Arusha: Risiti za vifo zaidi ya 50 zakutwa ndani ya nyumba ya Ramji Hatibu Mlacha

Arusha: Risiti za vifo zaidi ya 50 zakutwa ndani ya nyumba ya Ramji Hatibu Mlacha

Nayasema haya kama mpare ambae niliamua kabisa kuukana na kuukimbia ukoo,,najua mambo ya huko kaskazini................

Kwa wapare kuwa na mambo ya kishirikina na uchawi kwa sana sijakataa lakini kwa jamii ya wachaga hapana aisee.
kumbuka kuzingatia general average ya population na sio umekutana na mchaga moja au wawili na Pengine hata sio full wachaga Pengine mama zao wazazi ni makabila yenye asili ya uchawi ukaanza kuzani wachaga wengi wako hivyo hapana aisee.
Mimi sio Mchaga lakini nasema ukweli na wengi wanaujua huu ukweli.
Na siku watakapoanza kujihusisha na uchawi na ushirikina wachaga kama ilivyo Upateni na Tanga baasi wajue watakwama na raha ya baraka iliyopo kwenye jamii zao uchagani itaanza kuwa historia.
Na maendeleo yataanza kurudi nyuma ,
Watakuwa kama vijiji vya Tanga na wilaya zake.
Uchagani vijijini kuna mtu anatembea peku peku kweli ?
Kuna nyuma za nyasi na tembe?
Labda kama sehemu ya utamaduni lakini sio sababu ya dhiki na njaa kali na laana za uchawi.
Moshi vijijini unakuta mtu hata Mzee kikongwe yuko smart kavaa Raba zake.
Walevi wanavaa viatu au malapa.
Hakuna funza wala mwenda peku.
 
Tukio lilianzia baada ya:

Mtoto wa miaka 11 (Maryam) anayesoma darasa la sita Kata ya Sokone One kukutwa ameuawa kwa kukatwa katwa na kutenganishwa mwili wake na kichwa na kisha kuwekwa kwenye beseni na kufichwa uvunguni mwa kitanda katika nyumba ya bwana Ramji Hatibu Mlacha.

Baada ya taharuki hii wananchi waliamua kuvunja nyumba, kuchukua na kutoa vitu vyote ndani ya nyumba

katika vitu vilivokutwa ni risiti zaidi ya 50 zikionesha malipo ya ada za vifo vya watu, risiti hizo zipo zinazoonesha vifo vinatakiwa 9 kwa risiti moja.

katika risiti hizo P.O.box inasoma
U.U.K.K. USANGI
P.O.Box 209 ARUSHA


Wananchi wanadai hiyo miaka sio hii tunayohesabu, pengine wanamiaka yao kwakua hizo risiti na za hivi miaka ya karibuni.

Mtuhumiwa alikua anaishi na mkewe.
Na aliyegundua kuwepo kwa mtoto huyo ni baada ya mtoto wao wakike aliyeolewa kuja kuwasalimia akiwa na mjukuu, mjukuu huyo aliingia ndani kutafta kiatu na kukuta mkono chini ya uvungu ndipo alipomuita mama yake na wakaanza kupiga kelele na watu kujaaa
View attachment 3123295

View attachment 3123250
SIASA MCHEZO MCHAFU SANA
 
Kila ufanyalo kumbuka Luka 12:2
Screenshot_20241013-130924.jpg
 
Kiswahili ni lugha yetu sote, lakini uelewa na matumizi yake saazingine hutofautiana.

Nilivyoelewa mimi kwa namna zilivyoandikwa risiti hizo ni kama kumbu kumbu ya michango ya kuhani ya 'nzengo' ambayo jamii inakuwa imekubaliana.

Michango ambayo huchangwa kila msiba utokeapo.

Sasa waliotajwa majina, walikuwa ni wadaiwa sugu wa michangoo ya rambi rambi hizo.
Vipi kuhusu kukutwa kwa viungo vya mtoto wa miaka 11? Pia ni mchango au geresha?
 
Again hivi vyama vya kufa na kuzikana vipo kisheria kabisa, mfano niliotoa hapo juu UMARO. Wanachama hudunduliza hela kwa ajili ya ku cover misiba inapotokea nyumbani

Again,.misiba ya kaskazini ni gharama sana kuliko mnavyodhani kwa sababu ukiwa hujatoka kaskazini utaona ajabu.

Alipofariki babu yangu walikuja watu 600 hivi. Ila matanga ilikuwa na watu 800 sio poa

Hakuwa kwenye chama cha kufa na kuzikana hivyo hela ilitutoka mfukoni. Ila kama angekuwepo huwa wanatoa fungu kwa mfiwa

Kawaida wachaga kuzikwa nyumbani. Kusafirisha gari ya msiba kwenda Moshi minimum ni million 1 gari. Unakuta zinatola coster zaidi ya moja huku

Bado huko unapoenda hawajala na huku dar lazima msiba ulillala..

Nadhani nimewafungua macho kuhusu vyama vya kufa na kuzikana

Ila swala la kukutwa mkono huko halihusiqna na vyama hivi.

Ni chama ambacho tunaweza anzisha hata JF
Lugha iliyotumika kwenye hizo risiti ni KIFO/VIFO Wala sio MSIBA/MISIBA
 
.....

Bado maelezo zaidi yanahitajika,kuelewa hizo risiti sio kazi ndogo.

Ada ya tsh 100,200,kwa ajili ya kifo mbona ni vitu visivyoeleweka?,Je ni vifo kweli au wameamua kutumia neno "Vifo" kumaanisha kitu kingine?

Pia inawezekana ni mchango wa chama kwa ajili ya rambirambi kwa waliofiwa.
Kwani ukitoa rambirambi risti hutolewa??? Na ikiwa ndiyo. Kwani ukitoa mchango nani anatakiwa apewe risti na yupi abaki na pesa sawa na risti ilivyoandikwa???
 
"Mbona kama...", inamaanisha huna uhakika na unachokisema halafu unakuja kuweka hitimisho la kufunga mjadala.

Aisee!
Niwe na uhakika asilimia mia mimi ndio risiti zangu hizo?

Wewe una uhakika asiimia mia ni za nini, freemason au?
 
Hali ya sintofahamu imeibuka katika Mtaa wa Muriet Jijini Arusha baada ya Mtoto aliyefahamika kwa jina la Mariamu Hatibu (11), aliyekuwa akisoma darasa la sita kudaiwa kuchinjwa na mwili wake kutenganishwa baadhi ya viungo kisha kuwekwa kwenye karai.

Mwili huo umekutwa katika moja ya Nyumba ya Jirani anayeishi Mtaa wa Muriet, Morombo huku katika eneo la tukio zikikutwa risiti za vifo zaidi ya ishirini zenye majina ya Watu.

Kulinga na Mashuhuda wa eneo hilo wanasema Mariamu alitoweka baada ya kutumwa dukani majira ya asubuhi na Mama yake kwenda kununua vocha, lakini hakurejea, licha ya kutafutwa bila mafanikio, ndipo Moto wa jirani alipouona mwili wa Mariamu ukiwa uvunguni baada ya kutoka Shule, akapiga kelele majirani wakafika na kuukuta mwili huo.

Ayo TV inaendelea kufuatilia kwenye Jeshi la Polisi ili kupata taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
#MillardAyoUPDATES
Screenshot_20241013-141335_1.jpg
 
Back
Top Bottom