Arusha: Mkuu wa Magereza Godson Mwanagwa akanusha Ole Sabaya kufanya vurugu gerezani

Arusha: Mkuu wa Magereza Godson Mwanagwa akanusha Ole Sabaya kufanya vurugu gerezani

Arusha. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Wilson Manangwa amesema aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya hajapigwa baada ya kufikishwa katika Gereza Kuu la Kisongo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Akizungumzia na Mwananchi Digital jana Juni 5, 2021 Manangwa amesema Sabaya amepokewa jana na anaendelea vizuri.

"Hizi taarifa kuwa amepigwa na mahabusu wenzake baada ya kukataa kuoga sio za kweli, "amesema.

Amesema Magereza wana utaratibu wa kupokea watuhumiwa na hakuna mtuhumiwa anayepigwa kwa kukataa kuoga.

Jana Sabaya alifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka pamoja na wenzake watano ambayo ni uhujumu uchumi, ujambazi wa kutumia silaha, rushwa, kuunda genge la uhalifu na utakatishaji fedha ambayo yote hayana dhamana.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 18,

Mwananchi.

images.jpg
 
Mamaee zake ukimwangalia tu sura lilivyokuwa nyeusi ka kapinduka na gari la kiwi, japo ana umateumate lkn kutokana na roho mbaya yake kashindwa hata kutia rangi,, sasa sikwambii huko mahabusu na kibaridi cha arusha akitoka atakuwa ka buti la mgambo.. jitu likawe lina roho ka shetani, Kwani yeye ndo mtumishi wa kwanza wa serikali kushtakiwa, lkn mbona raia wamemkalia sana kooni. Hii ni kutokana na matendo yake, na kuna mwingine yule aliyekuwa mpambe wa rais nae huko aliko sasa hivi mimavi mbwambwambwa,, bashite[emoji1]
Kwa wale walio na deep knowledge na miji ya Arusha na Moshi: Watu wenye sura na haiba kama ya Sabaya mara nyingi wanakuwa majambazi au wababe makatili sana kwenye hii miji.
 
Back
Top Bottom