Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Makala ya Leo ya Kwa Maslahi ya Taifa, Inaanza na A Declaration of Interest

  1. Utangulizi Kama kawaida, leo tana nimepata tena fursa ya kushuka na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" leo nazungumzia kuponywa kwa taifa na trends za kuelekea 2025 za Rais Samia. Rais Samia ameonyesha kwa kauli na matendo, yeye ni mtu wa haki, sio tuu ni muwaza haki, na msema haki bali ni mpenda haki na mtenda haki kukifanya kile anacho kihubiri, yaani by practicing what she is preaching
  2. Kwa haya anayoyasema sasa, na haya anayoyatenda sasa, tunaamini soon Rais Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa, ataifanyia marekebisho Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuifanya kuwa tume huru zaidi na shirikishi, na atazifanyia marekebisho sheria kandamizi zinazonyima haki ambazo licha ya kuwa ni sheria batili, kwasababu zinakwenda kinyumbe cha Katiba ya JMT, ubatili huo, bado umechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.
  3. Katiba yetu ya 1977 ilitoa uhuru kwa kila Mtanzania mwenye sifa na vigezo, kuwa huru kushiriki kwenye kuunda serikali toka serikali za mitaa hadi serikali kuu kwa sherti moja tuu la Utanzania wake. Hivyo kila Mtanzania ana haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa!.
  4. Katiba hiyo imetoa uhuru wa kila Mtanzania kuwa huru kushiriki uchaguzi kwa kugombea nafasi yoyote na kushiriki kuwachagua viongozi wetu, bila vikwazo vyovyote. Hili ndilo lilikuwa lengo la mtunga katiba.
  5. Baadae kukajitokeza wataalamu fulani wa kufanya "mambo", wakafanya mambo!. Ile haki ya kila Mtanzania kuchagua viongozi Kwa kupiga kura kuwachagua viongozi, kwa uhuru, yenyewe bado ipo na inaendelea kuwepo, lakini haki na uhuru wa Mtanzania yoyote kushiriki kwenye kuunda serikali, yaani haki ya kugombea na kuchaguliwa, haki hii imeondolewa kwa ubatili fulani!.
  6. Japo Rais Samia ameunda timu ya "kikosi kazi" cha kumshauri, kikosi kazi hicho kinaita baadhi tuu ya watu, sijasikia kama sisi wananchi wa kawaida ambao ndio wamiliki wa katiba, pia tuko huru kufika mbele ya kikosi kazi, kuwasilisha mawazo yetu, ila mimi na haya mawazo yangu, nitayaandika na kuyawasilisha,
  7. Kwa vile tayari Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendio, yeye sio tuu ni muwaza haki na msema haki, bali mpenda haki na mtenda haki kwa kauli na matendo ya haki kuonekana, tunamuomba atutendee haki Watanzania, kwa kutuondolea ubatili huu wa ajabu kabisa, ndani ya Katiba Yetu!.
  8. Angalizo Bandiko hili, linauzungumzia ubatili fulani kwenye katiba yetu, kwa vile Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitu vikubwa, virefu, vigumu, wanapenda vitu rahisi rahisi, na mabandiko mafupi mafupi, wale wa type hii, mnaweza kuishia hapa, halafu mkarukia moja Kwa moja kwenye hitimisho. Wale mastory mastory tuendeleeni na Mastori ya Pasco Mayalla.

Hitimisho
Jana kwenye mitandao ya kijamii, zimesikika habari, Tundu Lissu amelipwa haki zake zote alizo dhulumiwa, hivyo hapa ni uthibitisho tuu wa matendo ya haki na sio tuu kauli za haki.

Kufuatia matendo haya, naamini kabisa kupitia “kikosi kazi”, soon Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa, ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi, pia atazifumua sheria kandamizi kuzifanyia marekebisho ili kufanya uchaguzi wa haki kwenye uwanja sawa wa ushindani na sio huu uwanja tenge wa uchaguzi wetu.

Tutunamuomba sana, sana, sana, Rais Mama yetu Samia, atuondolee na huu ubatili fulani ndani ya katiba yetu, uliochomekewa kiubatili, unao zioa haki ya kila Mtanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa. Haki hiyo imenyofolewa kwa kuchomekewa kiubatili kipengele batili cha kudhaminiwa na chama na siasa!. Ubatili wenyewe nimeuleza hapa na jinsi ulivyochomekewa kiubatili
KATIBA YETU INA UBATILI, SHERIA YA UCHAGUZI INA UBATILI!. na SHURTI HILI KWENYE KATIBA YETU NI BATILI!

Hivyo mpaka sasa, Rais Samia, ameishathibitisha kwa kauli na matendo, kuwa yeye ni mpenda haki na mtenda haki. Analiponya taifa, hivyo kwa matendo haya ya haki, Rais Samia anayoyafanya, atabarikiwa sana, na taifa litabarikiwa na kupata ustawi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Nimalizie kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia: Ni muwaza haki, msema haki , mpenda haki na mtenda haki!. Soon ataruhusu mikutano ya siasa na kuiunda NEC Shirikishi, jee vipi kuhusu ubatili huu ndani ya Katiba yetu?

Asante Mungu kwa Rais Samia, ni Baraka kwa nchi yetu!, naomba lile jicho, liuone na ubatili huu ndani ya katiba yetu, lituondoshee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.

Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Huo ubatilifu haupo kwa bahati mbaya... Ni fimbo ya kudhibiti nidhamu ndani ya vyama, na CCM wanaitumia vizuri sana. Mtu kama SH Amon angeweza kugombea Rungwe kama mgombea binafsi na akashinda.
 
Acha nao mkuu, mbona wao unakuta midume mizima iko humu kumsifu mwanaume mwenzao tena mume wa mtu, kisa tu huyo wanaemsifia ni kiongozi wao wa chama. Je na wao wanataka teuzi za kwenda kufanya kaz za ndani kwa mwenyekiti wao au wanasifia ili mwenyekiti aendelee kuwatumia kwa style ile ile ya kuwageuza chawa na nyumbu wa kisiasa kwa faida yake na familia yake.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Kumezuka huu mtindo wa mtu yoyote humu, akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshwa vidole vya kutafuta uteuzi, niliwahi kuwafundisha watu humu...
Ni rais aliye muwazi sana, katika nchi hii tangu imeumbwa hatujawahi na sidhani kama tutakuja kupata rais aliye systematic, anayesikia empathy, sympathy na anayewapenda watu wake kama Rais Samia. Huyu ni rais anayefanya mambo kwa uwazi sana, tunaona maendeleo...Hakuna siri kwenye hilo.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Kumezuka huu mtindo wa mtu yoyote humu, akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshwa vidole vya kutafuta uteuzi, niliwahi kuwafundisha watu humu
Pascal Mayalla

Nakusalimu tuu huko ulipo

lkn naomba niweke kumbukumbu kwamba wewe mwenyewe umeshawaikusema umestaafu uandishi wa mabandiko ukasema unaenda kugombea ubunge


sasa hili bandiko lako limetoka wapi
 
Mimi Mkenya hapa, napenda sana kusoma makala yako, huwa very deep, insightful and thought provoking, sema ndugu zako wazembe wa kusoma, comments zao zinaonyesha hawasomi kitu na kuelewa, wanajibu tu moja kwa moja.
 
Pascal Mayalla
Nakusalimu tuu huko ulipo
lkn naomba niweke kumbukumbu kwamba wewe mwenyewe umeshawaikusema umestaafu uandishi wa mabandiko ukasema unaenda kugombea ubunge
sasa hili bandiko lako limetoka wapi
Mkuu kibori nangai , baada ya wale ndugu zetu "wajumbe" kufanya yao!, nilikubalimatokeo na nikatoa taarifa ya kurejea mnipokee na kueleza
Kila kitu hapa!
P
 
Ukweli Raisi amejitahidi sana kwenye swala la haki. Alionekana mtu wa haki tangu hajawa Raisi. Ikumbukwe ndie kiongozi pekee alieweza kumtembelea Tundu lisu akiwa hospitalini Nairobi. Mungu ni mwema akamwinua kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Ameweza kutenganisha vizuri Mamlaka makubwa aliyonayo na Ubinadamu. Anaweza tofautiana na wewe kisiasa lakini kwa sababu ya ubinadamu bado mtaendelea kuwa marafiki.

Anastahili kupongezwa na tuna paswa kujifunza kuwa Ubinadamu lazima utangulie mamlaka makubwa katika maisha yetu.
Tusitende mabaya sababu ya madaraka kwani huja na kupita.
 
Neno HAKI limeanza kutamkwa baada ya Mbowe kukutana na Rais na kutangaza walichokubaliana kukihubiri badala ya kuhubiri amani wakati haipo. Hii kuwa ni msema kweli na mtenda haki itajulikana pale mazungumzo Kati yake na Chadema, na CCM yake kama mwenyekiti yatakapokamilika.

Sehemu kubwa ya ulahaghai wa siasa za Tanzania ni ya kitaasisi zaidi(CCM) kuliko mtu kama unavyochukulia.
Hapa CCM kama taasisi ndiyo kivuli cha uovu wote, maana huo ubatili wa kwenye katiba un aousema upo kwa sababu CCM ndiyo ngao yao katika kulinda maslahi yao.

Ni vigumu sana kwa mwanaccm kujitoa katika kibano hiki, ndiyo maana Chadema wakaona ni Meza ya mjadadala na makubaliano ambayo yanaweza Kuwa fanya CCM wakajipindua na hapo Mamlaka ya Rais kama taasisi nayo ikawajibika kwa kile kitakachokuwa kimekubaliwa na pande zote.

Hata hivyo bado tuna tatizo la kimfumo, kwa CCM kuwa Rais ndiye mwenyekiti wa chama. Kuna namna hata chama hakiwezi kuiagiza serikali katika baadhi ya mambo, kwani Mwenyekiti kujiagiza, Rais, na au kujisimamia ni ngumu kibinadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…