ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
=====

Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.


Chanzo: Mwananchi
Kutoa rambirambi na waandishi wa habari wakiambatana na meya wapi na wapi! Unapomwalika meya na waandishi wa habari jua kuwa huo ni mkutano wa siasa.
Au shule haina AC no. ya bank? Kama ipo kwanini wasitume moja kwa moja kwa hiyo AC no. Mbona kama kuna kauchokozi kakisiasa kanaanzishwa!?.
 
Poor my country duh......Yani tumefika huko..Bsi wampeleke GAMBO awe mkuu wa wilaya ya KIBITI.
 
huyu mkuu wa mkoa anatumia mkuu wa upelelezi ili aonekane ndie aliyefanya kumbe anapokea amri tu, kama mtakumbuka hata yule aliyemzuia Nape si baadae alikana sio yeye aliyezuia
 
Polisi Arusha inawashikilia takribani Watu 24 wakiwemo wanahabari waliokuwa wakishuhudia shirikisho la wamiliki wa shule binafsi Tamongsco wakitoa rambirambi ya sh,million 18 kama pole katika shule ya Lucky Vincent Leo,

Wengine waliokamatwa yumo Meya wa Arusha Kalist Lazaro,mashekh wachungaji ,padri na madiwani Wawili ,mkuu wa shule ya Lucky Vincent na viongozi wa Tamongsco kanda ya kaskazini.

Polisi wanadai ni mkusanyiko usio halali.ni maelekezo ya RC Mrisho Gambo.
Kama taifa tumefika pabaya na tunakoelekea ni majuto.
 
nafikiri alikuwa anafatilia ukweli wa rambirambi,hakuna rc wa arusha alikuwa mbabe kama mulongo magesa,leo hii anaenda kwa shubash patel kuomba ajira....gambo you are exception and your downfall will be quick and heavy


Like this..........

iron-man-3-movie-poster-2-e1359630282283.jpg
 
hahaha tunakoelekea ni patamuuu
Katika watu wa ajabu ni godbless lema bungeni alisimama kuuliza swali kuwa kwa nini mumiliki kakamatwa badala ya kuuliza kuwa hiyo gari iliyoua hakuwa na bima malipo ya bima yatakuwaje kwa wafiwA na majeruhi? Haki zao zimepoteA au vipi? MawAkili komaeni jitoleeni kumburuza mahakamani mmiliki alipe wafiwa na majeruhi
 
nafikiri alikuwa anafatilia ukweli wa rambirambi,hakuna rc wa arusha alikuwa mbabe kama mulongo magesa,leo hii anaenda kwa shubash patel kuomba ajira....gambo you are exception and your downfall will be quick and heavy
mkuu sijui huu ubuyu. Magesa amefanikiwa kupata kazi kwa Shubash au ameendelea kuwa miongoni mwa vijana wasio na ajira
 
Kikao cha kazini na meya+wachungaji+waandishi!! no huo ni mkutano tn wa kisiasa.
Mkutano wa siasa ni ule wenye agenda ya KISIASA tu, raisi wabunge na viongozi wowote(+waandishi wa habari) wakienda kwenye hafla au msiba wowote haifanyi shughuli hiyo kuwa Mkutano wa kisiasa.
 
Mkuu kwa hiyo hata kutoa rambirambi ni mpaka upate kibali, hiki ni kichekesho, mnamuharibia raisi badala ya kumsaidia

Ndo mana wamepelekwa polisi wakaseme hzo taasisi zote (meya,mchungaji/wachungaji na waandishi) walikuwa wana shughuli gn pale!

kwenye hilo kundi hatujui ni nani aliekuwa anapeleka rambi rambi na nani alikuwa msindikizaji!!? ngoja wakajib hayo maswali polisi.

Afu km sikosei juzi kati hapa nilimsikia huyo meya analalamika kuhusu hzo rambi rambi bila shaka amekipata ss alichokuwa anakitaka!
 
wanazidi kujenga chuki na wananchi , kwani wangenyamaza waache wakatoe rambirambi zao wangepugukiwa nini
 
Back
Top Bottom