Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Mamburula wote jeshini ndio wanaishia hivyo na wengine wameshastaafu,jeshi la sasa hivi ni la wasomi..sasa hivi huwezi kuingia JWTZ na division 4 kule wanaingia watu wenye taaluma zao.
°acha uongo division iv ndio wengi kwenye majeshi yote police, prison,jwtz, Uhamiaji nk
 
Wewe Akili zero JWTZ ndio linaongoza kwa wasomi sasa hivi JWTZ hauingii na division 4, police division zero na darasa la saba zipo za kutosha na bado wanaendelea kuchukua vihiyo
°huu ni uongo, tafuta matangazo ya kazi za police kama utakuta wanaajiri darasa la 7 au wenye division zero form iv
 
°staff sajenti mtu mdogo Sana at least angekuwa COMMISSIONED OFFICER
Commissioned officer Wana strict code of conduct. Wakipanda public transport hawavai uniform. Ndio maana huwezi kuona uniformed officer kwenye daladala au mwendokasi au kumkuta anakula kwa mama ntilie, au akiwa maeneo ya ma dada utamu.
 
°sasa huyo satff sajenti ana influence gani?
 
Mkuu mbon una roho mbaya namn hyo , kufutw kaz kwa MTU sio jambo la kushabikia kbs kaz ni maish anao wategemez na kutokana na ktu alichofany hakin uzto huo wakumpelekea kufutw kaz labda kam alishatend makosa mengn ndan ya kaz

Apew kalipio tuu na ajielez bas
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482744
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz muwanunulie bia
Kuna mazngr yake yakutumia hiyo lugh
 
Mkuu mbon una roho mbaya namn hyo , kufutw kaz kwa MTU sio jambo la kushabikia kbs kaz ni maish anao wategemez na kutokana na ktu alichofany hakin uzto huo wakumpelekea kufutw kaz labda kam alishatend makosa mengn ndan ya kaz

Apew kalipio tuu na ajielez bas
°yeah sio jambo jema kufukuzwa kazi.
° Huyo na elimu yake ya form iv sijui atakuwa mgeni wa nani au ataenda Lumumba buku7 🤣
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz muwanunulie bia
Hii clip ni ndefu mkuu wamekata kipande tu huyo traffic ndiyo alianza kuonesha dharau Kwa kuchelewesha gari bila sababu za msingi abiria walipo taka ufafanuzi akiwemo mjeda ambaye alikuwa anaomba wamalizane na dereva ili wawahi ndiyo traffic akawa mkali na kumpiga mkwala mjeda kuwa asimfundishe kazi na ikawa mwanzo wa kutoleana lugha za kibabe ila traffic ndiyo mkorofi
 
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482744
Punguza mihemuko ya kijinga Hii clip ni ndefu mkuu wamekata kipande tu huyo traffic ndiyo alianza kuonesha dharau Kwa kuchelewesha gari bila sababu za msingi abiria walipo taka ufafanuzi akiwemo mjeda ambaye alikuwa anaomba wamalizane na dereva ili wawahi ndiyo traffic akawa mkali na kumpiga mkwala mjeda kuwa asimfundishe kazi na ikawa mwanzo wa kutoleana lugha za kibabe ila traffic ndiyo mkorofi
 
Polisi alikuwa anamuonya dereva lkn yule JWTZ kwa kimbelembele chake tu akaingilia
Mzee sio kwel traffic aliweka gari Kwa muda mrefu bila sababu za msingi kuandika faini alikuwa hatak ndiyo chanzo Cha mzozo
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Mamba ni hatari akiwa kwenye maji.
Huyo mjeshi akifukuzwa kazi anakua ni mtu wa kawaida sana.
Akijaribu kujihusisha na uhalifu asubiri kutafutiwa mochwari.

Mfumo wa kiulinzi wa Nchi hii ni tofauti sana na unavyofikiri mkuu.

Askari wa usalama Barabarani wanafanya kazi kubwa sana . Tatizo ni SHERIA sio askari wa Tarafiki. SHERIA na maelekezo yanawafanya TRAFIKI wapewe lawama nyingi zisizowahusu.

SHERIA inamtaka akamate kosa na kuandika faini au kumpeleka mkosaji mahakamani na haingii kazini na SHERIA au kanuni yake Bali imetungwa na Bunge.
Bunge linapaswa kubadili SHERIA za usalama Barabarani ili askari wasikamate wanaovunja kanuni au waseme wasimamishe magari na kuwasalimia TU madereva Kisha wawatakie safari njema hapo ukiona rushwa au kukamata mtu basi tutashangaa sana.

SHERIA za Latra ni Kali sana lakini hawalalamikiwi Kwa sababu ya kimtizamo TU na sio uhalisia kwa sababu kiuhalisia SHERIA za Latra ni za uonevu kuliko SHERIA zinazosimamiwa na TRAFIKI. Mfano Kondakta asipova sare faini ni 250000 lakini mtu akiovertake kwenye Kona na akapigwa mpaka picha Kisha akakamatwa na Polisi faini yake ni Elfu 30. Na akitoa rushwa haizidi Elfu 10. Rushwa ya Latra haipungui laki Moja.
Perception ya wanasiasa na malengo yao mara nyingi yamesababisha Polisi kazi yao kubwa wanayofanya isitambuliwa na KUONEKANA KUWA hawana maana Wala umuhimu wowote kwenye jamii.

Lakini ukweli ni kuwa Polisi wanafanya kazi kubwa sana kwenye nchi yenye amani na hata amani ikitaweka wahanga wa kubwa huwa ni Polisi Kwa kuwa wahalisi wanapata urahisi sana wa kuwavamia Polisi kulingana na mpangilio wa kazi yao. Huwezi ukawakuta Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wawli tu kwenye Kazi huku wakiwa na Bunduki za kivita zinazotafutwa na Wahalifu lakini ni kawaida sana Kwa Polisi Wawili kuhatarisha maisha yao wakiwa na silaha Tena hata Kwa masaa 24. Ndio maana unakutwa wanavamiwa na hata kuuawa Kwa ajili ya kulinda Mali za watu au fedha benki n.k.

Kama Mwanajeshi ambaye naye ni mlinzi wa SHERIA za nchi na katiba ya nchi anatumia cheo chake kumtukana askari akiwa kwenye majukumu yake basi nchi hii imeanza kufitinika.?
Askari wa Jeshi akikosa nidhami ni hatari sana Kwa usalama wa nchi.
Askari wa Jeshi akianza wazi wazi kukiuka SHERIA Kwa kiburi ni hatari sana Kwa usalama wa nchi.
Rais na viongozi wote wa nchi wanaongozwa na Polisi kwenye misafari yao na hata majumbani mwao. Sasa kama Kuna Askari wa Jeshi asiyewaheshimu walinzi wenzake katika nchi kunasiku atavamia nyumba ya Waziri Mkuu au hata Ikulu au Akavamia msafara na kufanya uhalifu mkubwa.

Huyo mwanajeshi ashitakiwe katika mahakama ya Kijeshi na afungwe gerezani miezi SITA akitoka aendelee na kazi. Akirudia afukuzwe kazi. Watanzania wengi wapo mitaani hawana ajira na wanautii na uzalendo mkubwa Kwa nchi yao.

Achululiwe hatua Kali za kinidhamu.
 
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482744
Tatz askari wa JWTZ wanajisahau kwamba wao pia n watumish wa umma

Wapo chin ya sheria ya utumishi wa Umma
 
Police wana lugha mbaya sana, waonevu sana na sio waelewa. wengi wanawaza rushwa tu muda wote na hata wakati mwingine kwa watu wanaofanya nao kazi huwa hawawaheshimu. kifupi polisi huwa sio wa kuwaamini, wote hata kama ni mtoto wako usimwamini,ni mtu anawea kukuchinjia baharini anytime. ndio maana wengi huwa hawaumii moyo kama polisi akitukanwa namna hii. wanaona poa tu. ni kutokana na matendo yao. ni tofauti kabisa na polisi wa mamtoni.
Mkuu Mambo mengine inabidi tupime wenyewe na sio kuwaamini sana wanasiasa . Jeshi hua halijadiliwi sana Bungeni ili wananchi wasijue madhaifu yao na kulidharau Jeshi. Lakini Kuna madhaifu kama zilivyo idara nyingine .Wanasiasa wanawasifia wanajeshi Kwa sababu Moja TU Jeshi ndilo serikali mbadala saa zote na wanaweza kupindua Nchi dakika Moja lakini kiuhalisia Wapo baadhi ya wanajeshi wa hovyo kama walivyo baadhi ya polisi wa hovyo, baadhi ya manesi wa hovyo,baadhi ya Madaktari wa hovyo, baadhi ya walimu wa hovyo ,baadhi ya mawaziri wa hovyo, baadhi ya wabunge wa hovyo , baadhi ya malecturer wa hovyo, maEnginia wa hovyo ,baadhi ya wahasibu wa hovyo ,baadhi ya Mashekhe wa hovyo ,baadhi ya manabii wa hovyo,baadhi ya wachungaji wa hovyo !
Haiwezekani Polisi wote wakawa wa hovyo . Ingekua hivyo hatunge weza kumwagilia moyo mtaani mpaka kunakucha. Wangekomba pesa pale benki na mishahara yao midogo. Wanalinda pesa za matajiri wakati wao ni maskini , wanalinda mawaziri wasiojali maslahi yao lakini wanawatukana mpaka watoto wao.
Wanaowalinda majaji ,mahakimu heshima yao sio Elimu zao Bali ni uwepo wa Polisi . Heshima ya mtu yeyote ni Kwa sababu Kuna Polisi . Ukimskiliza Mbowe akiwatukana Polisi unaweza ukadhani kule Moshi Kuna majambazi watupu na Polisi wameshindwa kulinda Mali zao. Mali za Mbowe hazikuharibiwa na majambazi Bali wanasiasa. Polisi wanafanya kazi yao ya kulinda Mali za Mbowe lakini wanaoziharibu ni wanasiasa wenzake ambao wanatukana Polisi kuwa ni hawafanyi kazi.

Kila waafrika Wana asili ya uhalifu bila Polisi kila mtu ni mhalifu .
 
Hii clip ni ndefu mkuu wamekata kipande tu huyo traffic ndiyo alianza kuonesha dharau Kwa kuchelewesha gari bila sababu za msingi abiria walipo taka ufafanuzi akiwemo mjeda ambaye alikuwa anaomba wamalizane na dereva ili wawahi ndiyo traffic akawa mkali na kumpiga mkwala mjeda kuwa asimfundishe kazi na ikawa mwanzo wa kutoleana lugha za kibabe ila traffic ndiyo mkorofi
Traffic yupo kazn ulijuaje hakun sababu za msing kwa gar kuendelea kusimamishwa kumbuk Trafik anaongea na staff wa gar tuu/derev na wasaidz huyo mjed angepasw kuwaz tuu kutokn na utofaut wake akiwek neno linawez kuw na ukakas
 
Back
Top Bottom