Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania




Asante kwa kijistori kizuri. Ila heb check kama umefanya spelling error kidogo hapa: Kariakoo -Carier crop
 
Kwa azizi ali, ni nina la mzee maarufu pale anaitwa Azizi Ally sasa ni marehemu
 

1. Kwa kuongezea tu kuhusu Dar as Salaam, ni jina linalopatikana ndani ya Qur'an Surat Yunus aya ya 25 (Yunus 10:25) na linamaanisha Nyumba (Makazi, Dar = home) ya Amani. (Abode of Peace) na si "Bandari ya salama" kama wengi wanavyotaka iwe.

Sahih International

And Allah invites to the Home of Peace and guides whom He wills to a straight path

Swahili
Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka.
[FONT=me_quran]وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
[/FONT]​


Baadhi ya nchi zenye majina ya miji yenye jina hilo ni pamoja na Jerusalem (maana yake ni hiyohiyo) na Dar us Salaam, Brunei.
 
we hujielewi.kwanza hapa c mahala pake kuweka huu uongo wako,pili kama unataka kukanusha maneno yangu basi uje na majina asilia ya sehemu hizo kabla ya kubatizwa kua na hayo majina mapya.
Hujasomeka kabisa hapa
 
kigamboni imetokana na jina la mzungu KEAGAN BONNY

Hii ya Keagan Bonny na ile ya Michael Chain nazitilia maswali.

Ninavyojua mie "Mikoche" ni aina fulani ya miti iliyokuwepo kwa wingi maeneo ya Mikocheni.
 
ROMBO. Dada zetu walikuwa wanapenda sana ule mchezo wa waliooana. chaajabu wakawa hawaridhiki. wageni walipofika kule wakakuta vile wakasema. hawa wasichana ni waroho wa Mb....... so wote wa kule ni Waroho wa .....oo. mpaka leo ni Warombo

Duh,aksante..
 
kuna anayefahamu buguruni-malapa, kimara-temboni,changanyikeni,makongo,goba,tegeta na bunju vilitokana na nini?

Buguruni malapa niliwahi kusikia kuwa kulikuwa na mzee mmoja maarufu sn hapo buguruni alikuwa anaitwa malapa so ndio ikawa buguruni malapa.
 
Majina mengi ya vitongoji yanatokana na majina ya wazawa wa hapo au vitu asili mfano
1.Tandale kwa Tumbo--Kuna mzee aliishi maeneo ya hapo miaka ya 60's na alikua na bar na alikua na bonge la kitambi(Tumbo) amebaki mtoto wake m1 tu ndio anaishi kwenye nyumba ya baba yake.

2.Kawe Ukwamani---Pale kitongoji kulikua na wakzi wazaramo kutoka ukwama ambao asili yao ni mabwepande ndio walikua wenyeji wa kwanza pale kawe na ndio jina la ukwamani lilipoanzia(wakwama)

3.Kwa Bonge:Kuna Jamaa fundi magari ni mnene kupita kiasi zaidi ya wacheza sumo na jina lake ni Bonge

Pendelea kuangalia Channel 5(EATV) zembwela anafanya vipindi kama hvyo
 
kawe-cow road!kulikuwa na barabara ya ng'ombe kwenda kiwandani wazungu wanatamka cow road wabongo wanachakachua kawe!

Tilly,
Ni COW WAY (Kawe) sio Cow road. Ilikuwa njia ya ng'ombe waliokuwa wanapelekwa pale Tanganyika Packers ambacho kilikuwa kiwanda cha nyama kwa wakati huo.
 
tangi-bovu...zamani kulikuwa na tangi kubwa bovubovu hivi...!

Tangi hilo la chuma limedondoka juzi juzi tu, nadhani 2000~. Nguzo zake za zege bado zimesimama, pembeni ya zile nguzo za umeme
 
Majina mengi humu naona waanzilishi ni Wzungu, Wahindi, Wachina, Waarabu: hivi hakuna mbantu hata mmoja aliyeanzisha jina wenzie wakalifata? Just curious
 
ILALA- Hailalallah... Waislamu walikuwa wakisema Hailallah... yaani mola tu anayepaswa kuabudiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…