ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Hii ni aibu kubwa sana sasa watu wakikusanyika kwa nia ya kusaidia kuna shida gani???
 
Ila na ninyi mmezidi uchokozi, sasa ndio nini kwenda kutoa direct wakati ilishatangazwa Rambirambi zote lazima zipitie kwa wateule? Mnategemea wao watapata posho wapi?

Hapa Rambaramba tu.
 
Sihitaji kuamini ama kuhoji your level of understanding and reasoning, make kuna comment zako naziona haieleweki kabisa, mara unadai eti Lema abanwe aeleze ni namna gani atawasadia wafiwa na majeruhi kulipwa kwa kile unachodai gari haikuwa na bima, Lema anabanwa kwa lipi au kwa kipi?

Lema ni vehicle Inspector? Lema alikuwa turafiki wa zamu barabarani wakati na saa gari inaondoka Arusha? Lema alikuwa transport Coordinator wa Lucky Vicent? Lema ni HSSE Manager wa Lucky Vicent? Lema ni HSE Manager wa Luck Vicent? Lema HSSE & HSE Advisor ( Lead) wa Luck Vicent? kama majibu yote hayo ni hapana JF siyo jukwaa sahihi kwako.
Kuna watu ambao wanapaswa kuwajibika kwa hili na wala siyo Lema, weka itikadi yako pembeni jikite kwenye utaalam zaidi na nini cha kufanya ili kuepuka haya yasijurudie tena mbeleni.

Kwa mmiliki hapo hakwepi kubanwa lakini siyo kama wewe unavojaribu kumdraw Lema ktk hili:-
Kwa kukusaidia unapoplan route yoyote ile lazima maswali yafuatayo yapate majibu
1. Ikiwa kuna viashiria vya kuhatarisha usalama au matatizo yoyote ya kiusalama, Je kitengo cha usalama kiruhusishwa kabla ya kuanza safari?
2.Je maeneo yale yenye kuhatarisha usalama yalikuwa Identified kwa kutumia road hazard assessment?
3.Je kulikuwa na tool box talk kwa ajili ya kuandaa madereva wataoendesha hayo magari yaliobeba hawa watoto?

USALAMA
Yafuatayo yalipaswa kuzingatiwa:-
Hali ya usalama kutegemeana na hali ya hewa
Matatizo yanayofahimika kuhusu barabara iliyopaswa kutumika

HALI YA BARABARA
Ni lami au changarawe?
Je kuna miinuko,kona, kuvuka mito au kutoka nje ya barabara

MUDA WA DEREVA KUPUMZIKA
Je dereva alikuwa amepata muda wa kupumzika usiopungua saa 8 ndani ya masaa 24?

Ukizingatia hayo utaona ni nani anapaswa kubanwa, atakuwa ni mwendawazimu tu atakayefikiria kuna sehem Lema anapaswa kubanwa. Karibu.
 
Mara nyingine unahisi ni movie ya kichina unajipa moyo itaisha. Haya madaraka ya kulevya nahisi kilevi kimezidi.
 
Ukiona MTU anatumia sana vyombo vya dola hata kwa mambo binafsi utambue huyo ni kilaza alias bashite !!
 
Ungejipa akili japo kiwango cha ujinga ungejua kuwa meya ni mwanasiasa na shughuli aliyokwenda kuifanya inalengo la kumjenga kisiasa. Pia ingia kwenye akili za watoto hawa waliopoteza wenzao kukaa wanakumbushwa vitu wanavyopambana kuvisahau halafu jitu lingine linataka kila siku kuja kutoa rambirambi kwa manufaa yake ya kisiasa. Fanyieni siasa kwingine waacheni watoto wetu wapumue na huzuni.

Walienda kuona watoto au wazazi??Maana watoto bado wako likizo au CCM hajui hilo??

Laana ya kula Rambirambi imewaingia.
 
Jamaa alikuwa anafuatilia ukweli wa mgawanyo wa rambiramb na kupeleka rambarambi nyingine moja kwa moja kwa wafiwa bila kupitia "middle man/mtu wa kati(RC/serikali).Maana kuna kipengere kilisema chakula na vinywaji vya wageni wa meza kuu ilikuwa milioni 4.3(?),wakati hakuna mtu wa meza kuu aliyekula hata kidali cha bata mzinga,watu walimaliza kuaga wakaingia kwenye magari kukwepa mvua.Sasa hiyo milioni 4 ya chakula na vinywaji ilikuwajekuwaje?

Wafiwa walipewa milioni moja,na baadae wakahaidiwa kupewa milioni 2 na ushee zilizobaki,sasa maswali ikawa,inakuwaje rambirambi zinakuja nusunusu wakati zilitolewa kwa pamoja?

Walisema Serikali itagharamia safari na mazishi ya watoto,walimu na madereva.Lakini kwenye mchanganuo wanaonyesha kuwa pesa za rwmbirambi zilitumika kulipa madereva na magari ya usafiri,wakati kina Chambili,Kampuni ya Leopards na wadau wengine walichangi kama msaada,sasa hizo zilipoteaje?

Kudhihirisha chuki ya Kisiasa,siku ya msiba Gambo alitangaza CHADEMA kama Chama kimetoa shilingi milioni 5,Lakini kwenye mchanganuo wa jedwali lake,hajaweka CHADEMA kama chama kilichochangia,zaidi kawaweka UWT-Taifa,CCM mkoa wa Arusha nk...Sasa haya mambo ndio yanajenga machuki yasiyo na maana.

Wanamtumia Nyalandu kupenyeza "userikali" kwa kuwapeleka watoto marekani,Lakini ukiangalia website ya hawa jamaa,utaona kuwa wao walitaka siku ileile watoto wapelekwe US kutibiwa,lakini urasimu wa serikali na Gambo kwa "kiburi" kuwa serikali itawatibu kiliwachelewesha,mpaka wakatumia nafasi ya Makamu wa Rais alipoenda Hospital Mount Meru,wakawasakizia wale wamama wenye watoto kumsihi Mama Samia watoto waende nje kutibiwa kwa msaada wa Wazungu.

Halafu wanajidai kusema "Uongozi unaoacha Alama"...Hizo ni alama gani?au za chuki na visasi?Buree kabisaa
Safi sana.huu ndio ukweli.
 
Hivi hao wauaji wa huko kibiti wamepewa special order ya eneo hilo tu Au wanaweza Fika Na mikoa mingine Na wanaoisoma namba ni wengine Au Na wale
 
Kama ni mkutano wa uchochezi ni sawa tu. Meya kaumbuka kwa kudai serikali imekula pesa, sasa wanataka kutumia siasa kufanya maajabu juu ya ajali iliyogusa wengi.

Mlianza mitandaoni kutishia kutumi nguvu kuichafua serikali, hiyo haikubaliki kabisaaaa.

Ni bora muweke sera zenu mbele zijulikane tho hamna, kuliko kudandia majambo kutafutia kiki.

Mengine tuheshimu dola itupe maelezo zaidi.
Unajifanya unachangia kama una busara vile, lakini sio kweli. Wewe unasumbuliwa na mahaba ya chama yaliyoambatana na ufinyu wa uelewa. Jaribu kutumia muda mwingi kusoma na kutafakari hizo hisia zako weka pembeni
 
CCM wamefikia hatua ya kuzuia Watanzania kuhani misiba? Dah, kweli tunaongozwa na machizi
 
Wazazi mbona hawakukamatwa au wao hawakukusanyika nao hao waliokamatwa????laana zinanza kupanda taratibuuu
 
Back
Top Bottom