Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Naamini kupitia “kikosi kazi”, soon ataruhusu mikutano ya siasa, ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi, pia tunamuomba rais Samia, auondoe na ubatili fulani ndani ya katiba yetu, inayoruhusu kila Mtanzania kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa, haki ya kuchagua bado ipo ila haki ya kuchaguliwa, imechomekewa ubatili fulani wa kudhaminiwa na chama na siasa!. Ubatili wenyewe ni huu
KATIBA YETU INA UBATILI, SHERIA YA UCHAGUZI INA UBATILI!. na SHURTI HILI KWENYE KATIBA YETU NI BATILI!
Huenda dhamira yake kutoka moyoni ni njema ila wanaomzunguka na kujiita washauri, wapukuta remote ndiyo wenye shida, wanapukuta remote na kubonyeza bila yeye kujua
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.
Siyo kazi ya Rais au kiongozi yoyote wa ccm kufurahisha tu viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani huku akiacha wanachama wa chama chake wakiteseka. Kesi ya Sabaya ni ya kisiasa pia imejaa uongo mwingi ndiyo maana alipokata rufaa mahakama ikatengua hukumu ya miaka 30 lakini Rais Samia yuko kimya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa ,sisi kama watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa.
Hatuwezi kuhukumu watu kwa kusikiliza upande mmoja wa wanafiki chadema ambao hawana jema kwa nchi yetu.

Chadema kila kitu wanapinga na kuponda, walipinga ndege, bwawa la umeme, elimu bure, ujenzi wa viwanda kila kitu wao ni kupinga tu, Ndege zilipokamatwa walishangilia.
Ndiyo tuwasikilize? Hapana.

#Justice for SABAYA
#Free SABAYA
Enzi ya ujinga na upumbavu ilishapita, sijui eti Dodoma inaizidi mapato Dar es salaam na majitu yanashangilia. Na huyo huyo anayewadanganya, wakati wa korona anasahau,anasema siwezi kuiwekea lockdown Dar es salaam,kwani 80% ya mapato yanatoka Dar.na siyo Dodoma tena.
Sabaya haitaji mchango wa kumsaidia kesi,zaidi msaidieni aombe toba tu. Ushenzi aliowafanyia wanadamu wenzake ili kumfurahisha mwanadamu mwenzake ni uharamia usioweza kuvumilika hata kidogo. Hata wewe kwa akili yako mkuu wa Wilaya Hai, anakwenda Dar es Salaam eti kwenye operesheni maalum!! Yeye kama nani???
 
Huenda dhamira yake kutoka moyoni ni njema ila wanaomzunguka na kujiita washauri, wapukuta remote ndiyo wenye shida, wanapukuta remote na kubonyeza bila yeye kujua
Mkuu Faana, hili lina ukweli kiasi fulani, Mama hayuko deep sana kwenye numbers, hivyo kuna baadhi ya wenzetu wameisha lijua hilo, hivyo wana take advantage ya kupiga!. Mama akija kujua kuwa anapigwa!, ataua!.

Mfano. Deni original la kesi ya Simbion lilikuwa US $ 150 millions. Mdai akakubali ku settlement out of court. Kwenye settlement akakubali part payment of half in lieu of the whole, hivyo serikali tulipaswa kulipa US $ 75 milions, bahati nzuri najua kiwango kilicholipwa!, naomba nisitaje kiwango kilicholipwa nikamponza bure Mkuu Max akatafutwa na wale jamaa zetu, kumlazimisha kutoa details za huyu member ili ahojiwe alijuaje hicho kiwango wakati ni siri?.

Ukiisikia figure iliyokuwa supposed kulipwa na the real figure iliyolipwa unaweza kudhani Mamie nae ni part and parcel, of the deal, lakini kwa kutumia jicho la tatu la roho, unaona wazi wazi kuwa Mama hana hili wala lile na hajui chochote, wajanja wanamzunguka, kupiga pesa ndefu, huku akiamini honestly kuwa analipa madeni chechefu yote.

2. Kwenye baadhi ya tenda kubwa kubwa za ujenzi, kwanza zinatolewa by single source, bila ushindani, halafu mzabuni ame inflates kwa cha juu kirefu kwa hoja ya "chakula ya wazee" watu kudhani Mzee ni Mama, kumbe ni wanamzunguka tuu, Mama hajui kitu.

P
 
Pascal Mayalla ukipewa Uwaziri wa habari utaukataa?
Kumteua Mwandishi yoyote wa habari au mtangazaji mwenye kipaji cha uandishi au utangazaji anayeijua kazi yake, into any position ya kiutendaji, is wasting a valuable talent.

Kitu cha maana kwa mtu kama mimi kufanyiwa ni kwa Mama, amuite Dr. Ayub Rioba, na kumpa maelekezo Pasco Mayalla apewe live airtime kwenye TBC, arushe kipindi chake cha "Kwa Maslahi ya Taifa" in Kitimoto style, niwakalishe viongozi, niwahoji, taifa lifaidike.

P
 
2. Kwenye baadhi ya tenda kubwa kubwa za ujenzi, kwanza zinatolewa by single source, bila ushindani, halafu mzabuni ame inflates kwa cha juu kirefu kwa hoja ya "chakula ya wazee" watu kudhani Mzee ni Mama, kumbe ni wanamzunguka tuu, Mama hajui kitu
Naafikiana nawe 100% Mkuu Pascal Mayalla kimsingi anahitaji timu ya watu smart na waadilifu kumsaidia otherwise nia yake ya 2025 inachafuliwa sasa na muda ukifika hataweza kuisafisha, possibly wanatumia hiyo statement ya chakula cha wakubwa kumchafua zaidi ili wwafanikishe mbinu zao za kumwondoa msimu ukifika
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Kumezuka huu mtindo wa mtu yoyote humu, akisifia jambo lolote kumhusu rais wa JMT, ananyooshwa vidole vya kutafuta uteuzi, niliwahi kuwafundisha watu humu, jinsi ya kutofautisha wasifiaji wa kujikombakomba na kutafuta uteuzi, na wasifiaji wa ukweli, kumsifu kiongozi anapofanya mazuri ili kumtia moyo. Wasifiaji wa kujikombakomba, wao kazi yao huwa ni moja tuu, kusifu, kuimba nyimbo za shangwe na mapambio, kawa wafanyavyo watu wanaitwa ma "chawa". Wasifuji wa ukweli, wa type yangu ni wale tunaosifu mazuri tuu, na kukitokea huyo unayemsifu akaboronga, tunamkosoa. Mtafuta uteuze kamwe hawezi kukosoa!.

Mimi Paskali, naomba ku declare interest, nansifu Rais Samia kwa mazuri yake na wala sitafuti uteuzi wowote, na kumsifu rais Samia sikuanza leo, tembelea HAPA! na HAPA! tena ni mimi mwaka 2015 nilimtaja Samia Suluhu Hassan kuwa na best female presidential material HAPA!

Hivyo pongezi zangu mbalimbali kwa Rais Samia, kama hizi PONGEZI! PONGEZI!, SAMIA TUMAINI JIPYA! SAMIA MPONYAJI!

ndio maana naelewa kuwa Rais Samia ni binadamu, na anaweza kukosea makosa ya kibinaadamu, akikosea pia tunamkosoa humu humu kama hapa jinsi nilivyo mkosoa RAIS SAMIA SIO MALAIKA, NI BINADAMU! na 2025 SIO LAZIMA SAMIA! na JAPO TUMEPANGA 2025 TWENDE NA MWANAMKE, KUNA HII SAUTI!

Hata kwenye utengenezaji wa filamu ya Royal Tour, tangu mwanzo tunaiandaa, tulikosoa na kushauri, local producers wa ndani pia tushirikishwe, ili baada ya filamu ya Mama ya kizungu kwa ajili ya wazungu, local producers, tumtengenezee Mama A Tanzanian Tour, kwa Kiswahili kwa ajili ya utalii wa ndani. Kabla ya uzinduzi wa Royal Tour, wengi wameishia kusifu tuu, akina sisi ambao tuko more objective, hatukusifu tuu bali pia tumekosoa!

ROYAL TOUR TUNGE...! Hivi msifia mtafuta uteuzi, atasifu tuu, hawezi kukosoa lolote, msifia ukweli, atasifu panapostahili sifa na kukosoa panapostahili kukosolewa!

Utangulizi
Kama kawa, leo tana nimepata nafasi ya kushuka na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" leo nazungumzia kuponywa kwa taifa na trends za 2025, Rais Samia, Ameosha kwa Kauli na Matendo, Yeye ni mtu wa haki, sio tuu ni msema haki bali ni mtenda haki, tunaamini soon ataruhusu mikutano ya siasa, na kuifanyia marekebisho Tume ya taifa ya Uchaguzi kuifanya kuwa tume huru zaidi na shirikishi.

Katiba yetu ya 1977 ilitoa uhuru kwa kila mtanzania mwenye sifa na vigezo, kuwa huru kushiriki kwenye kuunda serikali toka serikali za mitaa hadi serikali kwa sheti moja tuu la Utanzania wake. Hivyo kila Mtanzania yuko ana haki na yuko huru kushiriki uchaguzi kwa kugombea nafasi yoyote na kushiriki kuwachagua viongozi wetu. Hili ndilo lilikuwa lengo la mtunga katiba. Baadae kukajitokeza "mambo", haki ya kupiga kura kuwachagua viongozi, kwa uhuru, hii ipo na inaendelea, lakini haki na uhuru wa mtu yoyote kushiriki kwenye kuunda serikali, yaani haki ya kugombea na kuchaguliwa, haki hii imeondolewa kwa ubatili fulani,

Japo Rais Samia ameunda timu ya "kikosi kazi" cha kumshauri, na hicho kikosi kazi kinaita baadhi tuu ya watu, sijasikia kama sisi wananchi wa kawaida pia tuko huru kufika mbele ya kikosi kazi, ila mimi haya mawazo yangu, nitayaandika na kuyawasilisha, ila kwa vile tayari Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendio, yeye sui tuu ni muwaza haki na msema haki, bali pia ni mtenda haki kwa matendo ya haki kuonekana, tunamuomba atutendee haki Watanzania, kwa kutuondolea ubatili huu, ndani ya Katiba Yetu!.

Angalizo
Bandiko hili, linauzungumzia ubatili fulani kwenye katiba yetu, kwa vile Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitu vikubwa, virefu, vigumu, wanapenda vitu rahisi rahisi, na mabandiko mafupi mafupi, wa wa type hii, inaweza kuishia hapa, halafu mkarukia kwenye hitimisho.

Mastori ya Pasco Paskali Snr

Hitimisho

Jana kwenye mitandao ya kijamii, zimesikika habari, Tundu Lissu amelipwa haki zake, hivyo hapa ni uthibitisho tuu wa matendo ya haki na sio tuu kauli za haki.

Naamini kupitia “kikosi kazi”, soon ataruhusu mikutano ya siasa, ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi, pia tunamuomba rais Samia, auondoe na ubatili fulani ndani ya katiba yetu, inayoruhusu kila Mtanzania kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa, haki ya kuchagua bado ipo ila haki ya kuchaguliwa, imechomekewa ubatili fulani wa kudhaminiwa na chama na siasa!. Ubatili wenyewe ni huu
KATIBA YETU INA UBATILI, SHERIA YA UCHAGUZI INA UBATILI!. na SHURTI HILI KWENYE KATIBA YETU NI BATILI!

Hivyo mpaka sasa, Rais Samia, ameishathibitisha kwa kauli na matendo, kuwa yeye ni mpenda haki na mtenda haki. Analiponya taifa, hivyo kwa matendo haya ya haki, Rais Samia anayoyafanya, atabarikiwa sana, na taifa litabarikiwa na kupata ustawi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nimalizie kumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais Samia: Ni Msema Haki na Mtenda Haki!. Soon Ataruhusu Mikutano ya Siasa na NEC Shirikishi, jee vipi kuhusu ubatili huu ndani ya Katiba yetu?

Asante Mungu kwa Rais Samia, ni Baraka kwa nchi yetu, naomba lile jicho, liuone na ubatili huu ndani ya katiba yetu.

Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
praise team hingera
 
Kwa kuwa dhamira njema ipo, masuala yote ya msingi yatafanyiwa kazi. Dhamira njema ni hatua muhimu sana kwa kuanzia.
Mkuu Azizi Mussa , naunga mkono hoja, Rais Samia ameonyesha a political will in good faith. Utashi wa kisiasa wenye dhamira njema ya kulitibu hili taifa.
P
 
Pointless zaidi ya kutafuta kuosha vyombo vya ikulu ujiliepo kidogo
 
Huo ubatilifu haupo kwa bahati mbaya... Ni fimbo ya kudhibiti nidhamu ndani ya vyama, na CCM wanaitumia vizuri sana. Mtu kama SH Amon angeweza kugombea Rungwe kama mgombea binafsi na akashinda.
Mkuu Mtama mchungu, naunga mkono hoja, huu ubatili haupo kwa bahati mbaya, kiliingizwa kwa makusudi mazima. Kiukweli kabisa, hicho kilichofanyika ni ubatili na uhuni mtupu!. Kwa vile Mama Samia ni mpenda haki, jukumu letu ni kumuangazia kwa kuumulikia huo ubatili, Mama Samia auone atuondolee.
P
 
Nje ya mada, hata sidhani kama umesoma bandiko la Pasco. Hiyo yako ya Sabaya ifungulie uzi wake na watu wa jinsi yako watakuunga mkono
Mkuu SAGAI GALGANO , asante sana kusaidia watu humu kwa kuwakumbusha kujadili hoja iliyopo mezani, na kama wana hoja tofauti, waanzishie thread yake inayojitegemea.

P
 
Acha nao mkuu, mbona wao unakuta midume mizima iko humu kumsifu mwanaume mwenzao tena mume wa mtu, kisa tu huyo wanaemsifia ni kiongozi wao wa chama.
Mkuu Mr Dudumizi , hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote wa jinsia yoyote kumsifia mtu mwingine yoyote, wa jinsia yake.
Je na wao wanataka teuzi za kwenda kufanya kaz za ndani kwa mwenyekiti wao au wanasifia ili mwenyekiti aendelee kuwatumia kwa style ile ile ya kuwageuza chawa na nyumbu wa kisiasa kwa faida yake na familia yake.
Kuna tofauti kati ya kumsifia mtu bonafide genuine na uchawa. Sio kila kusifu au kupongeza ni uchawa!.
P
 
Uko vizuri katika kufuatilia news kuhusu TZ. Bila shaka unaielewa nchi hiyo kwa undani wake. Itabidi RAO akutafutie walau nafasi ya ajira katika ubalozi wa Kenya nchini TZ hapo atakapoapishwa kuwa rais.
Mimi Mkenya hapa, napenda sana kusoma makala yako, huwa very deep, insightful and thought provoking, sema ndugu zako wazembe wa kusoma, comments zao zinaonyesha hawasomi kitu na kuelewa, wanajibu tu moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom