Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala ya Leo kwenye Nipashe
Jumapili ya June 8, mwaka 2021, katika safu hii, niliandika makala ya kumpongeza Rais Samia, kwa kuwasisitiza watendaji wa serikali kutenda haki, kufuatia baadhi ya haki zilizotolewa na katiba yetu na kugeuzwa ni hisani, Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki Malala ya leo ni kumpongeza tena rais Samia.
Baada ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya siasa, sasa ni nderemo na vifijo nchi mzima!. Na mimi kama Mtanzania mzalendo wa taifa letu, pale linapofanywa jambo jema lolote la kheri kwa mustakabali mwema kwa taifa letu, sina budi kujiunga na wengine wote wanaolitakia mema taifa hili kwa kumpongeza Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya siasa, kukubali kurekebisha sheria mbalimbali kandamizi na kubwa kuliko, kukubali kuendeleza mchakato wa katiba mpya.
Kwenye hili la kuzuiwa mikutano ya hadhara, kwa vyàma vya siasa kwa vile mikutano hiyo ya vyama vya siasa ni jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, hivyo vyama vya siasa kufanya mikutano ni miongoni mwa haki za vyama vya siasa zilizoainishwa na katiba, hata lile swali langu la Ikulu, kumuuliza rais wa JMT, ametumia mamlaka gani kwenye kifungu kipi cha sheria, kuzuia jàmbo lililoruhusiwa na katiba?, japo sikumbuki siku ile pale ikulu nilijibiwa nini, lakini sasa ndio Rais Samia, amemjibia.
Waswahili wana msemo, "anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!", jambo linalozuiliwa kwa utashi tuu, bila kifungu chochote, cha katiba au sheria, sasa limeruhusiwa kwa utashi tena, bila kutumia kifungu chochote cha katiba na sheria. Jambo lolote lililozuiliwa, linaporuhusiwa, hatua ya kwanza ni kushukuru kwa jambo hilo kurusiwa, hivyo Watanzania wote tujiunge pamoja na kusema kwa kauli moja, "Asante Sana Mama".
Baada ya kushukuru, tusipojiuliza hili liliwezaje kutokea, ili lisije kujirudia kutokea tena. Sasa twende ndani kidogo zaidi ya jambo lenyewe lililoruhusiwa, kwa vile mikutano ya siasa ilizuiliwa kwa utashi tuu, na sasa imeruhusiwa kwa utashi tena, tukishukuru na kusema tuu asante bila kutia neno jingine lolote, hii inapelekea suala la mikutano ya siasa kuonekana ni kama jambo la hisani tuu ya rais aliyepo madarakani, JPM alizuia mikutano kwa utashi tuu, na leo Rais Samia ameruhusu mikutano hii kwa utashi na kwa hisani tuu!, tusipoliwekea muongozo, kesho atakuja kiongozi mwingine naye ataweza kuzuia jambo loloye kwa utashi tuu.
Kitu kama ni haki, haki hiyo ni stahili sio hisani!, Je sisi Watanzania tutaendelèa kuruhusu viongozi wetu, wazigeuze haki zetu na stahili zetu kuwa hisani mpaka lini?.
Tena afadhali ya hili la haki ya mikutano ya siasa, limefanywa kwa utashi tuu kwa kutumia kauli tuu, yaani mikutano ilizuiliwa kwa kauli, na sasa imeruhusiwa kwa kauli, lakini kuna na haki nyingine mbili ambazo ndizo haki kuu za kiraia zilizotolewa na katiba yetu, haki za kuchagua na kuchaguliwa, haki moja kati ya haki mbili hizo, imegeuzwa hisani!. Haki ya kuchagua yenyewe bado ipo, ila haki ya kuchaguliwa imegeuzwa hisani!.
Tunamshukuru sana Rais Samia kutuhisania Watanzania kuturudishia haki hii, Tuendelee kumuombea Rais Samia Mungu aendelee kumlinda na kumbariki, ili kufikia mwaka 2025, awe ameisha turudishia haki zote za kikatiba ziliporwa na kugeuzwa hisani. Nimeutaja mwaka 2023 japo ninaelewa Rais Samia anayo gursa ya kuendelea kuhudumu kipindi cha pili cha mwaka 2025-2030, mimi natumia mtindo wa linalowezekana leo lisingoje kesho. Sasa tuko 2025, tujipange kukamilisha ypte ya msingi, akiendelea, arndelee na mengine wakati ya msingi yamekamilika.
Watanzania tuendelee kuwa watu wa shukrani kwa kushukuru kwa yote, hata kama ni madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, hivyo tuendelee kusema asante sana Mama Samia kwa a good political will la kuruhusu mikutano ya siasa, kwa utashi tuu hivyo vyama na Watanzania kukushukuru kwa hisani yako hii, tunakuomba tumia a political will kama hii hii kuwaruhusu Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa!.
Wakati tukisubiria hisani ya Mama Samia kwenye hili, kupitia marekebisho ya sheria mbalimbali na kumruhusu kila Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa, naendelea tuu kukumbushia kuwa
Haki ni stahiki sio hisani!, haki haiombwi na kutegemea hisani, wala haki haihitaji vikao, mikutano na majadiliano na maridhiano kuzijadili haki, na haki hauletewi kwenye kisahani cha chai kama hisani, fadhila au zawadi, haki ni stahiki inayopaswa kutolewa unconditional bila masharti yoyote, Haki is a right, inayopaswa kutolewa unconditional na isipotolewa, haiombwi, wala haibembelezewi kwa vikao vya maridhiano, bali hudaiwa, na katika kuidai huku kukishindikana kuidai kwa amani na kisheria, ndipo nguvu hutumika kuipigania, kwa kuweka mashinikizi ya mikutano na maandamano ya kudai haki hizo na sio kuziomba, na hapa ni pale tuu inapobidi, baada ya njia nyingine zote kushindikana ni katika kuipigania huku kuna wakati machozi, jasho na damu huweza kumwagika, katika kupigania haki.
Kwa vile Rais wetu Mama Samia, keshaonyesha utashi, kwa kauli na matendo, tuzidi kumuombea ili Mungu amuwezeshe ayaweze yote haya kabla hajamaliza awamu yake hii ya kwanza, ili hata ikitokea akaendelea kwa awamu ya pili, hiyo itakuwa ni awamu ya shukrani na kumpa asante kwa aliyotatenda, na sio awamu ya kukamilisha ambayo hayakumamilika.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania