DOKEZO Askari huyu aliyeomba rushwa waziwazi bado yupo kazini?

DOKEZO Askari huyu aliyeomba rushwa waziwazi bado yupo kazini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nchi imeoza imebaki mifupa t

Wakuu,

Katika nchi ambayo ina uwajibikaji na Polisi inafanya kazi kweli sio kuweka “Patrol za Mtandaoni” kusaka wanaoikosoa Serikali na kuhamasisha uwajibikaji, askari huyu alitakiwa kuwa ameshachukuliwa hatua na hata umma kufahamishwa hatua zilizochukuliwa.

Tunao TAKUKURU, wanatumika kama political weapon badala ya kufanya kazi tarajiwa.

Nchi imevurugwa hii!

Hebu angalia video yenyewe
Halafu kiingereza ni kibovu sana.
 
Atawajishwa na nani wakati wote ndiyo kazi wanayofanya.

Kosa lake ni ufala wa kuamini kuwa watasha ni mafala kama waswahili.

Usikute kaajiriwa kwa kinoti cha ndugu yake.

Siku hizi hakuna askari bali matapeli wanaotumia ngao kupiga pesa.
Kiingereza ni kibovu sana. Halafu hata Jiografia hajui huyu kenge, anauliza eti unatoka Florida? Kwani Florida ni nchi? Pumbavu sana, wanatuletea aibu sana.
 
Halafu kiingereza ni kibovu sana.
kuandika kiingereza katika nyaraka za kiserikali kwenye nchi inayotumia kiswahili kama lugha ya taifa ni uhaini, polisi wawajibishwe kwa kuizalau lugha ya taifa na kwa kuitia makandokando lugha ya mkoloni.
 
Trafiki kupewa pesa za bure wanaona ni hali yao.
Nchi imejaa wezi sana..)()()
 
Wakuu,

Katika nchi ambayo ina uwajibikaji na Polisi inafanya kazi kweli sio kuweka “Patrol za Mtandaoni” kusaka wanaoikosoa Serikali na kuhamasisha uwajibikaji, askari huyu alitakiwa kuwa ameshachukuliwa hatua na hata umma kufahamishwa hatua zilizochukuliwa.

Tunao TAKUKURU, wanatumika kama political weapon badala ya kufanya kazi tarajiwa.

Nchi imevurugwa hii!

Hebu angalia video yenyewe
pesa walizopewa 29oct kuuwa watanganyika zimeisha sasa wameanza usenge wao
 
"Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake

Ila mnapokula angalieni msile mpk mkavimbiwa."

Polisi hawezi kuvimbiwa kwa kuchukua TEMBO mmoja
 
Give me utafikiri ni pesa za babake.
Halafu akaambiwa ,” give me my licence, I have to go… that’s illegal”. Na huyo Askari akamrudishia lessen.
Swali, Kwa nini alimsimamisha, kumuomba leseni, rushwa, na kumrudishia tena? Nimemuhurumia huyo mama Askari Kwa aibu alizopata kisa tu malipo kiduchu ya kazi zao yanayopelekea vishawishi vya kuomba rushwa. Mungu awasaidie sana hawa Ndugu zetu wapewe mishahara mizuri wayamudu maisha bila kubangaiza huko barabarani..
 
Hakuna atakaewajibishwa hapo. Tena uyo mzungu angekua mbongo yeye ndie angegeuziwa kibano. Ungesikia anashikiliwa kituoni kwa kosa la kuzuia askari kutekeleza majukumu yake.

Hawa pokisi wakikusimamisha kama mpo wawili mwambie mwenzako rekodi maongezi kama hivi. Vinginevyo ukikataa kutoa rushwa utageuziwa kesi.
 
Back
Top Bottom