Kwa watu kama wewe na wale wanaoiponda polisi, hebu fikiria serkali itangaze kuwa kwa muda wa wiki moja polisi wa aiana ypoyote hawatakuwepo. Vituo vyote vya polisi vimefungwa. Raia watakaa bila huduma ya ya polisi wiki nzima. Fikiria wewe na familia yako, ndugu zako, jirani zako, na kwa ujumla wananchi wote watakuwa katika hali gani. Ni rahisi kuwatukana polisi hata pamoja na mapungufu yao wakikosa kuwepo wote tutajuta. Na kama unamshabikia mwanajeshi au wanajeshi hebu jiweke chini ya utawala wa jeshi angalao kwa wiki. Mimi nimeishi kwenye nchi zizokuwa zinatawaliwa na jeshi na ninajuwa naqongelea nini! Usiombe uwe chini ya jeshi, utaona polisi chekechea!