PreGE2025 Askari waliofunika sura zao wanadaiwa kumfuatilia John Heche huko Mwanza, yadaiwa wanataka kumkamata

PreGE2025 Askari waliofunika sura zao wanadaiwa kumfuatilia John Heche huko Mwanza, yadaiwa wanataka kumkamata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askari waliovaa mask si kawaida, ni hivi karibuni wameanza kufanya hivyo..
Nahisi wanachukua tahadhari kwa kile kinachoendelea nchini..
 
chadema si wana kesi kisutu wameshitakiwa na wapemba mbona heche hayuko kisutu kuhamasisha wanachama kuja kusikiliza kesi.
 
Heche siyo wa kumuwinda ni wa kumuita polisi kama wana shida naye atajipeleka mwenyewe
Sijui nn kinawashinda, nadhan wanata kutumia zile njia zao haram baadae waseme hawajui yuko wapi
 
Bora hata mmewapiga picha za ukumbusho. Maana hao jamaa kwa kukana tu kuhusika na hayo matukio yao ya hovyo, hawajambo. Hao bila ya ushahidi watakuambia hawahusiki.
Askari walioficha sura zao inadaiwa wanamfulia John Heche mchana huu huko MWANZA. Askari hawa wanatumia gari lenye USAJILI PT 4833.

Kwanini wavae hivi wakiwa kwenye gari za POLISI? wanajificha nini?

rais wa chadema labda wa TFF siyo tanzania hii kazchezeni na dadazebnu huko ccm mbelekwambele

Kwa hatua hii mbaya kabisa ya kisiasa ilipofikia, hakuna namna nyingine yoyote ile zaidi ya Watu wa CHADEMA kuishi maisha yao binafsi ya kila siku Kama vile ambavyo Watu wa ANC walivyokuwa wakiishi chini ya mwavuli wa uMkhonto weSizwe enzi zile za Utawala wa Ubaguzi wa Rangi wa Makaburu kule Afrika Kusini. Hakuna njia nyingine yoyote ile mbadala kwa watu wa Chadema ya kuweza kukwepa kuishi maisha ya namna hiyo.

Ni dhahiri shahiri kabisa kwamba, Watawala kwa sasa hivi wanaichukulia CHADEMA kama Kundi la Kigaidi na Wala siyo Chama Cha Siasa tena kilicho halali kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Kwa upande mwingine, CHADEMA nao kwa upande wao sasa wanayo HAKI na Uhalali wote kabisa wa kisheria, na wa kimaadili wa kuweza kuchukua hatua zote kabisa za tahadhari katika kujihami na kujitetea kutokana na mashambulizi yoyote yale ambayo yanayoelekezwa kwao.
Kazi kwao, chaguo ni lao!
 
Kila siku huwa nasema ..kama Mungu amekupa uhai na afya njema na una watoto hakikisha wanapata elimu vizuri!
Maisha ya kuvalishwa matambala usoni namna hii ili usitambulike ukimdhuru mtu ambae hata humjui na hata hujui kosa lake ni laana kwenye ukoo.
Kama mzazi inabidi uape kabisa, none of your son and daughters watafanya hizi mambo. Ni beyond laana

Bora taasis zingine lakin sio hii
 
Mzenji kanogewa na damu za Watanganyika
Damu gani tena si mlisema hakuna damu chini ya samia anaupiga mwingi niliwaonyeni kuhusu hekima ya kukisoma kifo cha jpm kutabiri mambo ya jayo ...niliwaambia kile kifo kama kina mikono ya watu basi hali ya nchi itakuwa mbaya zaidi walio husika awawezi kamwe kufanya makosa juu ya nafsi zao ....maana wanajua madhara yake ...
 
Kesho Watasema hawawajui, na hamtaenda kuumiza Familia zao coz hamtawatambui.
 
Kazi ya laana huwezi kuifanya ukiwa comfortable yaani sura ionekane vizuri never😂, hovyo kabisa. Kazi za kutumwa na kujibu SAWA Mkuu, Ndio Boss...hovyo sana
 
MM NIPO HAPA, MBONA MNAZUA TAHARUKI MITANDAONI HIVO?
KWANI NI MARA YA KWANZA POLISI KUVAA HIVO?
DAAH KWA KWELI MBINU ZIKIISHA HUWA NI USANII UNABAKI
Kwanini polisi wavae hivyo .
Kwa nini wafiche sura zao hivyo nitajie sababu moja tu.
 
Sasa ni kafara?

Soon itawageukia wao, kama Mungu aishivyo, CCM watanyongana wao kwa wao kuanzia sasa hadi July hapo

Hapatakalika, Bwana wa Majeshi atayageuza mabaya waliyoyakusudia kwa wapinzani ambao ni watanzania na viumbe wake kuwa ubaya kwao

Trust me!

Wengine chekeni na kukebehi kama mlivyozowea
 
Masikini wanatumia Kama toilet paper na mafisadi maisha yao magumu Sana na mishahara ya laki 5

Ugumu wa maisha bwana unakuta hapo akitoka anaenda ofisini kusaini elfu 50 Kama posho bila kujua anayemlipa hiyo pesa anaweka mfumo hata kitukuu chake kitakufa hakijagusa hata cheo Cha ubunge tu achilia uwaziri na urais wa Tanzania

Nchi hii imejaa watu wengi wajinga Sana !!
Ni shida sana. Maskini anatumika kama mbwa kumkamata mtu ambaye (Heche) anapambana kubadili mifumo ya inayomkandamiza hata mtoto wa huyo askari kupata maisha bora.
 
Kama sijakosea

Mahakama ilishatoa agizo polisi wazivae mask
imekuwaje wanakaidi maagizo ya mahakama, wahusika watoe maelezo na ikiwezekana wawajibishwe kisheria
 
Askari walioficha sura zao inadaiwa wanamfuatilia John Heche mchana huu huko MWANZA. Askari hawa wanatumia gari lenye USAJILI PT 4833.

Kwanini wavae hivi wakiwa kwenye gari za POLISI? wanajificha nini?

Form failures katika ubora wao,
Yaani, hawa, kenge huwa, wanajiona kama Navy Seal, kumbe ni mazwazwa, tu, yanajiona yamepatia, maisha, yqkitoka hapo, yanakwea, daladala, na, kuwenda kuishi, uswazi, kenge kqbisa
 
Back
Top Bottom