Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 19,687
- 23,689
Labda kimoyomoyo anawacheka kwa nini wao wafiwe wakati yeye hafiwi.Kosa hakuna bali kaamua kuwakomoa tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda kimoyomoyo anawacheka kwa nini wao wafiwe wakati yeye hafiwi.Kosa hakuna bali kaamua kuwakomoa tu
Unglikuwa askari wa polisi wewe ungekataa kwenda?
Ungejipa akili japo kiwango cha ujinga ungejua kuwa meya ni mwanasiasa na shughuli aliyokwenda kuifanya inalengo la kumjenga kisiasa. Pia ingia kwenye akili za watoto hawa waliopoteza wenzao kukaa wanakumbushwa vitu wanavyopambana kuvisahau halafu jitu lingine linataka kila siku kuja kutoa rambirambi kwa manufaa yake ya kisiasa. Fanyieni siasa kwingine waacheni watoto wetu wapumue na huzuni.
Umeonaaa !? Dili lina fumuka .kula rambi rambi yenye sala za watz mamilioni hipo kazi hapo .hii itatokea puani tuuHapa si bure!
Safi sana.huu ndio ukweli.Jamaa alikuwa anafuatilia ukweli wa mgawanyo wa rambiramb na kupeleka rambarambi nyingine moja kwa moja kwa wafiwa bila kupitia "middle man/mtu wa kati(RC/serikali).Maana kuna kipengere kilisema chakula na vinywaji vya wageni wa meza kuu ilikuwa milioni 4.3(?),wakati hakuna mtu wa meza kuu aliyekula hata kidali cha bata mzinga,watu walimaliza kuaga wakaingia kwenye magari kukwepa mvua.Sasa hiyo milioni 4 ya chakula na vinywaji ilikuwajekuwaje?
Wafiwa walipewa milioni moja,na baadae wakahaidiwa kupewa milioni 2 na ushee zilizobaki,sasa maswali ikawa,inakuwaje rambirambi zinakuja nusunusu wakati zilitolewa kwa pamoja?
Walisema Serikali itagharamia safari na mazishi ya watoto,walimu na madereva.Lakini kwenye mchanganuo wanaonyesha kuwa pesa za rwmbirambi zilitumika kulipa madereva na magari ya usafiri,wakati kina Chambili,Kampuni ya Leopards na wadau wengine walichangi kama msaada,sasa hizo zilipoteaje?
Kudhihirisha chuki ya Kisiasa,siku ya msiba Gambo alitangaza CHADEMA kama Chama kimetoa shilingi milioni 5,Lakini kwenye mchanganuo wa jedwali lake,hajaweka CHADEMA kama chama kilichochangia,zaidi kawaweka UWT-Taifa,CCM mkoa wa Arusha nk...Sasa haya mambo ndio yanajenga machuki yasiyo na maana.
Wanamtumia Nyalandu kupenyeza "userikali" kwa kuwapeleka watoto marekani,Lakini ukiangalia website ya hawa jamaa,utaona kuwa wao walitaka siku ileile watoto wapelekwe US kutibiwa,lakini urasimu wa serikali na Gambo kwa "kiburi" kuwa serikali itawatibu kiliwachelewesha,mpaka wakatumia nafasi ya Makamu wa Rais alipoenda Hospital Mount Meru,wakawasakizia wale wamama wenye watoto kumsihi Mama Samia watoto waende nje kutibiwa kwa msaada wa Wazungu.
Halafu wanajidai kusema "Uongozi unaoacha Alama"...Hizo ni alama gani?au za chuki na visasi?Buree kabisaa
Unajifanya unachangia kama una busara vile, lakini sio kweli. Wewe unasumbuliwa na mahaba ya chama yaliyoambatana na ufinyu wa uelewa. Jaribu kutumia muda mwingi kusoma na kutafakari hizo hisia zako weka pembeniKama ni mkutano wa uchochezi ni sawa tu. Meya kaumbuka kwa kudai serikali imekula pesa, sasa wanataka kutumia siasa kufanya maajabu juu ya ajali iliyogusa wengi.
Mlianza mitandaoni kutishia kutumi nguvu kuichafua serikali, hiyo haikubaliki kabisaaaa.
Ni bora muweke sera zenu mbele zijulikane tho hamna, kuliko kudandia majambo kutafutia kiki.
Mengine tuheshimu dola itupe maelezo zaidi.