Asante sana we mdada ulionilipia nauli

Asante sana we mdada ulionilipia nauli

Nadhani upo humu,

Kama kweli basi pokea asante yangu. Ilikuwa hivi:

Naamka najiandaa kwenda job, Naingia kwenye gari kuweka switch on kitaa cha wese kina blink, sio kesi ni kawaida tu matarehe yakichachamaaga hivi kulitelekeza gari na kujiunga na public transport.

Mzee baba nikachomoka kwenye gari nikakimbilia kituo cha daldala chaap, (nilikua nishachelewa)
Nikazama nikapambania siti, hatimae nikapata safari ikiendelea ulekeo makumbusho,

Baada ya vituo kadhaa konda huyoo anapitia kudai chake, nikajisachi mifuko yote hakuna hata silva ukiachana na masimu tu. Hee nikakumbuka kumbe mzigo niliuacha pale kwenye gari nikaamka kama nilivyo. Nilifanikiwa kuokota simu tu! Daah itakuaje.

Konda alivyoona nazidi kujisachi bilamafanikio huyoo akaendelea siti nyingine. Baada ya muda konda huyo karudi tena. Daah Leo nishaumbuka!

Nikamwomba konda kwa upole kua pesa ipo kwenye simu nashuka mwisho wa gari nitakutolea kwa wakala nikishuka.

Dizaini konda akataka aanze kuzingua pale "tatizo muda" Daah mzee baba nikaona mzee mzima naumbuka leo. Basi nikatulia zangu tu siti ya upande wa pili kuna mdada kumbe alishachora michoro yote.

Ki buss hichoo kinaingia makumbusho huku naangazaaangaza sehemu ya mpesa nikishuka tu nimtolee konda pesa yake mwishowe kibasi kikasimama. Konda kakomaa mlangoni abiria ndio tunashuka.

Ghafla Mdada (mrembo) akanifata akaniminyia jero "mpe hii konda". Daah sijaamni macho yangu.

Nilishindwa kukushukuru pale public nimeona nije nikushukuru huku. Asante sana.
Yaani hata mkiwa mmeshuka hukuweza kutoa shukran?
 
We mtoto wakike ni rahisi kumlainisha sio mpaka uumpe mahela mengi, we ukimpa tu ya vocha imetosha yaani lazima aingie kwenye laini

Taratibu ataanza kujipa mwenyewe, kwanza uzuri wanawake wanajua ukiwa anadate na mtu hoihoi anamfahamu kitambo kwahyo anatafuta namna ya kuishi naye

Alafu pia mademu wetu hawa huwa kuna vitu wanapenda kwa mtu unaweza ukawa na hela ila asikupende ila unaweza ukawa kijikuku tu fulani ila akavutiwa na ww

Ki ukweli hawa mademu ni wanamaajabu
mshamba_hachekwi ona Kaka yako Huku.

Kwahiyo vocha inatosha? Hawajawai kueleweka ila tafuta hela utapunguza kelele na dharau za Ke wengi.
 
Wamebaki wanaJF wachache sana hawamiliki magari.
 
Ndio mjifunze kutoa lift na magari yenu ya mkopo hayo, mnatuvimbiaga sana ist zenu
 
Back
Top Bottom