Asiyetakiwa ni Waziri Mkuu Majaliwa, kila kitu kimepangwa, ajiandae kuachia ngazi

Asiyetakiwa ni Waziri Mkuu Majaliwa, kila kitu kimepangwa, ajiandae kuachia ngazi

Msimamo wa uchaguzi 2025 kukiwa na Tume huru ya uchaguzi ndio kutamfanya Samia ajue Rungu ni nani na alipatwa na nini kwenye uchaguzi Zambia.
Atakutana na ubao ukisema;
*Mgombea ACT Wazalendo: 4.8%
*mgombea NCCR 2.08%
*Mgombea CCM 39.8%
*Mgombea Chadema 52.01%
*Wengineo wote 2.2%.
Kwa kweli na iwe hivyo ndugu yangu Chakaza...
 
Hakuna cheo chenye lawama na kigumu kama cha uwaziri mkuu.

Binafsi naona majaliwa ana ustahimilivu mkubwa kwa kiasi chake, tokea enzi za hayati vile alivyokuwa anasemwa hapa na pale, mara kupigwa kwa shangazi zake.
Kipindi cha hayati kutoonekana na kufariki kwake majaliwa alibeba lawama kwa kiasi chake kwa taarifa zisizo wiana.

Kipindi alichopo sana yalipo tokea huko bungeni alisemwa yeye kimtindo, kauli ya huko bungeni kwa kina kasimu!

Kuletewa msaidizi , kuagizwa na muenezi aliye ofisini kwa siku mbili hali yeye yupo madarakani kwa miaka nane karibu.

Nadhani kabisa ameshajiandaa kisaikolojia ndio maana kila aonekanapo amejaa tabasamu.

Pamoja na yoote lakini amejitahidi sana kuongoza , wananchi hatuna deni naye.
Cheo cha waziri mkuu ni kigumu sana Tanzania kwakuwa wamekuwa hawaachwi watekeleze na kutumia mamlaka yao kama Katiba inavyotaka. Na hii inatokana na mamlaka ya juu yake kuhofia kumezwa na kupoteza umaarufu kisiasa.

Taasisi ya urais ni taasisi yenye wivu sana juu ya mamlaka yake, msione vile mawaziri na watendaji wote wanageuka machawa kila wakisimama ni "mheshimiwa rais dokta hoyee hoyee"
 
Hii point kama yale maneno ya kwenye amri kumi...mm ni mungu mwenye wivu..usiwe na miungu mingine ila mm
 
Yaani ukishaona watu wenye mdomo lakini hawana akili kichwani kama Paul Makonda na Philip Mulugo wanapewa jukwaa la kusema chochote juu ya ubovu wa baraza la mawaziri basi jua wazi kwa 100% system imewatuma. Ni suala la muda tu.
Baraza la mawaziri limetakiwa na makonda kumpelekea ripoti zao Kila nusu mwakan...ole wake ambae hatopeleka 😂😂😂
 
Ila mkuu uliyoyasema, kwa Lowassa yote yalikuwa yanafit - alifarakanishwa na wakuu wake chamani, wananchi wakawa wanamkubali ila bado kina JK wakamchinjia baharini
Wala sio jk!!ni wenye nchi Yao DS ndio hawkumtaka coz angeingia yangekua yale yale ya upigaji ya awamu ya nne halafu vurugu tu za visasi na wizi!!

Kumbuka kampeni zake zilifadhiliwa na wafanyabiashara wale ambao angewalipa fadhila na u Mungu mtu ungetamalaki nchini!!

Hata hivyo mlutheri asingeingia ikulu pia Bado wale jamaa wasingekubali!!
 
Teuzi ya Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu, teuzi ya Makonda kuwa msemaji wa CCM na blah blah za wabunge kuicharukia serikali ni mpango kamili na kabambe katika kutengeneza njia ya kumng'oa Kassim Majaliwa kwenye nafasi ya waziri mkuu. Kila kitu kwa 100% kimepangwa na kinachoendelea ni utelekezaji tu. Ni ama aachie ngazi kabla ya mwaka huu kwisha au wakati wowote mwakani.

Hakuna kipya au kitu cha ajabu, aliyebakia na asiyetakiwa ni Majaliwa tu. Magufuli alishatolewa, Ndugai alishatolewa, Lukuvi alishatolewa, Kabudi alishatolewa, Bashiru alishatolewa nk. hakuna kilichobakia wote wameshakwenda, bado Majaliwa tu, na safari yake ya kutolewa kwa 90% imeshaiva, ajiandae kukaa benchi.
CCM ITAPASUKA VIPANDE VIWILI CHALI, THEY SHOULD NEVER PRACTISE THIS EXERCISE, NEVER NEVER IT'S NOT A TIME TO DO THIS.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini hili.....kaka yake kbs katika imaan nasubiri atolewe nitaamini
kaka yake katika nini ?! Aloo makobazi huyajui mkuu
Screenshot_20231030-145554_Quora.jpg

makobazi hata mama mzazi yanampelekea moto sembuse kaka tena sio wa damu ila katika iman ?! Ebo unayajua makozi kweli wewe ?! Haya hua yanaweza hata lipigane lenyewe mikono ikipigana na miguu ya hilo hilo likozi limota.
Screenshot_20231017-090333_Quora.jpg
 
Teuzi ya Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu, teuzi ya Makonda kuwa msemaji wa CCM na blah blah za wabunge kuicharukia serikali ni mpango kamili na kabambe katika kutengeneza njia ya kumng'oa Kassim Majaliwa kwenye nafasi ya waziri mkuu. Kila kitu kwa 100% kimepangwa na kinachoendelea ni utelekezaji tu. Ni ama aachie ngazi kabla ya mwaka huu kwisha au wakati wowote mwakani.

Hakuna kipya au kitu cha ajabu, aliyebakia na asiyetakiwa ni Majaliwa tu. Magufuli alishatolewa, Ndugai alishatolewa, Lukuvi alishatolewa, Kabudi alishatolewa, Bashiru alishatolewa nk. hakuna kilichobakia wote wameshakwenda, bado Majaliwa tu, na safari yake ya kutolewa kwa 90% imeshaiva, ajiandae kukaa benchi.
Mbona beteko hajatolewa?
 
Kupitizia thread kama hizi mnazidi kumtia pressure mzee wa watu. Mtafanya mpaka superblack idunde, mvi zionekane.

Kama ana kamati yake ya ufundi wa jadi itakuwa inapiga pesa ndefu kwa sasa, keshatumwa mpaka ushuzi wa mwanamke bikra mwenye watoto mapacha .
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Binafsi sioni kama wanataka wamtoe ila CCM ni wajanja sana wanamtengenezea njia Majaliwa ya Urais.

Washaona hawana wakumsimamisha na mtu pekee alie katika system anae eleweka utendaji kazi wake ni PM.

Chakufanya ili wakamilishe mchezo wao, wanafanya kama kwa JPM kabla hajawa waziri, wanamchonganisha na wana CCM wengine abaki ONE MAN ARMY halafu wakishafanikiwa kumchonganisha.

Wanamtupa kwa wananchi, ambao kwa asilimia 90 wataona PM anafaaa, Chaguzi za Rais zikifika Jina CCM wanatoa jina la MAJALIWA. hakika lazima wapite na kijiji cha kura.

CCM ni moja ya chama ambacho kinapomuandaa Rais wake kinamfanya Adui wa chama adui wa wa ilani yake halafu kinaangalia respond ya wananchi.

Katika yanayoendelea sitoshangaa sana nikisikia Majaliwa kajiuzuru halafu akaja tena teuliwa kuchukua fomu ya urais kwa kulazimishwa.

Msiwaangalie CCM kama malofa hiki chama kina mfumo wa 4 4 2 ukikiangalia juu juu huwezi kielewa.
Hii inasaidia nini wakati yeyote watakayemuweka atashinda tu kwa katiba na tume iliyopo??
 
Back
Top Bottom