Askofu Bagonza amnanga mkulu kimafumbo, soma kwa kifupi

Askofu Bagonza amnanga mkulu kimafumbo, soma kwa kifupi

a Askofu Bagonza

AKILI na IMANI

Hivi kipi kinaanza? Kipi kinawezesha kingine? Imani ndiyo inakuongoza kuwa na akili au akili inakuongoza kuwa na imani na kuitegemea?

Wanaopuuza umuhimu wa kutumia akili, wawaulize wazazi ambao kwa bahati mbaya wana watoto au jamaa waliopungukiwa na akili, kwa kuzaliwa au kupata tatizo hilo ukubwani. Zawadi kubwa, ya pekee na ya thamani aliyotupa Mungu ni akili. Tunaitumia kutambua na kufanya maamuzi. Hata imani tunayoienzi na kumwamini muumba wetu, tunawezeshwa na akili aliyotupa muumba huyo huyo.

Ndiyo maana pamoja na kwamba Mungu yupo:

1. Tunajenga nyumba na kulala ndani yake, hatulali nje ili Mungu atulinde.

2. Tunajenga uzio mkubwa kuzunguka nyumba, hatuaiachi nyumba ili Mungu atulinde.

3. Tunafuga mbwa wakali, licha ya kuwa na uzio.

4. Tunaajiri walinzi wenye silaha, kana kwamba uzio na mbwa havitoshi.

5. Tunaweka na CCTV kamera licha ya kuwa tuna walinzi, uzio na mbwa wakali.

6. Tunanunua na bima kubwa kuonyesha kuwa wizi bado upo licha ya kuwa tuna yote hayo.

7. Usiku tunaamka mara tatu tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.

Pamoja na yote hayo, Mungu aweza kutuchukua kutoka katikati ya ulinzi wote huo. Anatupa akili tuzitumie kujilinda, lakini anabaki na uwezo wa mwisho juu ya maisha yetu.

Hatuwezi kuacha kutumia akili eti kwa sababu yeye yupo. Na hatuwezi kutegemea akili tu eti kwa sababu akili katupa yeye. Imani na akili vyote ni mali ya Mungu, yeye katukabidhi tuvitumie.

TUSIHUKUMIANE na TUSILAUMIANE.
Mimi kwa mtazamo wangu IMANI uanza ndipo zinafuata AKILI

1. Imani ujenga HAKIKA/Hakikisho ambapo AKILI utumika kuchakata Kama Mashine na kutoa kitu ambacho Imani Imekijenga.

2.Kuna AKILI na MAARIFA, akili ujengwa na Binadamu lakini MAARIFA utoka kwa MUNGU.
Unaweza ukawa na AKILI lakini Mwenyezi MUNGU asikufunulie MAARIFA ya kutumia Akili zako.
2 mambo ya nyakati : Mlango 1
10 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?

Mathayo : Mlango 11
25 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.

Warumi : Mlango 10

2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia 90 ya vitu alivyoviorodhesha mimi sina katika hivyo mimi nina Akili na Imani tu.
Barakoa sivai ndani sijifungii na Corona sipati hii homa imekuzwa sana kuliko uhalisia wa madhara yake.
Corona ni homa ya kawaida ambayo naamini asilimia kubwa ya watanzania wamewahi kuugua kabla lakini walikuwa hawajijui lakini baada ya kuwapata wazungu na kuwaathiri sana ndio shida ilipoanzia.
Mtumishi fanya kazi ya Mungu achana na siasa Watanzania tuchape kazi.
HONGERA JPM NAIPENDA TANZANIA
"Corona ni homa ya kawaida....."
Halafu dunia nzima inahaha kwa sababu ya homa ya kawaida?
Hata hapa kwetu tulifunga shule na vyuo kwa sababu ya homa ya kawaida?
Hiyo akili tuliyopewa na Mungu tulishindwa kuitumia kujua kwamba corona ni homa ya kawaida? Au tulifuata mkumbo?

Akili yangu inakataa kabisa kuona corona kama homa ya kawaida. Sitakuhukumu wewe kuiona ni homa ya kawaida maana akili yako imeona hivyo. Nami usinihukumu kwa kuiona siyo homa ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumuamini Mungu ndo ujitie hatarini atakuokoa?
Usimjaribu BWANA Mungu wako
Kila anapita kwa kiwango chake. Sijui kama hili ni LA kumjaribu Mungu au ni la kumtukuza. Kama unajua neno lake linasemaje na unamfuata kwa uaminifu kumjaribu ndio hasa tunalotkiwa kufanya.
Neno lake linasema "
Wewe ni wa "mwilini" huwezi jua mambo ya "rohoni" kwahiyo unaposema adhihirishe nguvu za mungu its as if zipo kariakoo unaenda kuziokota tu, hujui ni suala la imani, pimbi
Asante. Wewe ndiye unaejua na wa rohoni zaidi ingawa hauko rohoni. Matusi yako yanakusuta.
 
Tanzania ya viwanda inayowekeza juhudi kuwaua watu wake ili kuokoa uchumi wake!!!sasa sijui wakifa wakabaki wachache watatawala nini!!jiwe anataka wapinzani wake wafe ili asipate upinzani mkali!!KUMBUKENI CCM IMEWEKEZA VIJIJINI AMBAPO CORONA HAIFIKI NDO MANA WAMEACHA MJINI WAFE MAANA NDIO WASUMBUFU NA WAJUAJI!!!
 
Rais ni binadamu Kama wengine ana mapungufu yake,lazima aambiwe ,bahati mbaya Jiwe ana mapungufu makubwa sana.
 
...Baba Askofu katupa jiwe gizani sijui nani limempata upande wa pili? Asante kwa kutufikirisha AKILI na IMANI
 
Ukimfuata Jiwe utalala mlango wazi. Hamna kitu kichwani. Sasa kwa nini alikimbilia mafichoni?

Tulitekeleza ushauri wa kitaalam wa kufanyia kazi nyumbani! Kufanyia kazi nyumbani siyo kuogopa korona!
 
Hawa ndio maaskofu Malaya tu na hana adabu kabisa pimbi huyu, kwanza anathubutuje, pumbavu kbsa hili dudu na limeandika ili aibike nani kama halitaki lihamie huko kwenye lockdown, Mungu hapangiwi procedures.
Punguza jazba jibu kwa HOJA kama umeshindwa kimya pia ni jibu
 
Kila anapita kwa kiwango chake. Sijui kama hili ni LA kumjaribu Mungu au ni la kumtukuza. Kama unajua neno lake linasemaje na unamfuata kwa uaminifu kumjaribu ndio hasa tunalotkiwa kufanya.
Neno lake linasema "

Asante. Wewe ndiye unaejua na wa rohoni zaidi ingawa hauko rohoni. Matusi yako yanakusuta.
kwakweli tupunguze lugha kali, Bagonza hajataja mtu
 
Kuna maaskofu wengi wana hirizi na chale za kinga...
Yuko sawa Bishopu...

Back
Top Bottom