Asante sana we mdada ulionilipia nauli

Asante sana we mdada ulionilipia nauli

Nadhani upo humu,

Kama kweli basi pokea asante yangu. Ilikuwa hivi:

Naamka najiandaa kwenda job, Naingia kwenye gari kuweka switch on kitaa cha wese kina blink, sio kesi ni kawaida tu matarehe yakichachamaaga hivi kulitelekeza gari na kujiunga na public transport.

Mzee baba nikachomoka kwenye gari nikakimbilia kituo cha daldala chaap, (nilikua nishachelewa)
Nikazama nikapambania siti, hatimae nikapata safari ikiendelea ulekeo makumbusho,

Baada ya vituo kadhaa konda huyoo anapitia kudai chake, nikajisachi mifuko yote hakuna hata silva ukiachana na masimu tu. Hee nikakumbuka kumbe mzigo niliuacha pale kwenye gari nikaamka kama nilivyo. Nilifanikiwa kuokota simu tu! Daah itakuaje.

Konda alivyoona nazidi kujisachi bilamafanikio huyoo akaendelea siti nyingine. Baada ya muda konda huyo karudi tena. Daah Leo nishaumbuka!

Nikamwomba konda kwa upole kua pesa ipo kwenye simu nashuka mwisho wa gari nitakutolea kwa wakala nikishuka.

Dizaini konda akataka aanze kuzingua pale "tatizo muda" Daah mzee baba nikaona mzee mzima naumbuka leo. Basi nikatulia zangu tu siti ya upande wa pili kuna mdada kumbe alishachora michoro yote.

Ki buss hichoo kinaingia makumbusho huku naangazaaangaza sehemu ya mpesa nikishuka tu nimtolee konda pesa yake mwishowe kibasi kikasimama. Konda kakomaa mlangoni abiria ndio tunashuka.

Ghafla Mdada (mrembo) akanifata akaniminyia jero "mpe hii konda". Daah sijaamni macho yangu.

Nilishindwa kukushukuru pale public nimeona nije nikushukuru huku. Asante sana.
Ulikuwa falla man, ulipaswa umwambie akusubiri.
Uchukue namba, mchana umkaribishe lunch au baadae umrushie ten.
Ni nadra kuionja pesa ya mwanamke so ukipewa kiroho safi jiongeze
 
Watu wahumu wazinguaji sana ok huna hela ya mafuta na Uber? Hakuna kitu inaboa Kwa hii dar kama unamikiki gari na harakat zako ni za private car alafu uje ukapande daladala inakuwaga kama uko jela
Kawaida tu mbona? Huwa tunaset budget kwa mwezi may be utumie gharama ya mafuta say 400k. Au fultank 3.
 
Ulikuwa falla man, ulipaswa umwambie akusubiri.
Uchukue namba, mchana umkaribishe lunch au baadae umrushie ten.
Ni nadra kuionja pesa ya mwanamke so ukipewa kiroho safi jiongeze
Hapo ndio nilibugi. Dada alikua mrembo hasa. Na nyash analo.
 
Kuna mmoja alionyesha ukarimu akaninunulia vinywaji; kilichofuata, alivikimbia vinywaji, vilikuwa vinakuja kama mvua; kwa kifupi ukarimu unalipa
 
Angekuwa na uoga kama angelipiwa na mwanaume mwenzie,acha kumtisha buana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Namzingua tu! Kijana ameweseka sana pale konda alipokua anatikisa chenji halafu mfukoni yupo teeeh! 😂😂😂😂
 
Namzingua tu! Kijana ameweseka sana pale konda alipokua anatikisa chenji halafu mfukoni yupo teeeh! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ata ingekua ni mimi lazima ningeweweseka makonda huwa wanakauli mbaya saaana [emoji3][emoji3][emoji3]
 
PESA ya jini huwa haisauliki utalipiwa tena mkuu uskonde
 
Watu wahumu wazinguaji sana ok huna hela ya mafuta na Uber? Hakuna kitu inaboa Kwa hii dar kama unamikiki gari na harakat zako ni za private car alafu uje ukapande daladala inakuwaga kama uko jela
913C0562-96CF-4F79-8C29-72DA01C8C49B.jpeg
 
Back
Top Bottom