Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Wewe nani kakuambia.Unakumbuka waongoza ndege waligoma JWTZ wakaenda kamata usukani airport? Unakumbuka madaktari waligoma Muhimbili wakaenda kamata usukani? Unakumbuka meli ya Ukerewe ilipinduka JWTZ wakaenda igeuza? Vita vya Kagera Iddi Amini alivunja daraja likajengwa lingine kwa muda mfupi? Wewe ulikuwa hujazaliwa
Jeshini ni wasomi mno kuna degree za phD na maproffesor wapo wa kumwaga yupo mmoja anaitwa Brigedier general dr??? Namuhifadhi jina lake.
Hakuna fani uraiani jeshini haipo
Wewe unaonekana ndio mbumbumbu na hujapitia jeshi
Yah upo sahihi kabisa kuna watu wana elimu nzuri na kuna vyuo huwa wanafundisha kwa muda tu.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482212
Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz muwanunulie bia
Constebo wa polisi awapo kazini anaweza kumhoji mtu yeyote hata kama ana cheo kikubwa kuliko yeye, isipokuwa awe na heshima katika kufanya hivyo. Tunaposema hakuna aliye juu ya sheria hiyo ndiyo maana yake halisi. Hata mkuu wa majeshi anaweza kuhojiwa na polisi wa cheo cha chini kama yuko katika kutimiza kazi yake. Nafikiri wanaodhani kuwa mwanajeshi au mwenye cheo cha juu hahojiwi ni wale ambao hawajapitia kazi ya uaskari kama vile JKT.
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Awaachie nafasi na wengine wakalewe
 
Hivi kati ya JWTZ na Polisi kina nani wanafanya kazi kubwa hapa nchini?
Nchi hii kila mtu au mfanya kazi ana umuhimu wake. Polisi ni muhimu, mwanajeshi ni muhimu, watumishi wa afya ni muhimu, magereza ni muhimu, wasafishaji wa barabara, choo, majumba n.k. ni muhimuwalimu ni muhimu. Kwa kifupi kazi zote za taaluma ni zisizo za taaluma ni muhimu kwa sababu tunategemeana ili kila mfanya kazi kutimiza wajibu wake.
 
hujui walianzia wapi hii video ni fupi! kwanza TRAFIKI anakosa adabu kibishana na mtu aliyemzidi cheo mbele ya RAIA
Kwenye makosa cheo weka pembeni. Ndiyo nimyi mnadhania dereva wa gari la mkubwa au mkubwa mwenyewe hatakiwi kupewa tiketi au kusimamishwa akikosea. Sijui katika kutenda hayo makosa ataua utamuachia kwa sababu ana cheo cha juu. Kuwa mwanajeshi au mkubwa siyo kinga yas kutpofuata sheria, ama sivyo TZ itakuwa nchi ya "man eat man".
 
Leo asbh nilikuwa natoka Mazoezi, nimefika mahala traffic amesimamisha Daladala lkn hapo hapo akawa ameenda upande mwingine kusimamisha Lorry, yule Konda wa Daladala akawa anamfuata upande wa Lorry akamfikia akamshikisha buku 2 wakaachana Konda akarudi kwenye gar Daladala ikasepa..... hebu hapo jiulize alisimamisha Daladala ya nn maana hata kukagua hajakagua usipokuwa kupewa buku mbili na daladala kuondoka.... amepoteza muda wa watu wangapi hapo, amesumbua watu wangapi hapo....Police kwa ujumla wake inahitaji reform wao wametanguliza Rushwa mbele kuliko kazi yao ya msingi ya kusimamia usalama wa raia/usalama wa barabarani, sometime wanahitaji such rude treatment!!
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Yaani umvumilie kwa sababu akifukuzwa atakuwa mwizi. Utavumilia wangapi? Kama kuna kazi inataka nidhamu ya hali ya juu kuliko zote jeshi ni mojawapo. Ndiyo maana mwajajeshi anaambiwa tii amri kwanza maswali baadaye. Kumbuka kosa dogo la nidhamu linaweza kuletelezakufagiwa kikosi kizima au hata kuleteleza nchi ikatekwa kwa sababu ya ya mjinga mmoja asiye na nidhamu.
 
Back
Top Bottom