PreGE2025 Askari waliofunika sura zao wanadaiwa kumfuatilia John Heche huko Mwanza, yadaiwa wanataka kumkamata

PreGE2025 Askari waliofunika sura zao wanadaiwa kumfuatilia John Heche huko Mwanza, yadaiwa wanataka kumkamata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askari walioficha sura zao inadaiwa wanamfuatilia John Heche mchana huu huko MWANZA. Askari hawa wanatumia gari lenye USAJILI PT 4833.

Kwanini wavae hivi wakiwa kwenye gari za POLISI? wanajificha nini?

Mchana wa jua kali yamevaa kama magaidi. Tukisema hiki ni kikundi cha uhalifu dhidi ya binadamu wakosoaji tueleweke.
 
Kila siku huwa nasema ..kama Mungu amekupa uhai na afya njema na una watoto hakikisha wanapata elimu vizuri!
Maisha ya kuvalishwa matambala usoni namna hii ili usitambulike ukimdhuru mtu ambae hata humjui na hata hujui kosa lake ni laana kwenye ukoo.
Yani hapo ni kulinda familia za akina Abdul waendelee kula kunywa kusaza kwa kodi za wamanchi
 
Kama Tanzania bado hakuna amri ya mahakama ya kuzuia policcm kuvaa mask inafaa wadau wafungue kesi kwa dharura ili kupata hiyo court order.

Polisi mwenye nia njema hana sababu ya kuficha sura.

Ukute wanataka wakitekeleza tukio la uhalifu wasijulikane kama yule afande Shabani wa Mbeya
Ndio maana nikasema wanaoteka watu ni polisi maana kama wako katika utekelezaji wa majukumu yao kukamata wahalifu kwanini wazibe nyuso zao?
 
Mimi siipendi CCM ila hapo Polisi mnawaonea maana duniani kote taasisi za majeshi wote huvaa hivyo kama ka utamaduni sasa yani kwetu hapa hata Askari wa Zimamoto utamkuta kapiga hiyo ko hiyo siyo ishu
 
Askari walioficha sura zao inadaiwa wanamfuatilia John Heche mchana huu huko MWANZA. Askari hawa wanatumia gari lenye USAJILI PT 4833.

Kwanini wavae hivi wakiwa kwenye gari za POLISI? wanajificha nini?

Kuna wakati mwingine tumieni akili kufikiria, acheni propaganda za kijinga. Hivi heche ni wa kuwinda au ni wa kukamata kama kuku? Acheni ushamba na kutafuta huruma za watu. Ni mara ngapi maaskari huvalia mask kama hizi? rubbish
 
Mpumbavu wewe..

Hebu tuambie vizuri. Ni wakati gani na katika mazingira gani askari anatakiwa kuvaa masks badala ya helmet za kipolisi...?

Kwanini wavae masks kuficha sura zao?

Jibu ni rahisi tu. Ni ili wafanye matendo yaliyo kinyume cha sheria za utendaji wa polisi (PGOs), matendo ya kihalifu, ugaidi na ujambazi kisha isiwe rahisi kuwatambua kwa sura zao itakapohitajika na baadaye viongozi wao waseme, "Jeshi la polisi halihusiki na matukio hayo...!!"

Ukweli ni kuwa, hawa sio askari wa Jeshi la polisi halisi.....!!

Hawa ni vijana wa UVCCM waliovikwa mavazi/sare za polisi kufanya vurugu kwenye mikutano ya CHADEMA...

Hawa wana tofauti gani na wale waliofanya vurugu tarehe 24/4/2025 pale mahakamani Kisutu - DSM kukamata watu hovyo, kuwapiga, kuwatesa, kuwavunja miguu na mikono kisha kwenda kuwatupa porini...

Polisi gani wa kawaida aliyefundishwa kutenda kazi yake vyema kwa kuzingatia sheria anaweza kufanya ujinga na uhuni ule wa tarehe 24/4/2025...?

Si RPC wa kanda maalumu ya DSM Afande Jumanne Muliro aliwakataa kusema kuwa hao hawakuwa polisi wake? Unakumbuka hilo..?

Au mmeamua kujitoa akili na ufahamu na kuwa muwe wajinga na wapumbavu tu...?

Tuambieni, hawa ni kina nani? Polisi gani kama sio wale "wasiojulikana?"
 
nani ameandaa hiyo art work?

na ni nani kaandaa script gentleman ya hii drama? mbona mnarudia makosa yaleyale kila siku gentleman? :pulpTRAVOLTA:

Ila Maza anautaka urais kwa gharama yoyote!

Au nasema uongo?
 
Ila Maza anautaka urais kwa gharama yoyote!

Au nasema uongo?
urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba ya nchi na kura za wananchi waTanzania.

Kinyume na hapo ni ushirikina gentleman 🐒
 
urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba ya nchi na kura za wananchi waTanzania.

Kinyume na hapo ni ushirikina gentleman 🐒

Katiba hii?

GqkkKYjWgAERs7G.jpeg
 
Hao ni askari wahuni wenye nia mbaya.Wanakamata vipi raia mwema wakiwa wanefunika sura?!!!!
 
Wewe jamaa unanivunja mbavu '!
Hata wewe ndugu yangu post zako zinaleta raha ndio maana na mimi naamuaga kukuchekesha Ki-Mwakaleli Mission Leteba huko Rungwe kuliko jaliwa hali ya hewa nzuri na wasomi sana.
Huwa nakujibu kwa uangalifu sana maana nakuwa najua na chat na mtu wa level gani
 
Back
Top Bottom