Arusha: Mfanyakazi wa Benki ya DTB ajiua kwa kujinyonga

Arusha: Mfanyakazi wa Benki ya DTB ajiua kwa kujinyonga

Bad news everywhere. Watu wameyeyuka mioyo na kukata tamaa. Mungu atusaidie watanzania.
 
Mfanyakazi wa Benki ya DTB, Jijini Arusha, Bryson Burchad (50) mkazi wa Ngusero jijini hapa,amejinyonga hadi kufa katika chumba Cha mpangaji wake kwa kutumia Kanga ya mkewe aliyoomba kwa lengo la kwenda kuoga huku akiacha ujumbe mzito kwa mkewe.

"Mke wangu Rose nisamehe kwa uamuzi niliochukua asilaumiwe mtu yoyote kwenye tukio hili ni uamuzi wangu mwenyewe,Dada zangu na mama ester mtunze wifi yenu na watoto wangu" ujumbe wa karatasi alioacha marehemu uliokutwa ndani ya suruwali yake.

Mwili wa marehemu uligundulika mapema leo majira ya saa moja asubuhi wakati mkewe,Rose Baraza akijaribu kumtafuta marehemu ili ampeleke mtoto shule .

Akiongelea tukio hilo Mke wa marehemu,(Rose) alisema kuwa majira ya saa 11alfajiri leo marehemu mumewe ambaye alikuwa ameajiriwa kama dereva katika benki hiyo, alimwomba kanga ili akaoge kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini.

Alisema ilipotimu saa moja na robo asubuhi alishituka usingizini kukuta mtoto wa shule Bado yupo nyumbani wakati marehemu huwa na kawaida ya kumpeleka shule majira ya saa moja asubuhi.

"Nilishtuka saa moja na robo asubuhi kuona mtoto hajapelekwa shule niliangalia vitu vyake ikiwemo simu yake ,nguo za kazini nikaona zipo nikabaki kushangaa huyu mtu atakuwa ameenda wapi,ndo baadaye wakati namtafuta nikaona kupitia dirisha amejinyonga kwenye chumba Cha mpangaji wetu"alisema.

Alisema baada ya kushuhudia tukio hilo alipiga kelele na baadaye majirani kukusanyika na kutoa taarifa polisi ambao walifika na kushuhudia mwili wa marehemu ukining'inia ikiwemo ujumbe wa barua katika suruwali ya marehemu.

Alifafanua kuwa siku moja kabla ya tukio hilo mumewe alikuwa akilalamika kuumwa na tumbo na alienda kutibiwa hospitali na kugundulika kusumbuliwa na Amueba ,Jambo ambalo mkewe alikanusha kuwa chanzo Cha mumewe kujinyonga.

Hata hivyo mke wa marehemu alifafanua kuwa marehemu aliwahi kumweleza kuwa pale kazini anaugomvi unaotishia kibarua chake na mfanyakazi mwenzake(hakumtaja)na kumfanya akose raha, Jambo ambalo lilimsababisha marehemu awe anakunywa pombe kupita kiasi kutokana na msongo wa mawazo.

Marehemu ameacha watoto wanne akiwemo mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi Mmoja na wiki tatu, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba Cha maiti katika hospital ya Mkoa wa Arusha ya Mt .Meru.

View attachment 2098766
Mmh aisee!
Makazini kuna uchawi jmn[emoji119]
Km humtegemei Mungu imekula kwako
 
Yaani mfanyakazi mwenzako akukere mpaka uamue kujiua?....


Jamaa ameiacha familia yake kwenye wakati mgumu sana.....ni vizuri kufikiria madhara ya yatakayowapata watu wako wa karibu/familia kabla ya kuchukua uamuzi wa hatari.
Kama roho ya mauti ikishatumwa kwako hata huwazi mara mbili !
 
Kuna maswali mengi sana juu ya hichi kifo na mke au mpangaji hawana la kujitetea juu ya hili
 
Hicho chumba Cha mpangaji Kuna uwalakini!
1. Huyo mpangaji ni jinsia Gani?
2. Huyo mpangaji hafanani na hicho kichanga Cha Mzee?
3. Huyo mpangaji alikuwa wapi?
4. Huyo Mpangaji yupo wapi sasa?
Usikute mpangaji ndo mwenye uyo mtoto wa mwezi mmoja kwa mke wa jamaa
 
Sijui kwanini watu wengi wanaamua kunywa pombe wakiamini ndio njia ya kuondoa stress/depression

''Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha''.

MATH 11:28-30
Sawa Mkuu, ngoja yakukute!
 
niliwahi kufanya kazi taasisi moja ya afya iliyoko chini ya wahindi..basi receptionist mmoja alikuwa anagongwa na meneja mhindi alikuwa ananizingua balaa ili niache kazi yeye amlete ndugu yake...nikaamua asubuhi kabla sijaingia kazini navuta bangi jicho linakuwa jekunduu...wale maboya walikuwa wakiniona wananikwepa ...nilipotimiza malengo yangu nikasepa.
Ungewala tigo mkuuu
 
Kama mke hajaweka barua yake sijui,kumbuka alikuwa wa kwanza kumwona lazima alikuwa wa kwanza kuona alichoandika mumewe.Mwanaume aache ujumbe kwamba mumtunze mke wangu!!!.....kuna walakini anataka wasimsumbue kwenye mali za mumewe.Sor kwa kuwaza tofauti.Sikuhiz zimeibuka tabia hovyo kabisa ukikata moto tu MTU wa kwanza kugundua kabla hajapiga ukunga ashakusachi sanaa
 
Wanaume sasa hivi tunatia huruma,ujasiri umetuisha kabisa...
 
Yaani mfanyakazi mwenzako akukere mpaka uamue kujiua?....


Jamaa ameiacha familia yake kwenye wakati mgumu sana.....ni vizuri kufikiria madhara ya yatakayowapata watu wako wa karibu/familia kabla ya kuchukua uamuzi wa hatari.
Mmmmmh,hapa kuna mashaka
 
Hicho chumba Cha mpangaji Kuna uwalakini!
1. Huyo mpangaji ni jinsia Gani?
2. Huyo mpangaji hafanani na hicho kichanga Cha Mzee?
3. Huyo mpangaji alikuwa wapi?
4. Huyo Mpangaji yupo wapi sasa?
Ukajinyonge chumba cha mpangaji????yaaan hapa
 
At the age of 50 anajinyonga, siku hizi kujinyonga imekua jambo la kawaida sana

Halafu ana mtoto wa mwezi mmoja maskini
At 50 una mtoto ana mwezi mmoja! Mtoto akifika 10yrs tayari una 60 umestaafu akiwa na miaka 5. Kama una vitega uchumi vya kutosha sawa, vinginevyo shule ataisikia tuu.
 
Back
Top Bottom