Askofu Bagonza: Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa Umma!

Askofu Bagonza: Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa Umma!

nimewapeni mbinu,2025 mkamtukane jukwaani kwamba alikiwa fisadi,muuaji,na alibana haku zote.
mtagundua jambo jipya.

Hizo mbinu ungewapa ccm ili iache kutegemea vyombo vya dola kubaki madarakani.
 
Ukweli gani mkuu? Ivi kweli wewe unathibitisha hayati Magufuli alikuwa kichaa? Ivi post yakuwa mkuu wa nchi mnaichukuliaje wakuu...yani nyie vichaa hamkutani nao uko street zenu? Tuache zihaka na dhambi!!!!'' hata wewe ukiwa jua wapo watakao kusema kwa mazuri na wapo watao sema kwa mabaya ila kwenye kukuita ulikuwa kichaa na haukuwa mimi nikiwa rafiki yako nanikasikia mtu kakuita kichaa wakati mimi najua haukuwa kichaa uyo kaumia... R.I.P JOHN MAGUFULI

Sent using Jamii Forums mobile app

Post ya Mkuu wa nchi inapaswa kuwa sensitive sana, ila kinachoendelea hapa nchini kwetu ni tofauti kabisa. Usitake kutufanya tuone kuna umakini mkubwa sana kumpata rais wa nchi hii. Kama kungekuwa na umakini wa hivyo, JK na Magufuli wasingeweza kuwa marais wa Nchi hii. Nadhani kwako ukichaa ni mpaka mtu avae makopo shingoni na kiwa kichaa. Hivi kiongozi anayeagiza kupambana na Corona kwa kuweka kibanda cha kujifukiza ushirikina, kwenye hospitali kubwa ya taifa bila scientific proof, unautetea vipi ukichaa wake? Nenda leo hapo Muhimbili kama kile kibanda kama bado kipo.
 
Mtu keshakufa ila bado anaendelea kusemwa kama vile bado yupo hai, hiyo sasa ni chuki.

Hitler, Mussolin nk wamekufa zamani lakini bado wanasemwa mpaka leo, itakuwa huyo wa juzi? Isitoshe hakuna anayekulazimisha umseme, acha wanaotaka wamseme, ili kuepusha huko mbele nchi kuangukia kwa kiongozi mwingine muovu tena.
 
INAFIKIRISHA! INASUTA! TUSUTIKE

Nilipochaguliwa kuwa Askofu baada ya wanaofaa kukosekana, marafiki zangu waliandaa tafrija ya kuniaga huko Chicago, Marekani. Mmoja wa watani wangu akatoa hotuba na kusema "Benson, wewe sasa ni Askofu. Tangu sasa una uhakika wa mambo matatu:

1. Daima utakula chakula kizuri
2. Daima utavaa vizuri
3. Daima hutaambiwa ukweli.

Ni miaka 19 tangu niambiwe na yote nimeyaona. Ufafanuzi wa niliyoyaona nitaufanya siku nyingine. Kimsingi Viongozi katika jamii tunaishi kwa kujidanganya, kudanganya na kudanganya.
Leo Nina hili:

Comrade Anthony Diallo amesema maneno mazito. Ametimiza ahadi ya mwana TANU/CCM isemayo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Ukweli uliochelewa ni bora kuliko uwongo uliowahi.

Nitoe ushauri ufuatao:

1. Viongozi na watawala wetu kama hawawezi kuzuia kusifiwasifiwa basi angalau wanune wakisifiwa.

2. Waliokwishamaliza muda wa uongozi wasijengewe masanamu au kutangazwa ni watakatifu mpaka muda maalum upite.

3. Ikithibitika kuwa kiongozi wa umma ngazi yeyote amewahi kuwa na tatizo la afya akili, maamuzi yake yote yatenguliwe.

4. Walioathirika au kunufaika na maamuzi ya kiongozi mwenye tatizo la afya ya akili wajulikane na kusaidiwa.

5. Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa umma hadharani au kupendekeza ukiukwaji wa Katiba. Kuwasifia iwe sawa na kuwakashifu. Anayetaka kumsifia au kumkashifu kiongozi amwandikie barua binafsi. Kusifia hadharani ni rushwa.

6. Iwe marufuku wananchi kuwapigia makofi viongozi au kuwachezea ngoma, badala yake Viongozi wawapigie makofi wananchi na kuwachezea ngoma. Waliomba kutumwa, makofi ni ya nini?

Haya yote yanasisitiza msimamo wangu wa TUSUBIRI KUPONGEZA WALA KULAUMU.

Tangu enzi ya Mwalimu mpaka Samia, wanajitokeza watu wa kushinikiza kuvunja katiba ili Viongozi waongezewe muda wa kutawala. Wakiishakufa ndipo tunaanza kuambiwa mambo mazito yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.

INAFIKIRISHA, INASUTA, TUSUTIKE.

View attachment 1848441
Dialo ameomba radhi
 
Hitler, Mussolin nk wamekufa zamani lakini bado wanasemwa mpaka leo, itakuwa huyo wa juzi? Isitoshe hakuna anayekulazimisha umseme, acha wanaotaka wamseme, ili kuepusha huko mbele nchi kuangukia kwa kiongozi mwingine muovu tena.

wewe huna uwezo wa kuamua nchi apewe nani.

kwani ni mali ya watu fulani pekee hii??una uhakika gani kama unayemwaminini ni mzima kichwani!!!

hitler na mussolin ni viongozi waovu kwa kila binaadamu goi goi na mpenda kitonga,kwa wanaume shupavu wale ni mfano wa kuigwa.
hii dunia ingebaki na wapenda kitonga milele isingekuwa ilipo leo hii,nawewe unajua.
 
f
Kumfananisha Mwendazake na Nyerere ndio wendawazimu aliousema Dialo Jana
Siku zote unapofananisha unaeleza vinavyofanana kwa hivyo unavyovifananisha na ndio maana nimeeleza nimewafananisha kwa lipi, sasa kama wewe umeangalia meno ya Nyerere ya yaliyokuwa yamechongeka ukaona hayafanani na meno ya Magufuli basi hapo kweli unaweza kusema hawafanani.

Wote wanazungumziwa hadi sasa na wote wanasemwa kwa mazuri na mabaya, tatizo unafikiri watu wote wanamchukulia Nyerere kama unavyomchukulia wewe.
 
1.Nadhani Dialo analipa kisasi kimtindo....anamkomoa marehem. Hatari sana.
2. Kwa wale wakazi wa Dodoma wanajua yakua Mirembe hawatibu magonjwa ya akili tu!
Hivo kua na faili Mirembe haimaanishi ugonjwa wa akili.

3. Ikitokea mtu mmoja katika jamii flan akawa na akili Sana, genius, na akaamua kua mzalendo na kuiongoza, Basi wakwapuaji na sehemu ya jamii ambao ni wajanja wajanja wataumia
Mwisho!!
Kama haya ninayo yaona mabarabara Hadi Mbamba bay huko, Ludewa Makete, sikonge huko, Ma SGR, Li Stiglers Gorge, Majizi na majambazi kukomeshwa, Mavivu serikali kukomeshwa, Mabeberu kutii amri, Tanzanite yetu Ndege zetu na mengine mengi.........

Kama kweli yote hayo yaliletwa na kichaa, basi nashauri 2025 turudi Mirembe tukatafute kichaa mwingine atuongoze Ili tupate maendeleo ya Chap-kwa -Haraka.

Lala salama Rais mzalendo
 
Hitler, Mussolin nk wamekufa zamani lakini bado wanasemwa mpaka leo, itakuwa huyo wa juzi? Isitoshe hakuna anayekulazimisha umseme, acha wanaotaka wamseme, ili kuepusha huko mbele nchi kuangukia kwa kiongozi mwingine muovu tena.
Na ndio nimesema hiyo ni chuki na si kitu chengine, tatizo hapa hamkubali kwamba wengi kinachowasumbua ni ile chuki mliyonayo kwa Mwendazake na ndio kinachowafanya mtowe haya mapovu yote mnaongea hata yale ambayo ni mambo binafsi ya huyo Mwendazake, sasa ni chuki ndio yenye kuweza kufanya mambo hayo na si vinginevyo.

Yani watu wanahasira zao binafsi dhidi ya Mwendazake ndio hujifanya wanakosoa kumbe ndio hupunguza hasira zao humo kwa michuki waliyonayo.
 
Kama ulikuwa hujui ndiyo ujue kwamba yule dhalimu mwendazake alikuwa mwendawazimu na siyo siri. Uwe unafuatilia habari za yanayojiri nchini kwa ukaribu badala ya KUKURUPUKA na kuanza ubishi wa kijinga. Na zihaka ndiyo mdudu gani!?

Ukweli gani mkuu? Ivi kweli wewe unathibitisha hayati Magufuli alikuwa kichaa? Ivi post yakuwa mkuu wa nchi mnaichukuliaje wakuu...yani nyie vichaa hamkutani nao uko street zenu? Tuache zihaka na dhambi!!!!'' hata wewe ukiwa jua wapo watakao kusema kwa mazuri na wapo watao sema kwa mabaya ila kwenye kukuita ulikuwa kichaa na haukuwa mimi nikiwa rafiki yako nanikasikia mtu kakuita kichaa wakati mimi najua haukuwa kichaa uyo kaumia... R.I.P JOHN MAGUFULI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe huna uwezo wa kuamua nchi apewe nani.

kwani ni mali ya watu fulani pekee hii??una uhakika gani kama unayemwaminini ni mzima kichwani!!!

hitler na mussolin ni viongozi waovu kwa kila binaadamu goi goi na mpenda kitonga,kwa wanaume shupavu wale ni mfano wa kuigwa.
hii dunia ingebaki na wapenda kitonga milele isingekuwa ilipo leo hii,nawewe unajua.

Hitler,Mussolin na waovu wengine wa aina hiyo hawapo, mbona dunia bado inapaa tu kwa maendeleo ya hali ya juu?
 
Na ndio nimesema hiyo ni chuki na si kitu chengine, tatizo hapa hamkubali kwamba wengi kinachowasumbua ni ile chuki mliyonayo kwa Mwendazake na ndio kinachowafanya mtowe haya mapovu yote mnaongea hata yale ambayo ni mambo binafsi ya huyo Mwendazake, sasa ni chuki ndio yenye kuweza kufanya mambo hayo na si vinginevyo.

Yani watu wanahasira zao binafsi dhidi ya Mwendazake ndio hujifanya wanakosoa kumbe ndio hupunguza hasira zao humo kwa michuki waliyonayo.

Hivi unadhani hatujui ipi ni chuki binafsi na upi ni ukweli hasi kuhusu yule dhalimu? Sema cha uongo alichokisema Diallo juzi ili tupime chuki yake dhidi ya huyo dhalimu. Ama unadhani dhalimu kufariki ndio kinga ya chuki aliyoeneza ndani ya nchi hii kunyamaziwa?
 
Back
Top Bottom