Askari aliyempiga mwanafunzi wa IAA asimamishwa kazi, SUMA JKT kufidia gharama za matibabu

Hata viongozi nao wote wamekurupuka... yaani wamechukua sheria kwa upande mmoja tu wa askari, vipi kuhusu mdada mwenyewe mnasemaje?
Kwanini mwanaume amrushie mateke mwanamke?

Umeona video ? Askari ndio alikuwa anashambulia
 
Wamekuwa wanyama? Wapata mafunzo stahiki yanayoendana na kazi zao, pia wasipachikwe bila ya vigezo na sifa kwa kujuana.
 
Nani atawalipa?
 
Askari unatakiwa uwe na nidhamu, unapokuwa mvunja amani, unapodhuru wengine, hufai kuwa askari. Ajitafakari!
 
Uliambiwa sababu ni kitambulisho? Au nawe unaonesha jinsi waTz walivyo finyu wa fikara?
 
Walinz wa suma wa magetin naona ni shida kila mahali.hapo wizara ya ardhi yule dada ka suma keupe hivi kale ukifika juz kanamfokea jamaa mmoja anasema anawah gorofa ya pili amechelewa kikao na wazir.anasema mpgie simu kakaanza kumtolea maneno.wanajikutaga askari wale kunbe sio.
SUMA kwanza nashaur wanafanya kaz sio zao unakuta wamegeuka receptionist
 
Huko makambini kwenye kulinda mipaka sifa/vigezo havikutosha ndiyo maana wamekuja SUMA..

Sasa kama na huku tena hawafai, inabidi itafutwe namna nyingine ya wao kujikimu!!!
 
Tusifike huku mkuu!!

Bado tuna muda wa kufanya marekebisho kama jamii..
 
SUMA wanajikuta wajeda maaniinaa zao waulize kilichowakuta Dar walipigwa chini na UDART kwenye mwendokasi baada ya kujifanya wanawanyoosha abiria , wao kila kitu ngumi mkononi, yaani kimsingi wale ni failures, na kazi za maana watazisikia kwenye redio, wenzao ulinzi ni pamoja na customer care sio mabavu tu
 
Inawwzekana huyo mwanafunzi alifanya ujeuri ndio maana akasababusha askari kupandwa na hasira.
 
kitendo hicho kilichotokea baada ya majibizano kati ya Askari wa SUMA JKT na mwanafunzi ambayo yalipelekea kitendo hicho.
Usikute hapo Dent alimropokea Mlinzi kwamba utanibabaisha nini mtu mwenyewe unalipwa alfu 70 kwa mwezi. Wanafunzi hasa wa vyuo huwa wanajikuta ni kama wanaishi visiwa vya Sayari ya Mars wanasahau kabisa kwamba wanaishi na jamii ambayo inahitaji nidhamu!
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]acha kabisa
 
Askari unatakiwa uwe na nidhamu, unapokuwa mvunja amani, unapodhuru wengine, hufai kuwa askari. Ajitafakari!
Nidhamu inatakiwa kwa pande zote.....raia wanatakiwa wawaheshimu askari na askari wawaheshimu raia........ upande mmoja unaposhindwa kuchunga nidhamu Kwa mwenzie ndio majanga yanaanza....... uvumilivu una ukomo wake.....
 
Ilikuwaje please?
Ni kutokuelewana tu kishwahili hapo kati ya mtu aliyehitimu elimu ya kidato cha sita na elimu ya chuo kikuu, dhidi ya yule aliyeishia kidato cha nne, halafu akaenda kupata mafunzo ya muda mfupi ya kijeshi! Huku akihubiriwa muda wote kwenye mafunzo yake kuhusu utii bila ya shuruti na nidhamu.

Sasa mtu kama huyo akikutana na mtu wa kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye kila jambo; haki ya nani lazima akili yake ivurugike.
 
Tatizo watanzania huwa mnaangalia upande mmoja

Watanzania wengi wana dharau Sana hasa hawa mabinti ambao wanasoma chuo

Wanahisi wamefika peponi kwa hivyo vidigrii vyao na inawezakana huyo mwanachuo alimtolea lugha chafu huyo mlinzi
 
Hao Suma JKT wana mawazo sana wengi wao waliwaza baada ya kumaliza kozi zao wangeajiriwa na JWTZ,TANAPA,Polisi nk.
Sasa kwenda kulinda kwenye mageti kuna wapa mawazo sana hadi wengine hasira zinapanda na kupiga hovyo watu.
Hao unaowaona suma jkt sio wale wanaotoka kwenye kambi za jkt, ni raia tu wa kawaida wanachukuliwa kwenda mafunzo kidogo na kuanza kupangiwa lindo.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…