Askofu Bagonza amnanga mkulu kimafumbo, soma kwa kifupi

Askofu Bagonza amnanga mkulu kimafumbo, soma kwa kifupi

Napata mashaka na uelewa wako
Asilimia 90 ya vitu alivyoviorodhesha mimi sina katika hivyo mimi nina Akili na Imani tu.
Barakoa sivai ndani sijifungii na Corona sipati hii homa imekuzwa sana kuliko uhalisia wa madhara yake.
Corona ni homa ya kawaida ambayo naamini asilimia kubwa ya watanzania wamewahi kuugua kabla lakini walikuwa hawajijui lakini baada ya kuwapata wazungu na kuwaathiri sana ndio shida ilipoanzia.
Mtumishi fanya kazi ya Mungu achana na siasa Watanzania tuchape kazi.
HONGERA JPM NAIPENDA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bagonza ni Mtumishi Wa Mwilini tu ndio maana anahangaika Mwilini.
Watumishi walio katika roho na wanaomjua Mungu walishapata maono ya maombi katika kipindi hiki, na kwa kuwa Mungu hajawahi kuwa mdogo Corona haiwezi kuwa kubwa kuliko Mungu, kama yeye ana Imani haba awaachie wenye Iimani wamtafute Mungu.
Katika Mungu kuishi ni Kristo na kufa ni Faida, Yeye anaogopa nini? Mpaka afunge Kanisa?
Hana Mungu? Hana Mungu? Hana Mungu?
Mungu ni utatu mtakatifu Baba,Mwana na Roho mtakatifu.
Mtafuteni Mungu kwanza na sio PhD mengine mtazidishiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nawajua maaskofu wenye phd na wale wanaojiita wasomi kiimani ni sifuri tena hapo utakuta amejaa mahirizi lukuki!

Sasa jiulize anafungua tena makanisa kwani corona imeisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hujafikiri sawasawa,wewe ni kati ya wale wa ndiyo baba.Panda,ndiyo baba, shuka,ndiyo baba kaa,ndiyo baba,simama,ndiyo baba.ili tu tumbo lako lijae.Hujaelewa hata chembe ya pointi yoyote aliyoitoa Dr.Unataka tuchape kazi ipi,uliyotupa wewe,unayetulipa wewe.Wapendwa,pelekeni watoto shule wasome,waweze kupambanua mambo.
Kumbe shida yako ni kuwa huna kazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumenyimwa haki yetu ya kusali msipofungua makanisa tutayachoma moto,hahah maigizo ya kaole sanaa group bana.
Kichwa chako kimejaa mbege asubuhi yote hii!

Mpe pole Bagonza kiki yake ya kufunga makanisa imebuma kama ile ya chadema kujifungia karantini alafu wakaishia kuvurugana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa chako kimejaa mbege asubuhi yote hii!

Mpe pole Bagonza kiki yake ya kufunga makanisa imebuma kama ile ya chadema kujifungia karantini alafu wakaishia kuvurugana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah waulize wao kama kweli wanaamini Mungu yupo ni kwanini wao wana ulinzi wa kufuru?kwanini wasimuachie Mungu tu awalinde?

Kwa sababu wanajua Mungu aliwapa akili wazitumie-Bagonza the great.
 
Hahah waulize wao kama kweli wanaamini Mungu yupo ni kwanini wao wana ulinzi wa kufuru?kwanini wasimuachie Mungu tu awalinde?

Kwa sababu wanajua Mungu aliwapa akili wazitumie-Bagonza the great.
Kama hayo ndio kasema Bagonza basi nahitimisha kwa kusema, aachane na huo uaskofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hayo ndio kasema Bagonza basi nahitimisha kwa kusema, aachane na huo uaskofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah anakwambia unamuona Simba anakuja kwako kwa kasi badala ya kukimbilia juu ya mti na kumuomba Mungu ukiwa ukiwa juu ya mti wewe unasimama huku ukisali kisa eti Mungu yupo nakuhakikishia utaliwa tu hahah

Bagonza ni PH.d kweli kweli.
 
Kumuamini Mungu ndo ujitie hatarini atakuokoa?
Usimjaribu BWANA Mungu wako
Mathayo 3:9
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.
*Mathayo 19:14
Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
*Mathayo 18:20
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
*Luka 11:9
Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
* Yohana 14:11-14
Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
* Marko 11:23
Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
- Maandiko haya in sehemu tu ya maandiko yanayohubiriwa kanisani. Je! Yanatuambia tutumie akili iwe ya kuzaliwa, ya kufundishwa au ya kusomea? Je! Kuna PhD inayothibitisha uwezekano wake? Kimsingi yote yanahitaji imani, tena imani isiyoyumba. Hapo hakuna hoja ya kumjaribu BWANA Mungu wetu.
Hapa kuna suala la kumuomba BWANA Mungu wetu kwa bidii atutoe katika janga. Kama akili zetu zinatuambia tusimuombe tusimjaribu basi imani yetu ni bure na haifai.
Wamwaminio BWANA Mungu wetu waliokusanyika na kuomba kwa bidii bila woga au hofu wako sahihi kabisa na mkono wa BWANA unaonekana juu yao.
Bwana Yesu Kristo asifiwe milele yote amina.
 
Hivi

Huyu askofu ni Mtanzania? Na je,mbona kanisa lote la KKKT yeye tu ndio ana maneno ya shobo hivyo? Wakubwa wake hawamwoni? Rais Na information nyingi kuliko yeye anayelala church hivyo kuna baadhi ya mambo anaweza kufanya akiwa anaijua siri yeye tu, sio kila kitu yapasa kumpinga.

HARMONISER ni Mtanzania?
Mbona anasifia tu hata mtu aki FRAT?
Mamlaka hazioni kwamba huyu msanii kuna jambo anaficha? kila kitu kusifia hata mtu akicheua ama kupumua hewa chafu mwilini?
 
Askofu wangu katika hili kubali tu ulimkaribisha shetani
Sasa unafungua makanisa corona imeisha?
Na ungejifungia hadi lini ?
Na jiuilize kwa nini maakofu wengine hawakufunga makanisa yao?
Je wewe ndiyo una akili zaidi kuliko maaskofu wote kwenye balaza la maaskofu?
Mtu mzima ukivuliwa nguo.chutama
Katika hili kubali imani yako imekuwa haba
wewe POYOYO, kabla hujamuuliza hayo maswali BAGONZA jiulize haya maswali?
UISLAMU na UKATOLIKI/LUTHERI umekuja na Meli.
ROMA/BABA MTAKATIFU alikuwa wa Kwanza kufunga Kanisa kubwa kabisa duniani St Peters Basilica na MECCA/UISLAMU wakafuata wakafunga msikiti mkubwa kabisa duniani na kufuta HIJJA za mwaka 2020, wewe POYOYO wa Tanzania usiyejua chanzo hata ch hizo dini, unayelishwa hadithi za MARIA , na Mtume ndio una imani kuliko walio zileta?>

Acha upumbavu, Corona ipo na inaua, haichagui dini wala kabila, mwezio alijifungia CHATO miezi miwili na mwanae alipoumwa akaagiza ndege ikachukue dawa madagaska, sasa wewe endelea na U-MATAGA wako utavuna unachotaka
 
a Askofu Bagonza


AKILI na IMANI

Hivi kipi kinaanza? Kipi kinawezesha kingine? Imani ndiyo inakuongoza kuwa na akili au akili inakuongoza kuwa na imani na kuitegemea?

Wanaopuuza umuhimu wa kutumia akili, wawaulize wazazi ambao kwa bahati mbaya wana watoto au jamaa waliopungukiwa na akili, kwa kuzaliwa au kupata tatizo hilo ukubwani. Zawadi kubwa, ya pekee na ya thamani aliyotupa Mungu ni akili. Tunaitumia kutambua na kufanya maamuzi. Hata imani tunayoienzi na kumwamini muumba wetu, tunawezeshwa na akili aliyotupa muumba huyo huyo.

Ndiyo maana pamoja na kwamba Mungu yupo:

1. Tunajenga Nyumba na kulala ndani yake, hatulali nje ili Mungu atulinde.

2. Tunajenga uzio mkubwa kuzunguka Nyumba, hatuaiachi nyumba ili Mungu atulinde.

3. Tunafuga Mbwa wakali, licha ya kuwa na Uzio.

4. Tunaajiri walinzi wenye silaha, kana kwamba uzio na mbwa havitoshi.

5. Tunaweka na CCTV kamera licha ya kuwa tuna walinzi, uzio na mbwa wakali.

6. Tunanunua na bima kubwa kuonyesha kuwa wizi bado upo licha ya kuwa tuna yote hayo.

7. Usiku tunaamka mara tatu-tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.


Pamoja na yote hayo, Mungu aweza kutuchukua kutoka katikati ya ulinzi wote huo. Anatupa akili tuzitumie kujilinda, lakini anabaki na uwezo wa mwisho juu ya maisha yetu.

Hatuwezi kuacha kutumia akili eti kwa sababu yeye yupo. Na hatuwezi kutegemea akili tu eti kwa sababu akili katupa yeye. Imani na akili vyote ni mali ya Mungu, yeye katukabidhi tuvitumie.
Hatuwezi kuacha kuvaa Mask/Barakoa eti Mungu yupo, kwani huko VATICAN na MECCA dini zilipoanzia Mungu hayupo, yupo Tanzania pekee? UCHUMI vs MAISHA YA WATU! [MSISITIZO NI WANGU]


TUSIHUKUMIANE na TUSILAUMIANE.
Ukichagua ukweli utaonekana msaliti na unatumika na mabeberu

Its not over until its over...[emoji769]
 
Back
Top Bottom