Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Najiuliza wamejuaje kwamba alikuwa anamtoroka mwanamke!??

Je huyu marehemu alimwambia mtu kuwa nipo na demu nakula show, ila nikimalizana nae nitamtoroka!??

Pia kwa maaskari wetu walivyo wababe sidhani kama angehitajika kuruka geti, pale ilikuwa anakwenda kumface mlinzi na kumuamuru amfungulie hata ikibidi angejitambulisha,, mlinzi asingegoma asilani

Kuna utata ktk hili
Hawamajitu wanaiba wake za watu Sasa wamekutana na wahuni wa ngalelo mamfya wamemuua na Kisha kuweka visingizio vya kuiba had na simu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kalala njaa( chips zake hajala)pili ni mwizi (alikuwa anatoroka cm ya huyo mwanamke wake)tatu tumwesabu kama kibaka (kwa nini aruke ukuta)nne ni nanga (unaruka ukuta unafikia kichwa?)ina maana kwenye mafunzo hakupitia vikwazo?ua alikuwa doja labda.

R.i.p pot uliekuwa kizembe.
Alafu ukute hata mzigo hajala.
Inauma sana
Ukute alikuwa tungi pia
 
Kwa hiyo hakula Mzigo? Hakuiba simu? Hakuondoka na Chips ? Hakuruka Ukuta? Hakwenda na yule demu pale Guest??? Usitoe statement nyepesi nyepesi hivyo...
Mtu mwenye akili timamu hata kama alikuwa anamkimbia dem hakukuwa na sababu ya kuruka ukuta, alafu ukakasi zaidi ni kwenye kuruka na kudondokea kichwa sijui akapasuliwa na kitu kichwani....ni upishi tu. Afande aliuliwa na kurushwa nje ya ukuta, upelelezi utafichua kila jambo na wahusika watakamatwa.
 
U
Jamaa yangu alikuwaga njaguanasema kama wakati ule wanakwe da kukamata bitchies pale kona bar unaambiwa wanawapitisha sehemu ya giza afu wanaanza kuwapiga mashine vibaya sana baadae ndo wanwapeleka Selo!!
Uongo huo
 
Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
 
Askari Polisi jijini Arusha amefariki dunia katika mazingira ya utata katika nyumba ya kulala wageni ya Mrina shine iliyopo makao mapya jijini hapa.

Taarifa za awali kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina Lake lihifadhiwe zimedai kuwa, Saiba aliingia katika nyumba hiyo majira ya saa sita usiku akiwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakufahamka mara moja .

Aliieleza kuwa marehemu aliandikisha katika kitabu cha wageni na kupewa chumba namba tano na kisha kuingia katika chumba hicho akiwa na mwanamke huyo, kibegi kidogo cha mgongoni na radio ya mawasiliano aliyokuwa ameshika mkononi.

Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.

Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa ,Justin Masejo ili kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba mara baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kutopokelewa.

Mwili wa marehemu Stewart unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kwa ajili ya maziko, baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Mwenyezi mungu alilaze mahala pema peponi roho ya marehemu Stewart, Amen!

===================

View attachment 2477611
View attachment 2477612
Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine
 
da kaondoka na zambi mbili za faster UZINZI na WIZI wa simu a demu bado zingine alizokuwa nazo mwanzo na kaondoka bila kutubu pengine alikuwa anawaza kesho aende kutubu
Uchoyo,ulafi na mawazo mabaya ya kukufuru uumbaji wa Mungu nazo ziongezwe.Askari gani mzembe asiyetumia vema akili yake?
 
Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Kwamba walikuwa wanamfuatilia kwa nyuma au walimuona kwenye kamera?Wawe makini.
 
Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine
Ina maana mwandishi/mleta habari alipewa hadi fursa ya kuangalia na kuhesabu vitu alivyobeba(vinavyosadikika) askari aliyetoroka maisha?
 
Najiuliza wamejuaje kwamba alikuwa anamtoroka mwanamke!??

Je huyu marehemu alimwambia mtu kuwa nipo na demu nakula show, ila nikimalizana nae nitamtoroka!??
Ukiunga dot unapata jibu wala huhitaji kuumiza kichwa
  1. Jiulize kwanini aruke gate/ukuta wakati mlinzi yupo na angeweza kumfungulia mlango apite
  2. Alitoka na simu ya mwanamke aliyekuwa naye chumbani ya nini?
 
Bora wewe umeamua kutumia akili kidogo, na bado hii taarifa ni ya upande mmoja.
Polisi wanatabia ya kukurupuka sana katika kutoa Taarifa.
Polisi wanachongena sana.

Uzinzi Kwa Wanandoa umekua ni mkubwa sana na Sasa Panaibuka Wanaharakati wa kuhamasisha kuishi bila ndoa mana wengi hawana ndoa .
Ukifika Polisi ukakutana na watu wanaoitwa wa dawati karibu wote ndoa zao zimevunjika na karibu wote ni wazinifu.
Hali ya Ndoa ni mbaya sana.
Hapo ndio utashangaa kama kweli Kuna viongozi wa dini makini au hata wananchi wanawawakilishi makini Bungeni wenye uwezo wa kutunga SHERIA ya kuwalinda watoto ambao wengi Kwa Sasa wanaishi maisha katikati ya migogoro inayojenga chuki kubwa kati ya watoto na wazazi.

Kuna Kada mmoja wa Chama tawala ni WA hovyo kabisa Mpaka anasema kuwa yeye anapenda Chama kuliko watoto wake.
Walioko SERIKALINI na kwenye Chama wanapaswa kuwa kioo Cha jamii .

Tukirudi Kwa huyo Polisi hapo ni wazi kuwa ameuawa na ama Kwa kupigwa risasi au kuviziwa na kutwangwa rungu na walinzi wa Nyumba hiyo.
Kwa Hali ya kawaida kabisa huyo Polisi alikuwa anatokea Kununua Chips na bia. Wakati anarudi akajaribu kugonga geti mlinzi hakufungua ama Kwa sababu hakusikia au kulala au muda wa kufunga geti ulikua umefika na Haikuwa ruksa kufungua geti muda huo kutokana na Ujambazi na wizi wa Mji wa Arusha na mazingira ya kijambazi ya Jiji Hilo lenye baadhi ya matajiri Wahalifu, hivo ikabidi aruke ukuta . Hapo Mlinzi akahisi huyo ni mhalifu ikabidi amtwange na kitu kizito kichwani na kudondokea nje na kupoteza maisha .

Hapo ni wazi kuwa simu alikua ameondoka nayo ili adhibiti mawasiliano ya huyo Mwanamke au alidhani Mwanamke huyo ataweza kuamka na kumtoroka.

Usiku kutoka gest ni rahisi kuliko kuingia.
Hivyo hapakua na sababu ya kutoka Kwa kuruka ukuta. Ila kuingia gest usiku wa manane ni ngumu mana muda wa usiku sana wahudumu wanaogopa majambazi kuvamia gesti au watu kuja kufumaniana usiku na kusababisha taharuki.

All in all wanaume ni adui wa wanaume wenzao. Hata wanavuruga ndoa za watu ni wanaume, wanaouna sana ni Wanaume . Hali kadhali adui mkubwa wa Wanawake ni Wanawake,wanalogana ,wanachukuliana wanaume na wachumba na kutoroka na pesa za vikoba.
Wanaoathirika ni watoto.
 
Nani ana uhakika kuwa alikuwa anatoroka? Vipi kama alishambuliwa na kisha kuuwawa kisomi?
 
Kama alinunua chips kwann hawakuila mpaka anarudi nayo?

Kama bia aliingia nayo kwann hakuinywa au kumpa mwenzie mpaka anaamua kurudi nayo?

Kama mchezo umepewa mpaka mtu kalala fofo na wakati umeingia wahudumu walijua lazima utakuwa n Askari sababu ya rediokol sasa kulikuwa na ulazima gani aruke ukuta?

Kwa mazingira yale Kama alifanikiwa kumwacha Mwanamke akiwa amelala fofofo na kumchukulia simu yake huku chakula na bia akiwa navyo mkononi pamona na kutambulika kuwa n Askari sidhan Kama alishindwa kupitia njia ya mlangoni.

Hapa kuna shida nyingine zaidi ya hili mnalojadili humu.

Nataka hilo faili litoke polisi walikete ofisini kwangu kwa uchunguzi zaid
Unaijua pombe vizuri ikiingia kichwani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom