Askofu Bagonza: ATCL imekosa aibu, basi iwe na huruma

Askofu Bagonza: ATCL imekosa aibu, basi iwe na huruma

Hiyo management ibadilishwe ikibidi serikali itangaze nafasi ya ajira aje mwenye kujielewa aendeshe hilo shirika, walilazimisha kulifufua kwa kuongeza ndege mpya lakini litakufa tena kwa kuwa na uongozi mbovu.
Kama Mkurugenzi haheshimiwi na maamuzi atakayotoa pia hayataheshimiwa! Raisi anapanda ndege ya abiria only in Tanzania vituko haviishagi!

Kwanini wasiweke order ya private jets mbona ni bei ndogo kuliko hilo li bombadier la billions of money? Jets zinaanzia 10 billion TZS unapata ila kinachoshindikana sijui ni kitu gani mpaka raisi atembelee ndege ya 300B peke yake na walinzi wake
 
Hili shilika ni kama zombie,a walking dead,CEO wake ni kilaza,sijuhi kwa nini serikali Bado inanunua Ndege kwa mapesa Mengi!inawezaka likawa shinikizo la wazungu kutufanya soko la Ndege zao,Ili viwanda vyao viendelee.
10% ndo sababu viongozi wanalazimisha wanunue ndege cash ili wachukue Chao mapema
 
ATCL Imekosa Aibu basi Iwe na Huruma

Ndani ya miezi miwili nikisafiri na ndege za ATCL nimeona haya:

1. Nilishindwa kuhudhuria mazishi ya ndugu na kukaa airport siku nzima

2. Nilishinda uwanjani Dar na kuondoka usiku wa manane siku ya pili.

3. Nilikosa connection ya ndege Dar baada ya ndege kutoka Mwanza kuchelewa kufika

4.Leo nimekesha uwanjani Mwanza (tangu saa Moja jioni Hadi saa 9 alfajiri).

Nashauri kirefu cha ATC kiwe:
"Any Time Cancellation" (ATC).

Tunatia aibu mbele ya wageni.

Pia soma: ATCL yatoa ufafanuzi kuvurugika kwa ratiba za ndege zake, yasema nyingi zilikuwa kwenye matengenezo makubwa!
View attachment 1899014
Hayo ni matunda ya fikra zisizoona mbali kwa kisingizio cha uzalendo, na kuona kujimilikisha soko badala ya kuruhusu ushindani, matokeo yake ni kujenga ugoigoi, uvivu na uzembe katika kufanya kazi.
 
Shirika linaendeshwa kienyeji, no professionalism at all.
Sababu kuu ya cancellations zisizo na kichwa wala miguu, ni kwamba, fleet zilizopo zipo busy na kuwazungusha watawala badala ya kuwahudumia wananchi.

Rais, Makamo wake, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Makamo wa Rais Zanzibar watumie ndege za serikali, ndege za ATCL za abiria zitumike kubebea abiria.

Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza
Kikwete hakuwa Fala, alivosema tukiruhusu kila kitu kutufanyia polisi Ccm na serikali tutakua tumekwisha kabisa. Haya ndo matokeo yake mkuu
 
Siku hizi Gulfstream haifanyi kazi ya kumbeba rais tena, kadri nilivyoona, safari zote za rais anatumia Airbus 220-300 inayobeba abiria 160; je rais huwa anasafiri na ujumbe mkubwa hivyo kama siyo matumizi mabaya ya ndege? Rais akichukua Airbus moja na Makamu wa Rais akachukua Airbus nyingine, basi ATCL inabaki haina ndege ya kubeba abiria wa kawaida.

Kuhusu matengezeo, hilo ni jambo jema lakini bahati mbaya ndege zinakwenda matengezo kwa sababu ya kutumika vibaya. Ndege zina matengezo ya aina mbili kuu. Matenegezo madogo ya A-Check hufanyika baada ya ndege kuruka masaa 400 mpaka 600, halafu matengenezo makubwa C-Check hufanyika baada ya ndege kuruka masaa 3000- Matengenezo ya B-Check na D-Chek yamo ndani ya hizo mbili. Tatizo la ATC mpaka sasa ni kuwa ndege inaruka masaa mengi kwa safari za viongozi tu badala ya kufanya safari za biashara. Kwa hiyo wanapozipeleka maintenance, inakuwa ni kwa sababu ya safari ambazo hazikuingiza mapato yoyote. Ni afadhali viongozi wabaki na Gulfstream tu, halafu hizi nyingine wawaachie abria wa kawaida.
 
BADO WANAONGEZA NDEGE KWA SHIRIKA AMBALO LINAJIENDESHA KIHASARA
 
Naona wengi tunalaumu kuhusu ubora wa ndege zetu eti ndio unasababisha hiyo Any Time Cancellations (ATC) to me sidhani kama hiyo ndio sababu, ukweli ni hu, watendaji almost wote wa serikali hawana uwezo wa ku run biashara, tusidanganyane, TTCL inafanyaje kazi, vivuko vyetu vinafanyaje kazi, fikiria kinacho endelea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hasa PSPF (sijui ndio hivyo ) how comes mfanyakazi anastaafu leo halafu anasubiri zaidi ya miezi 18 ndio alipwe mafao yake? Ukweli hakuna watu wazembe nchi hi kama watendaji wa serikali. Mbona Precision haina matatizo ya kubadiri ratiba zao? Nashauri kama kweli tunataka ATC ifanye kazi zake vizuri, tufanye either of the following, tubinafsishe management yake au tuzikodishe hizo ndege hata kwa FastJet, nje ya hapo ATC sio salama kuitegemea kama una safari za kidharula au kama unataka kuunganisha safari. Next week nilikua na safari to somewhere, jamaa zangu kazini wamenishauri nisi book na ATC, nisafiri na shirika lingine, imagine hali ndio iko hivyo. Halafu mtendaji mkuu jana anaongea kwa kujiamini kabisa as if ni sawa tu kubadirisha ratiba hovyo hovyo, hivi hajui ni kwanini mtu ameamua ku book ndege ya muda fulani? Very sad. RIP Magufuli, haya mambo hayakuwepo enzi zake.
 
Hilo la kwanza lakini pia huo utetezi unazusha maswali mengi zaidi.. Hivi zinaenda normal service au 'matengenezo makubwa'?
Je zile tuhuma kwamba tuliuziwa mitumba ni za kweli?
Service za bombadia mbili zilitugharimu zaidi ya shilingi bilion 12 vipi haya madege makubwa na matengenezo makubwa?

Mungu anakuona huko uliko kayafa!
Na msemaji mkuu wa Serikali kasema kwa kujiamini kabisa jana kuwa wako kwenye mpango wa kununua Dream liner nyingine mbili!!

Maamuzi mengine yanatia kichefu chefu.
 
Je tulipokuwa tunanunua mijindege cash kwa mkupuo, hatukuwaza kuwa zitaenda kwa mkupuo kwenye matengenezo makubwa?
Tatizo la nchi yetu ni Uongozi wa Juu kutokana na Katiba mbovu tulionayo. Kiongozi Mkuu anaweza kufanya lolote wakati wote bila kushauriwa/kushauriana na mtu yeyote.

Katiba mpya ndiyo mwarobaini wa haya yote. "MBOWE SIO GAIDI"
 
Shirika linaendeshwa kienyeji, no professionalism at all.
Sababu kuu ya cancellations zisizo na kichwa wala miguu, ni kwamba, fleet zilizopo zipo busy na kuwazungusha watawala badala ya kuwahudumia wananchi.

Rais, Makamo wake, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Makamo wa Rais Zanzibar watumie ndege za serikali, ndege za ATCL za abiria zitumike kubebea abiria.

Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza
Siyo kienyeji kijinga
 
Back
Top Bottom