TANZIA Arusha Wing tumepata msiba wa mwenzetu Freetown

TANZIA Arusha Wing tumepata msiba wa mwenzetu Freetown

kwa masikitiko makubwa napokea taarifa hii, natoa pole nyingi mno kwa familia ndugu jamaa na rafiki na jamaa wa hapa jamii forum.
 
Write your reply...
Nilipigiwa simu jana alfajiri na Jamaangu anayeishi eneo la UsaRiver akaniambia kuwa wako Kilimanjaro International Airport muda wa saa 1.00

Akaniambia kuwa wamefika hapo kuupokea mwili wa Rafiki yetu Freetown ambao umeletwa na Ndege ya Emirates.

Freetown alikuwa mfanyakazi wa UN na alikuwa akiishi Pakistan na kufanyia kazi huko kwa muda mrefu

Taarifa zinasema kuwa Freetown alifariki katikati ya mwezi wa 6, na suala la kuusafirisha mwili wake kumrudisha nyumbani lilikuwa tata kutokana na hali ya usafiri wa ndege lilivyo kwa sasa.

Mwili wa Freetown ulisafirishwa hiyohiyo jana kuelekea kwao Mkoa wa Njombe

Mungu aiweke pema peponi roho ya mwenzetu Freetown.
Sad indeed really sad..Rest in un eternal peace Freetown until we meet again.
 
Kwa masikitiko makubwa tunapenda kuwajulisha members wote kuwa, mwenzetu Freetown hatunae tena,ametwaliwa kutoka kwenye ulimwengu huu.
Kwa members wa zamani, nadhani mtakuwa mnaifahamu hii ID vizuri.
Kwa wale tuliofanikiwa kusafiri pamoja kuelekea Tarangire kipindi kile, niwape pole sana kwa msiba huu.
Member mwenzetu PakaJimmy atakuja kutupa habari kamili kama alivyozipokea.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Apumzike kwa aman......Amen
Prishaz@Lily Flower@Mwanajamiione@Sahara Voice@Ncha@Derimto@Maxence Melo@Geoff@Asprin@Kaizer@Filipo@Blaki Womani@Cantalisia@Igwe@LiverpoolFC@Marejesho@Mzee wa Rula@Sweetlady
Poleni sana. Naikumbuka hiyo ID, ingawa sijaona post zake kwa muda mrefu pia.

RIP Freetown.
 
Innalilah wainna ilayhi raajiun

Sisi ni wa mungu na kwake tutarejea.

Tunamuomba mungu atupe mwisho mwema sotee tukumbuke ipo siku tutaondoka ndani ya ulimwengu huu!!!!

Rest in peace mate!
 
Back
Top Bottom