Askofu Bagonza: Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

KUNA MAMBO HAYAKO SAWA

Kuna mambo yanayotuunganisha wote bila kujali itikadi, dini, jinsia, kabila, hali ya mtu kiuchumi, ufupi au urefu wa mtu kama mimi. Haya yote yanaunganishwa na neno HAKI au kwa Kijaluo JUSTICE.

Kuna mambo 10 hayako sawa kwa sababu:

1. Hivi sasa, Mtu anapozungumzia HAKI, anatazamwa yeye ni dini gani badala ya kusikiliza anaongea nini!

2. Mtu akiongelea HAKI anatazamwa ni wa chama gani badala ya kusikiliza anaongea nini?

3. Mtu akilalamika amepotelewa na nduguye, anaambiwa anavuruga amani.

4. Mbuzi akipotea anapatikana lakini mtu akipotea hapatikani.

5. Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani.

6. Kutumia dini kueneza siasa ni dhambi lakini kutumia siasa kueneza dini ni sawa tu.

7. Kumsifu mtu akifanya vizuri inapendeza, lakini kumkosoa akikosea ni sawa na kumdai marehemu kabla hajazikwa.

8. Yaonekana kuna dini inayohubiri amani bila kuhubiri HAKI na kuna dini “inajifanya”kuhubiri HAKI bila kuhubiri amani. Mimba ya HAKI ni amani lakini AMANI bila HAKI ni tasa.

9. TUMEGAWANYIKA: Wapo wanaoona mtutu wa bunduki unavuruga amani. Na wapo wanaoona mtutu wa bunduki unatunza amani. Msuluhishi wa kweli anaitwa HAKI.

10. Rais ni wetu sote. Anaongoza wapenda HAKI na wapenda AMANI. Hatuna shaka na mahaba yake kwa AMANI. Wapenda HAKI wanasikia baridi. Tulimsikia akiapa kuongoza kwa HAKI. Bahati njema, HAKI ilimbeba. A
kiibeba kama ilivyombeba, AMANI itafurika kama Bwawa la Mwalimu Nyerere. HAKI na AMANI vipeane busu.

Hekima ya Wajaluo: Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma.
1743486629591.jpg
 
View attachment 3289378
Facts
 
Askofu Bagonza ulipinga ujenzi wa bwawa la mwl Nyerere kwa hiyo huna legitimacy yoyote ya kukaa unalitajataja
 
Sijawahi kuzielewa kofia za huyu Askofu
1743490006972.png
 
Jinsi ya kujibu hoja za Askofu :

1. Sio Mtanzania.
2. Anatumiwa na mabeberu.
3. Mdini.
4. Mchochezi.
5. Kibaraka wa Lissu.
6. .....

Kuna mwingine hapo juu kasema hajwahi kuielewa kofia ya huyu Askofu, tunaweza tukaiongezea namba sita hapo.
 
Back
Top Bottom