Askofu Bagonza amnanga mkulu kimafumbo, soma kwa kifupi

a Askofu Bagonza

AKILI na IMANI

Hivi kipi kinaanza? Kipi kinawezesha kingine? Imani ndiyo inakuongoza kuwa na akili au akili inakuongoza kuwa na imani na kuitegemea?

Wanaopuuza umuhimu wa kutumia akili, wawaulize wazazi ambao kwa bahati mbaya wana watoto au jamaa waliopungukiwa na akili, kwa kuzaliwa au kupata tatizo hilo ukubwani. Zawadi kubwa, ya pekee na ya thamani aliyotupa Mungu ni akili. Tunaitumia kutambua na kufanya maamuzi. Hata imani tunayoienzi na kumwamini muumba wetu, tunawezeshwa na akili aliyotupa muumba huyo huyo.

Ndiyo maana pamoja na kwamba Mungu yupo:

1. Tunajenga nyumba na kulala ndani yake, hatulali nje ili Mungu atulinde.

2. Tunajenga uzio mkubwa kuzunguka nyumba, hatuaiachi nyumba ili Mungu atulinde.

3. Tunafuga mbwa wakali, licha ya kuwa na uzio.

4. Tunaajiri walinzi wenye silaha, kana kwamba uzio na mbwa havitoshi.

5. Tunaweka na CCTV kamera licha ya kuwa tuna walinzi, uzio na mbwa wakali.

6. Tunanunua na bima kubwa kuonyesha kuwa wizi bado upo licha ya kuwa tuna yote hayo.

7. Usiku tunaamka mara tatu tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.

Pamoja na yote hayo, Mungu aweza kutuchukua kutoka katikati ya ulinzi wote huo. Anatupa akili tuzitumie kujilinda, lakini anabaki na uwezo wa mwisho juu ya maisha yetu.

Hatuwezi kuacha kutumia akili eti kwa sababu yeye yupo. Na hatuwezi kutegemea akili tu eti kwa sababu akili katupa yeye. Imani na akili vyote ni mali ya Mungu, yeye katukabidhi tuvitumie.

TUSIHUKUMIANE na TUSILAUMIANE.
Askofu wangu katika hili kubali tu ulimkaribisha shetani
Sasa unafungua makanisa corona imeisha?
Na ungejifungia hadi lini ?
Na jiuilize kwa nini maakofu wengine hawakufunga makanisa yao?
Je wewe ndiyo una akili zaidi kuliko maaskofu wote kwenye balaza la maaskofu?
Mtu mzima ukivuliwa nguo.chutama
Katika hili kubali imani yako imekuwa haba
 
Achunguzwe uraia huyo mchungaji, anaweza kuwa Mkenya.
 
Hivi
a Askofu Bagonza

AKILI na IMANI

Hivi kipi kinaanza? Kipi kinawezesha kingine? Imani ndiyo inakuongoza kuwa na akili au akili inakuongoza kuwa na imani na kuitegemea?

Wanaopuuza umuhimu wa kutumia akili, wawaulize wazazi ambao kwa bahati mbaya wana watoto au jamaa waliopungukiwa na akili, kwa kuzaliwa au kupata tatizo hilo ukubwani. Zawadi kubwa, ya pekee na ya thamani aliyotupa Mungu ni akili. Tunaitumia kutambua na kufanya maamuzi. Hata imani tunayoienzi na kumwamini muumba wetu, tunawezeshwa na akili aliyotupa muumba huyo huyo.

Ndiyo maana pamoja na kwamba Mungu yupo:

1. Tunajenga nyumba na kulala ndani yake, hatulali nje ili Mungu atulinde.

2. Tunajenga uzio mkubwa kuzunguka nyumba, hatuaiachi nyumba ili Mungu atulinde.

3. Tunafuga mbwa wakali, licha ya kuwa na uzio.

4. Tunaajiri walinzi wenye silaha, kana kwamba uzio na mbwa havitoshi.

5. Tunaweka na CCTV kamera licha ya kuwa tuna walinzi, uzio na mbwa wakali.

6. Tunanunua na bima kubwa kuonyesha kuwa wizi bado upo licha ya kuwa tuna yote hayo.

7. Usiku tunaamka mara tatu tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.

Pamoja na yote hayo, Mungu aweza kutuchukua kutoka katikati ya ulinzi wote huo. Anatupa akili tuzitumie kujilinda, lakini anabaki na uwezo wa mwisho juu ya maisha yetu.

Hatuwezi kuacha kutumia akili eti kwa sababu yeye yupo. Na hatuwezi kutegemea akili tu eti kwa sababu akili katupa yeye. Imani na akili vyote ni mali ya Mungu, yeye katukabidhi tuvitumie.

TUSIHUKUMIANE na TUSILAUMIANE.
Huyu askofu ni Mtanzania? Na je,mbona kanisa lote la KKKT yeye tu ndio ana maneno ya shobo hivyo? Wakubwa wake hawamwoni? Rais Na information nyingi kuliko yeye anayelala church hivyo kuna baadhi ya mambo anaweza kufanya akiwa anaijua siri yeye tu, sio kila kitu yapasa kumpinga.
 
Asilimia 90 ya vitu alivyoviorodhesha mimi sina katika hivyo mimi nina Akili na Imani tu.
Barakoa sivai ndani sijifungii na Corona sipati hii homa imekuzwa sana kuliko uhalisia wa madhara yake.
Corona ni homa ya kawaida ambayo naamini asilimia kubwa ya watanzania wamewahi kuugua kabla lakini walikuwa hawajijui lakini baada ya kuwapata wazungu na kuwaathiri sana ndio shida ilipoanzia.
Mtumishi fanya kazi ya Mungu achana na siasa Watanzania tuchape kazi.
HONGERA JPM NAIPENDA TANZANIA
Usipo jihusisha na siasa uta tawaliwa na wajinga! Siasa ni maisha ya kila siku kupitia siasa ndipo unapangiwa Bei ya vywakula, bima , Afya nk..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia 90 ya vitu alivyoviorodhesha mimi sina katika hivyo mimi nina Akili na Imani tu.
Barakoa sivai ndani sijifungii na Corona sipati hii homa imekuzwa sana kuliko uhalisia wa madhara yake.
Corona ni homa ya kawaida ambayo naamini asilimia kubwa ya watanzania wamewahi kuugua kabla lakini walikuwa hawajijui lakini baada ya kuwapata wazungu na kuwaathiri sana ndio shida ilipoanzia.
Mtumishi fanya kazi ya Mungu achana na siasa Watanzania tuchape kazi.
HONGERA JPM NAIPENDA TANZANIA

Ni sawa kabisa kumpa hongera RAIS, Ila isiwe kigezo cha kuidharau CORONA hii covid 19 ipo tena hapa kwetu nchini ,Hata rais anasema chukua tahadhari jikinge .Tumpongeze kwa anayo ya sema .MUNGU IBARIKI NCHI YETU NA RAIS WAKE.
 
Mimi kwa mtazamo wangu IMANI uanza ndipo zinafuata AKILI

1. Imani ujenga HAKIKA/Hakikisho ambapo AKILI utumika kuchakata Kama Mashine na kutoa kitu ambacho Imani Imekijenga.

2.Kuna AKILI na MAARIFA, akili ujengwa na Binadamu lakini MAARIFA utoka kwa MUNGU.
Unaweza ukawa na AKILI lakini Mwenyezi MUNGU asikufunulie MAARIFA ya kutumia Akili zako.
2 mambo ya nyakati : Mlango 1
10 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?

Mathayo : Mlango 11
25 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.

Warumi : Mlango 10

2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikuwa umeanza vizuri lkn ulipoanza nukuu za hiyo mistari umechemka, hiyo mistari mtu mwongo na mkweli wanaweza kuitumia na wakaonekana ni wakweli juu ya wanachokusudia, abarikiwe sana Baba Askofu
 
Bagonza ni Mtumishi Wa Mwilini tu ndio maana anahangaika Mwilini.
Watumishi walio katika roho na wanaomjua Mungu walishapata maono ya maombi katika kipindi hiki, na kwa kuwa Mungu hajawahi kuwa mdogo Corona haiwezi kuwa kubwa kuliko Mungu, kama yeye ana Imani haba awaachie wenye Iimani wamtafute Mungu.
Katika Mungu kuishi ni Kristo na kufa ni Faida, Yeye anaogopa nini? Mpaka afunge Kanisa?
Hana Mungu? Hana Mungu? Hana Mungu?
Mungu ni utatu mtakatifu Baba,Mwana na Roho mtakatifu.
Mtafuteni Mungu kwanza na sio PhD mengine mtazidishiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia 90 ya vitu alivyoviorodhesha mimi sina katika hivyo mimi nina Akili na Imani tu.
Barakoa sivai ndani sijifungii na Corona sipati hii homa imekuzwa sana kuliko uhalisia wa madhara yake.
Corona ni homa ya kawaida ambayo naamini asilimia kubwa ya watanzania wamewahi kuugua kabla lakini walikuwa hawajijui lakini baada ya kuwapata wazungu na kuwaathiri sana ndio shida ilipoanzia.
Mtumishi fanya kazi ya Mungu achana na siasa Watanzania tuchape kazi.
HONGERA JPM NAIPENDA TANZANIA
Nadhani hujafikiri sawasawa,wewe ni kati ya wale wa ndiyo baba.Panda,ndiyo baba, shuka,ndiyo baba kaa,ndiyo baba,simama,ndiyo baba.ili tu tumbo lako lijae.Hujaelewa hata chembe ya pointi yoyote aliyoitoa Dr.Unataka tuchape kazi ipi,uliyotupa wewe,unayetulipa wewe.Wapendwa,pelekeni watoto shule wasome,waweze kupambanua mambo.
 
7. Usiku tunaamka mara tatu tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.

🙌 🙌
 
Back
Top Bottom