Pre GE2025 Arusha: Yanayojiri kwenye Maandamano ya Amani yaliyoandaliwa na CHADEMA, leo Februari 27, 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tangu maandamano yaanze nini kimebadilika

..kama hakuna kilichobadilika baada ya maandamano maana yake Rais Samia na serikali wameshindwa kazi, au kuja na majawabu ya kinacholalamikiwa.

..yaani ni sawa Mama mwenye katoto kachanga kanakolia halafu Mama huyo ashindwe kukapatia katoto hitaji lake, au hata ashindwe kujua kanahitaji nini.
 
Angalau Kwenye matembezi leo tulifika watu 100 tukapanga mistari 10 ya watu 10 tukaanza kutembea
 
27 February 2024
Arusha, Tanzania

HOTUBA
Tundu Lissu, Freeman Mbowe akishambulia kwa hoja Arusha leo umuhimu wa kuweka shindikizo kupitia maandamano ya wananchi hadi kieleweke

View: https://m.youtube.com/watch?v=2CGuQTQAl3c

Makamu wa mwenyekiti CHADEMA ageukia wasomi kina Prof. Kabudi Palamagamba wanaosema rais ni mungu mtu.

Katiba ya nchi imetengeneza mungu wa nchi yaani ardhi, ardhi yote ni mali ya umma chini ya uangalizi wa rais.

Watu wanaporwa adhi kona zote za nchi kuanzia Mbarali kusini hadi kaskazini Ngorongoro

Madini ya dhahabu, tanzanite, gesi asilia ardhini na baharini ipo chini ya udhamini wa rais mungu kukodhi mali zetu ndiyo maana watanzania hawana haki na mali zao vijijini, walizorithishwa na wazazi au kununua kihalali .....

Wanyama 10,000 wapo Sharjah katika zoo kwa amri ya mungu aliyepo ikulu

Misitu, bandari vyote vimegawiwa kwa wageni kwa marafiki zake uarabuni hectare milioni 8 zimekabidhiwa kampuni ya Uarabuni ili kuuza hewa ya carboni / ukaa pia hectare milioni 6 za Mwiba Holding Serengeti amepewa mzungu na yote hii ni kutokana na katiba ya rais mungu.

Sasa wewe mwananchi umebakiwa na nini? Umasikini na kutimuliwa kutoka katika ardhi yenu ya urithi yenye mali nyingi na mazao

Tozo, kodi zote zimeanzishwa na mungu rais Samia Hassan ambaye katiba iliyopo imempa mamlaka ya kuanzisha na kukataa kodi, tozo zote ili kuneemesha wateule wa rais ili fedha hizi wale kupitia V8 kwa viongozi wateule lakini hakuna ambulance.

Juzi eneo la ajali majeruhi waliondolewa na guta, canter kwa kutumia raia wema kwa sababu fedha zote zimenunua V8 mashangingi kila kona huku hakuna ambulance, gari za zimamoto, na huduma za paramedical hakuna

Biashara ya kodi na tozo huanzia kupangwa ikulu kisha kupelekwa bungeni. Hivyo kodi hizo ni za rais Samia katiba iliyopo inasema hayo.

Hivyo hakuna namna ya mungu rais kujinasua na lawama za kodi kubwa na matumizi mabaya yaliyo ya anasa.

Wafanyakazi wamebaki kuwa masikini wana mishahara midogo wanashindwa kugoma na kila Mei Mosi wanatembeza bakuli yallah masikini rais mungu tuongezee mshahara. Katiba iliyopo inasema rais mungu ndiyo aliye na mamlaka ya kuongeza mshahara..

Hivyo haki inatafutwa kwa maandamano, migomo na katiba mpya ili kuondoa mungu rais na vimiungu wake wateuliwa

Makamu mwenyekiti CHADEMA amaliza hotuba yake na sasa kumkaribisha mwenyekiti wa CHADEMA taifa kamanda Freeman Mbowe ahutubie mamia ya wananchi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi na watanzania popote nchini na ulimwenguni wanaotusikiliza kuhusu mustakhabali wa nchi na namna bora ya kwenda mbele.

Mh. Freeman Mbowe anasema leo tumehitimisha raundi ya kwanza ya maandamano katika majiji manne ya nchini Tanzania

Mh. Mbowe anaongeza kamati kuu ya CHADEMA imejiridhisha CCM haina nia njema bali inafanya ulaghai mtupu kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Dar es Salaam kilometa 50, kule Mbeya kilometa 42 Arusha leo kilometa 30 kuanzia eneo la KwaMrefu na kukutana na wananchi waliotueleza kero na taabu za maisha.

Tunakwenda kule Mtwara kutengeneza Azimio la Mtwara kwa mkutano wa kamati kuu na kuwapa taarifa ya maandamano haya ya majiji manne ambapo tumetembea jumla ya kilomita 160 kwa miguu kukutana na wananchi wa kada zote, vyama vyote ...

c.c Erythrocyte
 
Mwenyekiti wa Chadema Mbowe amesema Kamati kuu ya Chadema itaketi Mjini Mtwara na kutoka na Azimio la Mtwara

Hii ni baada ya kukamilika Maandamano ya kilometa 160 katika majiji manne ya DSM, Mwanza, Mbeya na Arusha na kukusanya maoni ya Wananchi

cc: The Big Show
 
Asante sana
 
Ni kawaida kwa ndugu Lema kutumia majukwaa ya siasa kutoa lugha za ovyo mfano,ugali ni chakula cha maskini,mimi ni mchagga,na kibaya zaidi huwa kuna wakati anaombea watu wafe.Mlioshiriki maandamano tunaomba mtuletee alichosema leo huyu mtaalamu wa kila kitu.
 
Back
Top Bottom