Askari wa Israel wavua magwanda,wakimbia wakiacha wenzao waungue kwenye kifaru

Askari wa Israel wavua magwanda,wakimbia wakiacha wenzao waungue kwenye kifaru

Katika hali ya kuzimwa data na umeme Gaza kuna mengi tunayokosa kuyaona.Hata hivyo machache yanayovuja kwa shida inaonesha vita huko ni kali kuliko ule ukali uliotarajiwa jeshi la IDF.
Mara kadhaa jeshi hilo limeshatangaza kuingia katikati ya Gaza lakini baadae ikaonesha kuwa bado wako pembeni kabisa wakitumia makombora ya kutoka kwenye ndege zao za kisasa.
Katika moja ya vidio zilizotolewa kwa shida na wapiganaji wa Hamas imeonesha kifaru cha Israel kikiripuka baada ya kupigwa na silaha hafifu.Baada ya hapo mmoja wa waendeshaji kifaru hicho akachomoka kwa nyuma huku akivua magwanda yake na kukimbia akiwaacha waenzake waungue ndani ya kifaru hicho.
Pembeni ya kifaru hicho vipo vyengine kadhaa vilivyotelekezwa baada ya ama kuharibiwa au askari wake kuamua kuviacha tu na kukimbia.
View attachment 2810206
mosadhiyo ni vita mura, kupigwa sometimes sio kitu cha ajabu. nakushauri nenda kwenye lini ya twitter inaitwa https://twitter.com/TheMossadIL pale utapata kuangalia list ya viongozi wa hamas ambao hadi sasa wamekuwa eliminated. ni wengi mno, hao waliobaki kupigana ni wafuasi tu na viongozi wachache wamebaki, ila majority ya makamanda wao wameshakuwa eliminated. na israel inasema inatafuta kwanza viongozi na wengine wanafuata. hadi nimewaonea huruma. usije kufurahi ukidhani israel peke yake ndio anaumia hapo, upande wa pili kuna kipigo kikubwa sana kinatokea hadi hamas wenyewe hawapati muda kwenda kuzika viongozi wao. kama kuna mambwa gaza, baada ya vita hii wataishi kwa mizoga ya wanahamas kwasababu sidhani kama israel baada ya kuwauwa inawazika, inawaacha tu wanazagaa.
 
Askari aliyetoka kwenye kifaru ni mmoja tu, ila Mpalestina toka Mkuranga anavyoongeza chumvi kama hadithi njoo utam kolea [emoji847]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Kwani kifaru kinaendeshwa na askari mmoja.Si wanakuwa zaidi ya watano.Huyo ndiye aliyebahatika kutoka.
Na hivyo vifaru vya hapo pembeni ni vya nani kama si vya IDF.Hamas hawajawahi kumiliki hata kimoja
 
Ndio maana tumesema, Lazima Vita hii iendelee, Tutahakikisha sisi wanaIsrael, GAZA haikaliwi Tena na HAMAS.

Hatutasimamisha vita, Uwezo tunao, nguvu tunazo, na Hari tunayo.


Tutawapiga na hamna mtu wa kutufanya kitu, lazima GAZA tuisafishe. .

Nenda basi kawasaidie ndugu zako,
3232424768283167784.jpg.png
3232962517750950258.jpg.png
Screenshot_20231110-104110_Instagram.jpg
 
Kwanza hamkufikiria yote haya, mara oh ni taifa teule, usipoibariki Israel hutobarikiwa, aise nyie watu hamstahili kuishi huku.
You're out of your mind! Yaani unaona kama ndo umeshinda vita? Unatia huruma kabisa
 
huyu jamaa wa ajabu sana, anashangaa askari kukimbia huku akivua nguo, hajui kama akibaki na nguo atateketea kwa moto. ulitaka abaki mlemle aungue? au arudi kumwokea mwenzake ambaye anajua hawezi kufanikiwa kumwokoa, na yeye si atakufa na wakati huohuo adui yupo kwenye range ampige risasi? sema israel nao hao vijana wameenda huko ni wadogo, wapo kwenye 20s, wapo vitani wanafikiria magirlfriend wao wamewaacha uraiani pengine. jeshi lao wengi ni vijana wadogo jambo ambalo pia ni zuri kwasababu ni hazina kwa taifa. na wengine wameitwa tu toka mataifa mbalimbali kwasababu wayahudi wote duniani lazima huwa wana kipindi wanaenda kutumikia jeshini israel na kurudi nchini kwao, wengine hawapo vizuri ndio maana tunasema kama isingekuwa zana za kisasa, israel wangesumbuka zaidi ya hapo kwa hamas.
 
Du! Huyo mwanajeshi ni kiboko. Hivi ule mlipuko wa kwanza haukuwa na joto kali kweli? Mana jamaa katoka mbio, kama vile hajapata chochote ndani ya kifaru.

Halafu hivi kitengo cha kifaru si ndio huwa hatari sana mana unakuwa umo ndani, watu wakikuotea wanapanda juu wanarusha bomu humo humo.
Ahahaha
Hatari
 
Back
Top Bottom