maguniolaf
JF-Expert Member
- Apr 11, 2017
- 506
- 197
Kutoa rambirambi na waandishi wa habari wakiambatana na meya wapi na wapi! Unapomwalika meya na waandishi wa habari jua kuwa huo ni mkutano wa siasa.Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .
Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
=====
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.
Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.
Chanzo: Mwananchi
Au shule haina AC no. ya bank? Kama ipo kwanini wasitume moja kwa moja kwa hiyo AC no. Mbona kama kuna kauchokozi kakisiasa kanaanzishwa!?.