status alimuambia amuombee awe na pesa mingi

R.I.P banjooo
Ni Sarah Mirambo?? Alilipendaga sana hili jambawazi
 
Abdilah Musa alimaaruf kama Banjoo alitikisa Arusha kwa ubabe wake na ujuzi wa kuishika na kuitumia bereta kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

Alikuwa mwizi wa madini na magari na mbabe haswa.

Soma Jambazi Sugu "BANJOO" larudi uraiani

Aliwahi kwenda magereza kwa vipindi tofauti lakini kesi yake maarufu ni Ile aliyomuua mfanyabiashara Laxman na kumuibia madini yake ya Tanzanite.

Siku sita zilizopita alichukuliwa kibabe na hakuonekana Tena mpaka Mwili wake ulipopatikana huko Kondoa akiwa ametobolewa macho na kuvunjwa mkono... exactly kama alivyokuwa anafanyia watu.

Banjoo amebaka wanawake na wake za watu sana tu kisa kuogopwa, kilichotokea Leo ni maandiko yametimia ua kwa upanga ufe kwa upanga.

Cha kusikitisha Leo hii waandishi vilaza wanamtaja kama mfanyabiashara maarufu wa madini huyu jambazi.

NB: Bereta ni bunduki bablay

Rest in hell Banjoo
Rest in hell Sadik Mkindi
Kama Kuna msamaha mamlaka za juu mbinguni zitaamua

B


Ikiwa ni saa kadhaa zimepita tangu Jambo TV iripoti taarifa ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mfanyabiashara wa madini, Abdillah Mussa maarufu kama Banjo, mkazi wa Sanawari mkoani Arusha, mwili wake umekutwa katika eneo la Bereko, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mwili huo ulikutwa ukiwa umeharibika, hali iliyozua maswali mengi kuhusu mazingira ya kifo chake.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mussa Abdillah, familia ilipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa kuna mwili umeokotwa pembezoni mwa barabara katika maeneo ya Bereko, Kondoa. Walipofika eneo hilo, walithibitisha kuwa mwili huo ni wa baba yao, huku ukiwa na majeraha ikiwemo kutobolewa macho na kuvunjwa mkono.

Mussa akizungumza hiyo jana alisema kuwa Februari 12 mwaka huu, baba yake aliondoka nyumbani kuelekea mazoezini katika eneo la jengo la Ngorongoro, lakini baadaye kulikuwa na taarifa kuwa alichukuliwa na watu wasiojulikana.

Juhudi za ndugu na jamaa kumtafuta hazikuzaa matunda hadi walipopokea taarifa za kupatikana kwa mwili wake huko Kondoa.

Jambo TV imetaka kufahamu suala hilo kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ambapo Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma imeeleza kuwa itatoa taarifa juu ya tukio hilo hapo baadaye kutokana na majukumu ya kiofisi yanayomkabili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma katika wakati tuliompigia.
1771512401104.jpg
 
Mtu ushapewa onyo mara kwa mara ila bado unajifanya mbabe na mkaidi lazima ushughulikiwe. Miaka ya 05-10 wababe wengi na mamafia wengi walipigwa onyo na biti, kama walikaidi walishughulikiwa. Hata huyu ni ukaidi wake, ila alishaonywa sana.
Kipindi cha Jiwe,kuna mwana nae alishindikana kabisa yule jamaa hadi police wakaenda kumkamata watapiga nae stoy tu au kibondo watapewa.
Jiwe naskia alipotezwa fasta yaani waliondoka nae nazima hakurudi mpk kesho hawajui yuko wapi
 
Sawa, lakini mrangi kuna sintofahamu kidogo juu ya nani aliyemteka,maana mtoto wake anasema baada ya kuhofia usalama wa baba yao baada ya kutoweka kwa siku kadhaa akitokea kwenye jengo la Ngorongoro tower alikokwenda kufanya mazoezi walienda polisi central na kuomba polisi wafuatilia kamera za jengo hilo ili kubaini kilichotokea,
Lakini katika hali ya kushangaza polisi waliwaonyesha footages za Banjoo akiwa anapanda kwenye jengo hilo, na nusu ya wakati anashuka, ila polisi wakagoma kuwaonyesha footage kutoka kwenye kamera za chini zikiwemo zile zinazoonyesha eneo la maegesho ambapo alikuwa amepaki gari lake, na hizo ndiyo footage muhimu ambazo zingeweza kubaini nini kilitokea baada ya kufika nje kwenye gari lake, cant you smell something fishy?
Mbona Kenya wamiliki binafsi wa eneo husika ndio huwa wanatoa cctv footage,hapa bongo ni mpaka polisi
 
Nitawapa story ya banjoo mwaka 2004
Kuna mshkaji wangu wa Tanga alikua anapiga mishe bandarini,zile za kutolewa mizigo ya wizi halafu yeye anauza kama dalali hv
Sasa kama wakaiba vifaa vya kuchimba yaani madigger,compressor pipes so jamaa akawa anahangaika sana kuuza ule mzigo dar...akashauriwa aende arushA
Kumbuka mtoto wa mjini kwa dar ila arushA haijui kabisa,
Akaambiwa ukifika arushA muone Nyari Justine,maana alikua na shimo that time na alikua kamanda wa vijana wa ccm mkoa wa arushA
Banjoo alikua kijana mtiifu kwa Nyari
Akamuona Nyari wakaelewana yuko na banjoo...
Nyari akasema twendeni mererani tukatest tulipane..Beka mshkaji wangu hajui ndio hatma yake
Wamefika mererani Nyari,na sterling wa Nyari na banjoo wakawa wanajiandaa kushuka chini..wakatest
MUNGU YUPO JAMANI
kumbe shimo la jirani sterling akawa anamfananisha dogo jamaa ni WA Tanga
Kumbe alimuacha dogo shule Tanga akaja zake mererani...
Akamuomba Nyari naomba niongee na dogo...ndio anamuhoji..we si mtoto wa Mzee Fulani? Ndio unakaa Tanga sehemu fulani dogo akasema ndio akamwambia subiri hapo hapo, akamfata Nyari akamwambia Nyari huyu ni mdogo wangu kabisa wa Tanga nakuomba pls...
Banjoo akatoa bastola akawa anairusha juu....kwa mtindo wa kuizungusa yaani anaibana mikono miwili kwa ubapa anairusha ikizunga alikua anarudia kusema maneno haya " unayo bahati chalii yangu,unayo bahati sana dogo ndio akashtuka alikua anamaliziwa manta ...wakapanda kwenye vx ya Nyari hapo...dogo akaachwa pale na vifaa vyake na yule sterling.,.aliogopa mno....hiyo ndio banjoo imagine 2004
 
Back
Top Bottom