Na katika haya maeneo uliyotaja yote yalikuwa ni mashamba na maeneo manamba walipokuwa wanafanyia kazi au kuishi kipind cha ukoloni na maeneo hayo hakuna wachaga wengi utakaowakuta labda ni wafanyabiashara tuu, ni maeneo ya watu wa hali ya chini na hata serikali haina mipango ya maendeleo nimekwishafanya reseach huko.
Maeneo wanayoishi wachaga mf. Marangu, rombo, hai, machame, kibosho, uru, old moshi, kilema n.k ni vigumu kukuta waislamu kwa sababu zifuatazo
1. Waarabu walipokuwa wanasambaza uislamu hawakiwahi kufika huko wengi waliishia mwambao wa pwani na wamishionari waliokuwa wanasambaza ukristo ndo walikuwa wa kwanza kufika huko
2. Maeneo haya(ardhi) iko kimgawanyo wa koo na wachaga wanarithishana hawauzi ardi kwa mtu wa nje ya ukoo na wakifanya hivyo ni lazima wawe wanamfahamu fika na atakuwa wa ukoo ambao wanalandana(ni vigumu sana kwa mtu wa machame kupewa ardhi marangu) au mwanamke akipewa ardhi hata akiolewa ardhi hubaki kama ya ukoo hii haitoi mwanya kwa waislamu kuingia na kusettle na kueneza dini yao maeneo ya wachaga
Maeneo ya same, mwanga hedaru makuyuni yaliyokuwa ni maeneyo ya uzalishaji wa mkonge n.k kipindi cha ukoloni asili ya watu wake wengi ni kutoka maeneo ya mtwara, lindi, tabora, kigoma na maeneo ya mwambao wa pwani ambapo uislamu ulikuwa umeenea hivyo walivyokuja kama manamba(pitia ukoloni na uzalishaji tanganyika) wakaleta na kueneza uislamu hivyo kukua sana maeneo haya ambayo hayakuwahi kukaliwa na wachaga hata kabla ya ukoloni
Ugumu wa uislamu kuenea uchagani ni sawa na ugumu wa ukristo kuenea Zanzibar(truth). Ili huku bara ukristo na uislamu utaenea sambamba (umeshaenea) kila mahali pwani na bara kutokana na sababu zifuatazo
1. Mahitaji ya huduma za kijamii mf. Shule, hospitals. Taasisi nying za kikristo zimejikita kutoa hizi huduma
2. Mahitaji ya kiuchumi, watu wanahitaji pesa kwa biashara hata kuuza maeneo yao ili wapate fedha ma kuendesha gurudumu la maisha(wakristo na waislamu wananunua)
3. Kukua na kupanuka kwa miji, kunaifanya kuwe na mchanganyiko wa watu wa aina na dini tofauti kuingiliana
Cha msingi ni kufanya kile kinachokupasa kufanya ukifatilia maisha ya wakristo na waislamu kukua na kuenea kwao haitakaa ikusaidie na wala haitakaa ibadilike uislamu kuenea kwa maeneo ya wachaga na wala ukristo kuenea zaidi zanzibar
Mkuu
Ritz uko biased sana unasahau wanachofanyia wakristo huko zanzibar, historia inambeba kila mmoja wetu nshakuona unaingiza na uchadema hufai katika jamii mtu kama wewe ni mchonganishi