Arusha: Risiti za vifo zaidi ya 50 zakutwa ndani ya nyumba ya Ramji Hatibu Mlacha

Nayasema haya kama mpare ambae niliamua kabisa kuukana na kuukimbia ukoo,,najua mambo ya huko kaskazini................

Kwa wapare kuwa na mambo ya kishirikina na uchawi kwa sana sijakataa lakini kwa jamii ya wachaga hapana aisee.
kumbuka kuzingatia general average ya population na sio umekutana na mchaga moja au wawili na Pengine hata sio full wachaga Pengine mama zao wazazi ni makabila yenye asili ya uchawi ukaanza kuzani wachaga wengi wako hivyo hapana aisee.
Mimi sio Mchaga lakini nasema ukweli na wengi wanaujua huu ukweli.
Na siku watakapoanza kujihusisha na uchawi na ushirikina wachaga kama ilivyo Upateni na Tanga baasi wajue watakwama na raha ya baraka iliyopo kwenye jamii zao uchagani itaanza kuwa historia.
Na maendeleo yataanza kurudi nyuma ,
Watakuwa kama vijiji vya Tanga na wilaya zake.
Uchagani vijijini kuna mtu anatembea peku peku kweli ?
Kuna nyuma za nyasi na tembe?
Labda kama sehemu ya utamaduni lakini sio sababu ya dhiki na njaa kali na laana za uchawi.
Moshi vijijini unakuta mtu hata Mzee kikongwe yuko smart kavaa Raba zake.
Walevi wanavaa viatu au malapa.
Hakuna funza wala mwenda peku.
 
SIASA MCHEZO MCHAFU SANA
 
Vipi kuhusu kukutwa kwa viungo vya mtoto wa miaka 11? Pia ni mchango au geresha?
 
Lugha iliyotumika kwenye hizo risiti ni KIFO/VIFO Wala sio MSIBA/MISIBA
 
Kwani ukitoa rambirambi risti hutolewa??? Na ikiwa ndiyo. Kwani ukitoa mchango nani anatakiwa apewe risti na yupi abaki na pesa sawa na risti ilivyoandikwa???
 
"Mbona kama...", inamaanisha huna uhakika na unachokisema halafu unakuja kuweka hitimisho la kufunga mjadala.

Aisee!
Niwe na uhakika asilimia mia mimi ndio risiti zangu hizo?

Wewe una uhakika asiimia mia ni za nini, freemason au?
 
Hali ya sintofahamu imeibuka katika Mtaa wa Muriet Jijini Arusha baada ya Mtoto aliyefahamika kwa jina la Mariamu Hatibu (11), aliyekuwa akisoma darasa la sita kudaiwa kuchinjwa na mwili wake kutenganishwa baadhi ya viungo kisha kuwekwa kwenye karai.

Mwili huo umekutwa katika moja ya Nyumba ya Jirani anayeishi Mtaa wa Muriet, Morombo huku katika eneo la tukio zikikutwa risiti za vifo zaidi ya ishirini zenye majina ya Watu.

Kulinga na Mashuhuda wa eneo hilo wanasema Mariamu alitoweka baada ya kutumwa dukani majira ya asubuhi na Mama yake kwenda kununua vocha, lakini hakurejea, licha ya kutafutwa bila mafanikio, ndipo Moto wa jirani alipouona mwili wa Mariamu ukiwa uvunguni baada ya kutoka Shule, akapiga kelele majirani wakafika na kuukuta mwili huo.

Ayo TV inaendelea kufuatilia kwenye Jeshi la Polisi ili kupata taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
#MillardAyoUPDATES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…