Siku ya kufa nyani....,Sasa si angepita getini?
Unamuambia tu mlinzi, mimi askari. Unatoa kitambulisho na Radio call, over.
Umepata taarifa ya tukio fulani kutokea. Unatokomea unakojua wewe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku ya kufa nyani....,Sasa si angepita getini?
Unamuambia tu mlinzi, mimi askari. Unatoa kitambulisho na Radio call, over.
Umepata taarifa ya tukio fulani kutokea. Unatokomea unakojua wewe.
Kwa hiyo serikali iwanunulie chakula?Ndo wajue sasa sirikali vyakula ni bei ona poti alkua anashika uelekeo wake na kiepe kavu
Poti ana maisha duni sana😂 kukimbia na chips kweliHapa umefanya nicheke mpaka nisahau bei za vyakula iliyopanda
Na chps nazo anakimbia nazo ,bado usikutee na pesa kamuibia dem ....Askali mwizi na msiba wake sihudhurii na rambirambi sitoi. Penzi ale na simu aibe?. Marehemu jambazi
Na alitoroka job maana ukiwa na radio call ni kwamba upo on dutyAskari mzima hovyo. Anatoroka hadi na Kiepe
Utata mwingi sanaAskari Polisi jijini Arusha mwenye namba Pf 18530, Stewart Saiba(40) amefariki dunia katika mazingira ya utata katika nyumba ya kulala wageni ya Mrina shine iliyopo makao mapya jijini hapa.
Taarifa za awali kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina Lake lihifadhiwe zimedai kuwa, Saiba aliingia katika nyumba hiyo majira ya saa sita usiku akiwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakufahamka mara moja .
Aliieleza kuwa marehemu aliandikisha katika kitabu cha wageni na kupewa chumba namba tano na kisha kuingia katika chumba hicho akiwa na mwanamke huyo, kibegi kidogo cha mgongoni na radio ya mawasiliano aliyokuwa ameshika mkononi.
Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.
Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa ,Justin Masejo ili kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba mara baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kutopokelewa.
Mwili wa marehemu Stewart unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kwa ajili ya maziko, baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Mwenyezi mungu alilaze mahala pema peponi roho ya marehemu Stewart, Amen!
Labda lakini..... na mi nimejizuia sana nisicheke, na kwanini aruke ukuta? Au kauwawa?Labda alikuwa kazini, hata hyo simu aloiba alikuwa anakazi nayo...
Labda lakini.