Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Huenda dhamira yake kutoka moyoni ni njema ila wanaomzunguka na kujiita washauri, wapukuta remote ndiyo wenye shida, wanapukuta remote na kubonyeza bila yeye kujua
 
Enzi ya ujinga na upumbavu ilishapita, sijui eti Dodoma inaizidi mapato Dar es salaam na majitu yanashangilia. Na huyo huyo anayewadanganya, wakati wa korona anasahau,anasema siwezi kuiwekea lockdown Dar es salaam,kwani 80% ya mapato yanatoka Dar.na siyo Dodoma tena.
Sabaya haitaji mchango wa kumsaidia kesi,zaidi msaidieni aombe toba tu. Ushenzi aliowafanyia wanadamu wenzake ili kumfurahisha mwanadamu mwenzake ni uharamia usioweza kuvumilika hata kidogo. Hata wewe kwa akili yako mkuu wa Wilaya Hai, anakwenda Dar es Salaam eti kwenye operesheni maalum!! Yeye kama nani???
 
Huenda dhamira yake kutoka moyoni ni njema ila wanaomzunguka na kujiita washauri, wapukuta remote ndiyo wenye shida, wanapukuta remote na kubonyeza bila yeye kujua
Mkuu Faana, hili lina ukweli kiasi fulani, Mama hayuko deep sana kwenye numbers, hivyo kuna baadhi ya wenzetu wameisha lijua hilo, hivyo wana take advantage ya kupiga!. Mama akija kujua kuwa anapigwa!, ataua!.

Mfano. Deni original la kesi ya Simbion lilikuwa US $ 150 millions. Mdai akakubali ku settlement out of court. Kwenye settlement akakubali part payment of half in lieu of the whole, hivyo serikali tulipaswa kulipa US $ 75 milions, bahati nzuri najua kiwango kilicholipwa!, naomba nisitaje kiwango kilicholipwa nikamponza bure Mkuu Max akatafutwa na wale jamaa zetu, kumlazimisha kutoa details za huyu member ili ahojiwe alijuaje hicho kiwango wakati ni siri?.

Ukiisikia figure iliyokuwa supposed kulipwa na the real figure iliyolipwa unaweza kudhani Mamie nae ni part and parcel, of the deal, lakini kwa kutumia jicho la tatu la roho, unaona wazi wazi kuwa Mama hana hili wala lile na hajui chochote, wajanja wanamzunguka, kupiga pesa ndefu, huku akiamini honestly kuwa analipa madeni chechefu yote.

2. Kwenye baadhi ya tenda kubwa kubwa za ujenzi, kwanza zinatolewa by single source, bila ushindani, halafu mzabuni ame inflates kwa cha juu kirefu kwa hoja ya "chakula ya wazee" watu kudhani Mzee ni Mama, kumbe ni wanamzunguka tuu, Mama hajui kitu.

P
 
Pascal Mayalla ukipewa Uwaziri wa habari utaukataa?
Kumteua Mwandishi yoyote wa habari au mtangazaji mwenye kipaji cha uandishi au utangazaji anayeijua kazi yake, into any position ya kiutendaji, is wasting a valuable talent.

Kitu cha maana kwa mtu kama mimi kufanyiwa ni kwa Mama, amuite Dr. Ayub Rioba, na kumpa maelekezo Pasco Mayalla apewe live airtime kwenye TBC, arushe kipindi chake cha "Kwa Maslahi ya Taifa" in Kitimoto style, niwakalishe viongozi, niwahoji, taifa lifaidike.

P
 
2. Kwenye baadhi ya tenda kubwa kubwa za ujenzi, kwanza zinatolewa by single source, bila ushindani, halafu mzabuni ame inflates kwa cha juu kirefu kwa hoja ya "chakula ya wazee" watu kudhani Mzee ni Mama, kumbe ni wanamzunguka tuu, Mama hajui kitu
Naafikiana nawe 100% Mkuu Pascal Mayalla kimsingi anahitaji timu ya watu smart na waadilifu kumsaidia otherwise nia yake ya 2025 inachafuliwa sasa na muda ukifika hataweza kuisafisha, possibly wanatumia hiyo statement ya chakula cha wakubwa kumchafua zaidi ili wwafanikishe mbinu zao za kumwondoa msimu ukifika
 
praise team hingera
 
Kwa kuwa dhamira njema ipo, masuala yote ya msingi yatafanyiwa kazi. Dhamira njema ni hatua muhimu sana kwa kuanzia.
Mkuu Azizi Mussa , naunga mkono hoja, Rais Samia ameonyesha a political will in good faith. Utashi wa kisiasa wenye dhamira njema ya kulitibu hili taifa.
P
 
Pointless zaidi ya kutafuta kuosha vyombo vya ikulu ujiliepo kidogo
 
Huo ubatilifu haupo kwa bahati mbaya... Ni fimbo ya kudhibiti nidhamu ndani ya vyama, na CCM wanaitumia vizuri sana. Mtu kama SH Amon angeweza kugombea Rungwe kama mgombea binafsi na akashinda.
Mkuu Mtama mchungu, naunga mkono hoja, huu ubatili haupo kwa bahati mbaya, kiliingizwa kwa makusudi mazima. Kiukweli kabisa, hicho kilichofanyika ni ubatili na uhuni mtupu!. Kwa vile Mama Samia ni mpenda haki, jukumu letu ni kumuangazia kwa kuumulikia huo ubatili, Mama Samia auone atuondolee.
P
 
Nje ya mada, hata sidhani kama umesoma bandiko la Pasco. Hiyo yako ya Sabaya ifungulie uzi wake na watu wa jinsi yako watakuunga mkono
Mkuu SAGAI GALGANO , asante sana kusaidia watu humu kwa kuwakumbusha kujadili hoja iliyopo mezani, na kama wana hoja tofauti, waanzishie thread yake inayojitegemea.

P
 
Acha nao mkuu, mbona wao unakuta midume mizima iko humu kumsifu mwanaume mwenzao tena mume wa mtu, kisa tu huyo wanaemsifia ni kiongozi wao wa chama.
Mkuu Mr Dudumizi , hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote wa jinsia yoyote kumsifia mtu mwingine yoyote, wa jinsia yake.
Je na wao wanataka teuzi za kwenda kufanya kaz za ndani kwa mwenyekiti wao au wanasifia ili mwenyekiti aendelee kuwatumia kwa style ile ile ya kuwageuza chawa na nyumbu wa kisiasa kwa faida yake na familia yake.
Kuna tofauti kati ya kumsifia mtu bonafide genuine na uchawa. Sio kila kusifu au kupongeza ni uchawa!.
P
 
Uko vizuri katika kufuatilia news kuhusu TZ. Bila shaka unaielewa nchi hiyo kwa undani wake. Itabidi RAO akutafutie walau nafasi ya ajira katika ubalozi wa Kenya nchini TZ hapo atakapoapishwa kuwa rais.
Mimi Mkenya hapa, napenda sana kusoma makala yako, huwa very deep, insightful and thought provoking, sema ndugu zako wazembe wa kusoma, comments zao zinaonyesha hawasomi kitu na kuelewa, wanajibu tu moja kwa moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…