No no no mkuu, ndio maana nchi hii bado sana na inachangiwa na generation kama hii ya kwako
Wewe ndugu yangu kubali kufanya utafiti na kujifunza mambo kiuhalisia achana na wanasiasa wanaoponda na kutukana Polisi Kwa sababu ya kuzuiwa mikutano ya Hadhara.
Hivi usomi wa Wakurugenzi ulisaidia Nini kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 ? Usomi wa majaji wa Tume ya uchaguzi ulisaidia Nini wakati wa Uchaguzi au uchaguzi wa mwaka 2020? Yaani Mkurugenzi na madigrii yake anakimbia ofisi ili asitoe Formu kisa analinda Ulaji wake. Kama Degree holder ni Chawa kiasi hicho inakuaje Kwa Darasa la Saba anayelinda ajira yake Kwa maelekezo ya wanasiasa?
Hivi umewahi kutafiti na KUELEWA kuwa Mwaka 2020 ndio mwaka uliokuwa na MaOCD ,Wakuu wa upelelezi, Wakuu wa Vituo na maafisa wenye nyota mpaka IGP wenye Digrii , masters mpaka PhD wengi kuliko mwaka wowote wa Uchaguzi hapa Tanzania ?? Lakini Cha ajabu wengi walijitikeza mpaka kuchukua fomu kupitia CCM na wakashirikiana na Wakurugenzi na maDC kama akina Sabaya kuvuruga uchaguzi Purposely. NI WASOMI WALIOFANYA UPUUZI ULE KWA MALENGO BINAFSI KAMA ILIVYO HULKA YA WASOMI WA KIAFRIKA ?
Jiulize ni Kwa Nini kila palipokua na mikutano au mpango wa kuzuia maandamano palikua na Mapolisi wasomi wenye vyeo vya juu na walikua wanahakikisha wazi kuwa wapinzani hawashindi ?
Wale wa Darasa la Saba wengi Wanavipaji halisi vya Kijeshi na wanauwezo mkubwa wa kuzuia Vurugu bila kuleta madhara Kwa sababu wengi wamejifunza wakiwa wadogo tofauti na wale wanye madigrii na vyeo wanaotafuta umaarufu na uteuzi.
Wale askari wa chini wengi wamehudhuria kozi nyingi za mapigano na ujasiri wa Hali ya juu ndani ya upolisi wao na sio digrii za Udom au SUA ambazo hazihitajiki kwenye mapigano ? Unaweza ukakutana na dogo wa Form four amefuzu kozi za Kung Fu na karate na anauwezo wa kumnyang'anya jambazi Silaha Kwa mbinu za kivita na amefuzu mafunzo yote ya Kipaolisi CCP halafu unamkashifu na kumtukana etu Kwa sababu Hana Digrii ya ushirika Moshi !! Ni Kushindwa kuheshimu taaluma za watu Kwa sababu ya ukosefu wa ajira na chuki TU ya kudhani kuwa kazi ya mtu Mwingine ni rahisi alimradi TU mtu ana digrii kumbe sio.
Ni msomi Gani anakubali kuwa askari wa chini ambaye Hana Sikukuu ,usiku ,Wala mchana Wala mvua Wala jua huku akiwa anakoromewa na WA juu yake au kuwa getini Kwa mkuu wa Wilaya halafu anayepita getini mlimaliza naye Digrii na ana Pass digee na wewe una First Class Digree na huna cheo mwaka wa 20 kazini ?
Tuache maneno ya kisasa mkuu . Tufanye utafiti na tuzungumze mambo Kwa uhalisia ili tuweze kuliponya Taifa Kwa haki ?
Ni Chuo Gani kinafundisha Shabaha na mapigano ya kujihami ya Judo au Kareti nje ya vyuo vya Kijeshi?
Sasa ukimuona mtu hamjasoma naye UDSM basi unaona hajui kazi yake ambayo hapo chuoni hakuna mafunzo hayo.
Mtu anaenda kupita kwenye Shimo la moto na risasi juu ataenda kusomea SUA badala ya CCP ?
Hivi watanzania mnashindwa kuamini Majeshi yenu?
Miaka ya 1995 na kuendelea mpaka 2005 askari wa Rwanda walikua wanapata mafunzo CCP na Sio Uingereza Wala China . Leo Rwanda Ina Polisi smart sana barani Afrika. Nyie mnabaki kusema Polisi wa Tanzania ni wajinga, hawajasoma n.k .
Kumbuka Jeshi la Polisi ni Jeshi kamili lenye mafunzo asilimia kubwa ya Kijeshi ndio maana tunapiga kelele ipatikane katiba mpya na SHERIA mpya za usalama wa nchi Jeshi libaki Moja TU ambalo ni Jeshi la Ulinzi JWTZ . Polisi iwe ni Idara ya Huduma ya Usalama wa Raia" Polisi Service Department ". Ili wakishapata mafunzo ya Kijeshi ya awali basi kozi nyingine ziwe ni za Elimu na Mbinu za kisayansi zaidi na sio kugaragara vichakani . Mapigano na vita ibaki kwenye Jeshi Moja TU.Tatizo Vyuo vya kipaolisi vyote ni vya Kijeshi muda wote kulingana na Taratibu za majukumu yalivyo.
Ukiondoa Amri kwenye Jeshi kazi za hatari haziwezi kufanyika. Tanzania ni Tofauti na Marekani au kwingine Ikitokea Vita Majeshi yote Wanakwenda ikiwemo Polisi mpaka mgambo na WA mwanzo kabisa kujaribu kukabiliana na uvamizi wanakua ni Polisi mpaka watakapobaini kuwa uwezo wa adui unahitaji zana kubwa za kivita ndipo Jeshi la Wananchi waingia Kwa nguvu kubwa.
Sasa utawezaje kuajiri Wenye Digrii za mitaani watupu ?
Digrii Chache zinahitajika kama SHERIA ,IT , Engineering, Uhasibu Kwa ajili ya utaalam wa kiofisi lakini sio mapigano ya nje.
Tatizo watu wanapoona wazungu wanaongea kingereza basi wanaamini kuwa ni wasomi kumbe ni wapuuzi TU mashoga wamejazana kwenye Majeshi yao na ndio maana walitaka wapandikize mashoga kwenye Jeshi letu wakashtukizwa.