Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Sijasoma vitabu vingi sana, lakini alau nimevisoma soma kidogo.

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, nimeweza kusoma Vitabu vichache, vikubwa kwa vidogo, vinavyozidi mia nne.
Hivi 400 ina sirii gani sijui huyu kala wanawake 400 mara wewe umesoma vitabu 400 sasa naomba kujua mia nne ina siri gani?
 
Sijasoma vitabu vingi sana, lakini alau nimevisoma soma kidogo.

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, nimeweza kusoma Vitabu vichache, vikubwa kwa vidogo, vinavyozidi mia nne.

Nimeiona faida yake. Kuna faida sana. Ni CHAKULA muhimu sana cha akili, hakika!.

Mara tu baada ya kuianza hiyo tabia, nilijaribu kuwashawishi baadhi ya watu, hasa wasomi, kuiga hiyo tabia. Kuna siku, nafikiri nilikosea, nikaenda kumshawishi mtu aliyenizidi kitaaluma naye awe msomaji. Alichonijibu kilinifanya nisirudi kwake tena kwa sulala hilo. Niliamini, usomaji wa Vitabu ungweza kumwongezea mawazo ya kuboresha shughuli alizokuwa akizifanya.

Siku ya kwanza, pengine alinivumilia, hakunijibu chochote.

Nilipoamua kumpelekea orodha ya vitabu nilivyoamini kuwa vingemfaa, aliishia kunijibu, "hivyo Vitabu havifanyi kazi Tanzania"

Havifanyi kazi Tanzania? How? Kisa tu vilikuwa vimeandikwa na Wazungu? Iweje visifanye kazi Tanzania, wakati vingi ya Vitabu alivyovitumia Chuo Kikuu vilitoka kwa Wazungu?

Namshukuru Mungu sikutetereshwa na kauli yake, ila na mimi sikurudia kumshawishi katika hilo. Niliendelea kujisomea, na sasa imeshakuwa ni tabia yangu.

Nahisi, maarifa niliyoyapata kwa kujisomea mwenyewe vitabu nilivyojichagulia, yamenisaidia zaidia kuzidi maarifa niliyoyapata chuo kikuu.

Vitabu, hasa Vitabu vizuri, haviwezi kukuacha kama ulivyokuwa. Ila ukivisoma "visivyo" salama kwa akili, utakuwa hatarini pia.

Soma vitabu vizuri, hutajutia.

Wanasema, LEADERS ARE READERS!

Soma VITABU, Vitabu vizuri! Vina faidi tele!

Dhamini Vitabu kuliko unavyoldhamini chakula cha kawaida, ni CHAKULA muhimu sana cha akili yako.
Nakubaliana na wewe.
 
Brother mwenye uzi huu ubarikiwe nilisoma vitabu viwili tu hapo hicho cha Robin na cha James vilinibadilisha sana.

Matokeo yake
Nimepata connection na watu wanaopenda vitabu kama mimi wapo USA .

Nimepata nafasi ya kutafsiri hicho kitabu cha Robin na James kwa kiswahili.

Nimejifunza digital translation and interpretation ambayo mwanzo sikuijua.

Nimejifunza graphics and designs kwa kujisomea tu.

Mwishi elimu haina mwisho kutokana na juhudi nilizozionesha nimepata sponsorship ya kufanya Masters.

Tusiache kusoma.
 
Back
Top Bottom