Ukwaju,
Janjaweed na wengineo wote katika mjadala huu.
Hoja nikwamba tunahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kujenga ushirikiano mzuri, bora na makini kwa majirani zetu.
Ujirani bora ni moja ya kujihakikishia usalama wa uhakika na zaidi matokeo bora ya vizazi vyetu hapo baadaye.
Sio sahihi wala hakuna tija kwetu kuwa na kiongozi
anaeshindwa kuishi anachukihubiri kwa wangine, anawaasa
wanyarwanda kuketi mezani lakini yeye hawezi kutekeleza kwa vitendo anachokihubiri.
Nitatowa mifano.
1. Ameshindwa kukaa na kagame ili kurekebesha tofauti zao katika anga za kimataifa (tatizo dogo kabisa lakini ......)
2. Ameshindwa kuketi mezani na waalimu waliokuwa wakidai maslahi bora na malimbizo yao (matokeo elimu ovyoooo...)
3. Ameshindwa kuketi mezani na madakitari waliokuwa wakidai maslahi bora, vifaa tiba nk (matokeo afya ovyoooo...)
4. Ameshindwa kuketi na wanamtwara kuwapa japo matumaini ya watapata mgao gani kama walinzi shirikishi kutoka mapato ya gesi. badala yake nikupiga nakulazimisha nasio kuketi mezani...........
5. Ameshindwa kuketi na waislam (kuhusu madai mbali mbali, bakwata, Ponda, sijuwi Necta nk) anangoja waandamane awapige na mabomu......why???? kwanini usubiri watu waandamane nawewe unaamini suluhisho ni majadiliano.........
6. Ameshindwa kuketi na CDM kujadili sintofahamu mbalimbali ikiwemo mauwaji na upigwaji mabom mikutano yao.
Sasa nakuulizen[MENTION] Ukwaju[/MENTION],
Janjaweed na wale wenye mtazamo kama wenu.
a) Baada ya kupitia mifano hiyo hapo juu, kikwete anapata wapi ujasiri wa kuvuka mipaka mpaka Rwanda kutoa ushauri ambao yeye hawezi kuutekeleza hapa nyumbani kwa vitendo?
b) Kama tatizo ni wahamiaji haramu, niwanyarwanda tu ndiyo wahamiaji haramu?
i) walioingia tangu enzi zile wakaowa na kuzaliana wanawekwa fungu gani (DW radio jion hii ndoa na familia zimetenganiswa.......taratibu zinasemaje?)
ii) Tumeshuhudia chombo na askari wetu kuzamishwa-ziwa Tanganyika na kuuwawa, kutoka mpaka wa DRC-kikwete amechukuwa hatuagani na kwanini iwe rwanda na isiwe DRC Pia? nini kipo nyuma ya hili jambo.........
c) Ukipita mitaa ya kariakoo na hata mikowani, tunawahamiaji haramu wanaojiita wawekezaji hususani wachina wakiuza bizaa ambazo watanzania wachini ndiyo biashara zao. Je kanuni na taratibu za uwekezaji zinasemaje na nini kinaendelea
d) Je kunasababu ya lazima kikwete kutumia Kipindi kizima akizungumzia mgogoro wake na Kagame pekee akisahau majanga mengine kama,
madawa ya kulevya wengi wanaangamia kwa maelf, huduma mbovu za afya na wengi wanakufa nk.
karibuni tutafakali hili pulukushani iliyopelekea sote kushuhudia tulivyo wazi na dhaifu kiasi kwamba tumeajiri wageni na
kuwapa vitengo muhimu kabisa kama huyu mwanajeshi katika mada hii tunayoijadili
-Je kwa maamuzi ya kukurupuka na fukuzafukuza tutasalimika ikiwa maaduwi wametapakaa kila secta mpaka jeshini....???
-
Kama nyerere angewafukuza waganda tunaitafakali vipi vita ya uganda..............................
............................................................................................................................................