Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Naona hii itakuwa habari njema sana kwa wafuasi wa Mbowe.
Sasa watachekelea utafikiri jimbo la Hai watalipata tena.
By the way, Sabaya alipaswa kupewa tuzo ya heshima na CCM na siyo kushtakiwa. Huu ni usaliti kwa mpiganaji kama huyu.
Neno haki haliko kwenye kamusi yako?
 
Hii Kuchuchumaa pia ipo kwenye sheria ?

Sio kwamba namtetea jamaa ila two wrongs does not make a right...., Huyu Jamaa adhibitiwe na kuhukumiwa kisheria na ikibainika sio tu kwamba achuchumae hata kama sheria inasema apigwe bakora na apigwe..., ila kabla ya hapo nadhani hii ni wrong precedent
Nyie ndiyo katika makuzi yenu hamjawahi hata kusukumwa na konda kwa daladala na misukosuko mingine katika maisha au hata kwenda kituo cha polisi kwa bahati mbaya. Unashangaa mtuhumiwa kuchuchumaa ? Smh
 
Hakuna uovu usio na malipo. Labda utubu kwa toba ya kweli. Kila mmoja kwa kipimo cha uovu wake, ndivyo na adhabu zao zikavyowaendea.

Bashite fanya toba ya kweli.
Ndugya tubu
Mahra jutia ouvu wako, omba msamaha
Mganga, shoka dhidi ya uovu halitakuacha usipotubu.
Wale wa chinichini huko, maded, maVeo, maocd, mnaojulikana ma
msiojulikana, neema na mafanikio kwenu utaendelea kuwa msamiati mgumu. Mlimtumikia, mlikula na kunywa na ibilisi, hata mkazinajisi nafsi zenu kwa matendo machafu, dhuluma, mauaji, utekaji watu, nanyi ni halali kwenu kuaibika na kuteseka.
 
Hiyo picha ikutafakarishe mtu yeyote utakayeiona.

Tambua ya kuwa nafasi uliyonayo ni ya muda tu. Hata kama utaishikilia mpaka mwisho wa uhai wako, ipo mahali utalipwa kutokana na matendo yako.

Busara zikuongoze utende haki na muombe Mungu akusimamie.

Majivuni na ukatili hayana lolote bora la kulipalilia.

Jana ulikuwa ukiwaamuru polisi na kukupigia salute, leo wanakupigisha magoti na pingu mkononi.
CC: Bashite
 
Vipi bwana makonda au tunaangaliana usoni..

Vipi hawa wanaokula mabilioni ya pesa!! Walioshutumiwa kufanya ubadhirifu?
 
Siku zaenda mbio. Mwana mamaaa (Wimbo gani huo tena?)

Sabaya naye wa kuficha sura leo? Kweli mwisho wa ubaya ni aibu. Nilifikiri vibaka wa mtaani tu ndio huficha sura mahakamani. Kumbe hata hawa vibaka wa serikalini! Ukisikia karma ndio hii.
Dunia kigeu geu- FM Academia
 
Hata akiachiwa kwa udhaifu wa ushahidi. Fresh tu. Ila siku ya leo mahabusu wa CHADEMA na ACT aliowafunga Gereza La Kisongo lazima wapeane zamu ya kumpeleka kwa mpalange.
Kwani ushajua anashitakiwa kwa Aina Gani ya Kesi Mpaka Akose Dhamama Mkuu?
 
Kwani kakosa nini,mbona huyu dogo anaonewa sana.
Samia naye tumpleke mahakamani maana utawala wake na Jiwe umeua watu wengi sana.lakini kama wote walikuwa wanafata maelekezo ya Jiwe basi dogo Huyo aachiwe.
 
Back
Top Bottom